Katavi: Watumishi 4 wasimamishwa kwa Ubadhirifu wa Tsh. Milioni 300 za Ujenzi wa Hospitali

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko, ameagiza kusimamishwa kazi kwa watumishi wanne walioiingizia serikali hasara ya shilingi milioni 300, kwa kujenga majengo ya hospitali ya wilaya ya Nsimbo chini ya kiwango na fedha zingine kutokujulikana matumizi yake.

Mrindoko amefikia hatua hiyo baada ya kukagua mradi huo na kubaini ubadhirifu huo huku ikimlazimu kuamuru wasimamishwe kazi Mhandisi wa wilaya, Afisa Mipango na Mkuu wa Idara ya Afya pamoja na Mkaguzi wa ndani ili kupisha uchunguzi.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mohamed Ramadhani na watumishi wake wa idara wameonesha kutokuwa na uelewa sawa juu ya fedha hizo ,wengine wakidai hawana taarifa na fedha hizo na wengine wakidai ilipelekwa kutekeleza mradi mwingine.

Mhe. Mrindoko ametoa siku saba kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za ndani mkoa wa Katavi kufuatilia taarifa za fedha hizo na ndani ya mwezi apate ripoti ikiwa ni pamoja na TAKUKURU kuchunguza mradi huo

Chanzo: East Africa Tv
 
Shida ni kuwa wanasimamisha watumishi, uchunguzi unafanyika lakini hatima ya hao watumishi hatuambiwi Wana nchi. Ilitakiwa tutaarifiwe mwisho wa hilo sakata.
 
Kuna jamaa angu hapo alikufa ghafla alikua clerk of work sijui walimfanya nn
 
Shida ni kuwa wanasimamisha watumishi, uchunguzi unafanyika lakini hatima ya hao watumishi hatuambiwi Wana nchi. Ilitakiwa tutaarifiwe mwisho wa hilo sakata.
Shida ni kwamba chini ya utaratib huu mpya wa force account, watumishi walimu au madaktar wanaambiwa wasimamie ujenzi sasa ikitokea tatizo wanachukuliwa hatua ipi wakati hawajasomea ujenzi wala hawajaariwa kusimamia ujenzi. Majengo mengi ambayo inasemekana yapo chini ya kiwango sio kwamba kamati imekula hela Ila ni uelewa mdogo wa ujenzi. Na muda mwingine kutaka kubana matumiz ili hela itoshe kunaleta ubovu wa majengo. Majengo mengi siku hizo serikali inaleta hela pungufu isiyoendana na gharama za ujenzi
 
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko, ameagiza kusimamishwa kazi kwa watumishi wanne walioiingizia serikali hasara ya shilingi milioni 300, kwa kujenga majengo ya hospitali ya wilaya ya Nsimbo chini ya kiwango na fedha zingine kutokujulikana matumizi yake.

Mrindoko amefikia hatua hiyo baada ya kukagua mradi huo na kubaini ubadhirifu huo huku ikimlazimu kuamuru wasimamishwe kazi Mhandisi wa wilaya, Afisa Mipango na Mkuu wa Idara ya Afya pamoja na Mkaguzi wa ndani ili kupisha uchunguzi.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mohamed Ramadhani na watumishi wake wa idara wameonesha kutokuwa na uelewa sawa juu ya fedha hizo ,wengine wakidai hawana taarifa na fedha hizo na wengine wakidai ilipelekwa kutekeleza mradi mwingine.

Mhe. Mrindoko ametoa siku saba kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za ndani mkoa wa Katavi kufuatilia taarifa za fedha hizo na ndani ya mwezi apate ripoti ikiwa ni pamoja na TAKUKURU kuchunguza mradi huo

Chanzo: East Africa Tv
 
Attachments

  • 65045ACE-B7E1-416C-AE3C-2F6AEBDB4262.jpeg
    65045ACE-B7E1-416C-AE3C-2F6AEBDB4262.jpeg
    2.3 KB · Views: 9
  • 02548B08-32C9-4BE1-B464-47A43A166F9C.jpeg
    02548B08-32C9-4BE1-B464-47A43A166F9C.jpeg
    60.7 KB · Views: 7
Shida ni kuwa wanasimamisha watumishi, uchunguzi unafanyika lakini hatima ya hao watumishi hatuambiwi Wana nchi. Ilitakiwa tutaarifiwe mwisho wa hilo sakata.
Inashangaza sana
 
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko, ameagiza kusimamishwa kazi kwa watumishi wanne walioiingizia serikali hasara ya shilingi milioni 300, kwa kujenga majengo ya hospitali ya wilaya ya Nsimbo chini ya kiwango na fedha zingine kutokujulikana matumizi yake.

Mrindoko amefikia hatua hiyo baada ya kukagua mradi huo na kubaini ubadhirifu huo huku ikimlazimu kuamuru wasimamishwe kazi Mhandisi wa wilaya, Afisa Mipango na Mkuu wa Idara ya Afya pamoja na Mkaguzi wa ndani ili kupisha uchunguzi.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mohamed Ramadhani na watumishi wake wa idara wameonesha kutokuwa na uelewa sawa juu ya fedha hizo ,wengine wakidai hawana taarifa na fedha hizo na wengine wakidai ilipelekwa kutekeleza mradi mwingine.

Mhe. Mrindoko ametoa siku saba kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za ndani mkoa wa Katavi kufuatilia taarifa za fedha hizo na ndani ya mwezi apate ripoti ikiwa ni pamoja na TAKUKURU kuchunguza mradi huo

Chanzo: East Africa Tv
Inakuaje Mkurugenzi asielewe chochote kilichokuwa kinaendelea?

Achunguzwe nae.
 
Bi Tozo anazurura, wajanja home wanajisevia tu

safi sana
 
Back
Top Bottom