Katavi: Wananchi wa Mishamo waomba kuwekewa minara ya simu, mawasiliano ya Radio

Katavi: Wananchi wa Mishamo waomba kuwekewa minara ya simu, mawasiliano ya Radio

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Baadhi ya wananchi kutoka katika vijiji tofauti tofauti katika makazi ya Mishamo mkoani Katavi katika wilaya ya Tanganyika, wanakosa huduma muhimu za mawasiliano ya Radio na simu.

Wanakijiji hao kutoka katika vijiji vya Mgansa, Isubangala, Bujombe na vijiji vingine jirani wamekuwa wakikosa huduma hiyo muhimu ya mawasiliano ya Radio na simu kwa muda mrefu hivyo kulazimika kusafiri kwenda kijiji chenye kushika mawasiliano kwa ajili ya kupata huduma ya kuongea na simu.

Viongozi wa vijiji hivyo wamesema wamekuwa wakipata shida hiyo ya mawasiliano katika vijiji vyao kwa muda mrefu kwani licha ya kwamba minara ya simu ipo mbali lakini pia hawapati mawimbi ya Radio kabisa na hivyo kukosa huduma muhimu za matangazo ya Habari, na mambo mengine yanayoendelea Dunia.
 
Hapo kwenye BUJOMBE nadhani umemaanisha BUSONGORA!!
 
Katente mwese lugonesi kasekeae kayenze Ikola nk Mpanda hoyeee
 
Back
Top Bottom