Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Mwalimu Nyerere aliwahi kunukuliwa miaka kadhaa iliyopita akitamka kwamba " CHAMA CHA SIASA NI MABARABARANI NA MAJUKWAANI " hapa alimaanisha kwamba Uhai wa Chama chochote cha siasa unategemea na harakati za kisiasa za chama husika kwa kunadi sera zake hadharani kwa wananchi kwa kutumia maandamano na Majukwaa halali ya kisiasa , hii maana yake ni kupiga mikutano ya hadhara nchi nzima bila masharti kama ilivyokuwa awali .
Tukitaka kuirejesha nchi yetu heshima yake iliyopotea kwa miaka zaidi ya 6 ni lazima turudishe demokrasia ya vyama vingi kama ilivyoainishwa ndani ya katiba ya nchi , turuhusu wanaotaka kuanzisha vyama vingine vipya vya siasa waingie mabarabarani na majukwaani kusaka wanachama 200 kwenye mikoa iliyoainishwa bara na visiwani , hatuna haja ya kuogopa , hiyo ndio Demokrasia yenyewe .
Mzee Kikwete aliwahi kunukuliwa akitamka maneno haya hapa chini .