GE2025 Katavi: Wananchi waibana CHAUMMA kwa maswali magumu. Mtalindaje kura?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) mkoani Katavi kimewatoa wasiwasi wananchi wa Kata ya Kakese, Manispaa ya Mpanda, kuhusu usalama wa kura zao kwenye uchaguzi mkuu ujao, kikiahidi kuwa na mikakati madhubuti ya kuzilinda ingawa hakijaweka wazi mbinu hizo kwa sasa.

Kauli hiyo imetolewa siku ya Jumatano na Mwenyekiti wa CHAUMMA Mkoa wa Katavi, Almas Ntije, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kakese, ambapo wananchi walitaka kujua kwa kina namna chama hicho kitapambana na wizi wa kura ambao umekuwa ukilalamikiwa na vyama mbalimbali vya siasa.

Mathias Kashinje, mmoja wa wananchi waliohoji, alisema: "Tumekuwa tunapiga kura lakini mnasema zikiibiwa mtamuachia Mungu. Je, tunampigia Mungu au tunachagua viongozi? Sisi wananchi tufanyeje kulinda kura zetu?"

Akijibu, Almas Ntije alisema: “Hatutatoa wazi mikakati yetu ya kulinda kura kwa sababu hiyo ni siri ya chama, lakini tunawaomba wananchi watuamini – tutazilinda kura.”

Wananchi wanataka waambiwe namna ya kulinda kura zao? Safari kweli bado ni ndefu.

Amandla...
 
Watakaoshiriki hakuna cha kulinda kura wala nini?..ni wanaenda kuhalalisha wizi wa kura..kwa kifupi ni CCM B hao
 
Kwa nini tulinde kura? Kwa nini yasitengenezwe mazingira ambapo kila mtu akipiga ana uhakika kwamba matokeo hayatabalishwa? Kwa nini turuhusu mfumo wa vyama vingi lakini vigezo na masharti ni ya chama kimoja?
 
CHAUMA wahuni hao, wana makubaliano ya CCM ili waachiwe majimbo ya Ubunge na Udiwani ili ku justify uchaguzi mkuu- hamna chama humo. Kundi la wanyamganyi.
 
Back
Top Bottom