Kati ya AS VITA na Florian Ibenge nani kaisha ?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Uwezo wa timu ya soka ya DRC ya AS VITA bila shaka umefikia kikomo , hawana jipya wala hawana uwezo tena wa kufanya lolote kwenye soka la Vilabu barani Africa , nimeifuatilia timu hiu kwenye game zote za club bingwa africa zinazoendelea , hii timu imekwisha .

Sasa swali langu ni hili , imekwisha AS VITA au kaisha Ibenge ?
 
kundi la as vital lote linacheza kabumbu kwa maana ya mpira wa kipumbavu na sio soka kwa maana ya mpira wa maana
 
Ungetuambia mafanikio waliyopata kabla hawajaisha?
 
Uzi wa kujifariji
 
Kwanini usiseme timu walizokutana nazo ndo zimekuwa bora zaidi tofauti na miaka ya nyuma.

Watanzania huwa tunakuwa vigeugeu sana.Kabla ya mechi ya jana,Wapenzi na washabiki tulikuwa tunaomba tupate hata droo tu japo nayo hatukuwa na uhakika nayo baada ya kuona as vita walivyocheza kule misri.

Vijana wamefanya kazi nzuri,wapongezwe na sio kwamba As vita ni wabaya, kabla mechi kuanza nani angetabiri Simba kufunga goli 4.

YOTE KWA YOTE,kocha ni fundi sana,angekuwa yule siju van nini aliyeondoka muda huu tungekuwa nafasi ya 3 au 4.

Simba au Al ahly kwa jinsi walivyocheza sio timu mbaya hata kidogo,ukuta wa kueleweka,winga nzuri katikati pazuri shida ni pale finishing kwa Mugalu.
 
AS Vita bado ni timu hatari sana, hapa nionacho ni kwamba watu hamtaki kukubali kwamba Simba imekuwa timu kali kabisa ikaipiku Vita. Kama ukisema Vita imeporomoka, basi useme tu timu zote Afrika zimeporomoka kasoro Simba
 
Timu ipo vizuri na Ibenge yupo vizuri pia ila ni zama tu zinapita.
Miaka mingi sisi timu za Tz huwa tunatolewa mashindanoni na timu za kongo na za waarabu lakini kwa sasa tumeanza kuzitoa sisi.
Nina imani hao waarabu wanaokutana na simba robo fainali hakuna namna lazima watolewe tu.
As Vital ni ya moto haijachuja ila timu nyingi zimeimprove zaidi kwa sasa ikiwemo simba.

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Vita haijaisha ila kundi la vita kuna timu moja inaitwa simba imeisha fika level ya vita na kuzidi, Mara nyingi tu hao vita wameishia group stage au confederation miaka ya karibuni lakini ni pale wanapokutana na mpinzani bora ndio huwa yanawakuta hayo.
 
Yaan nilivyo mtazama ibenge jana ni kama alikuwa anajutia nafasi aliyo pewa na simba nahisi usiku mzima alikuwa ana kumbukia siku aliyo kutana na Bimkubwa Barber Gonzalenzi yaan Ibenge alitepeta hamna cha mbinu wa mbanu kwanza tumwe wakosa makoli kama ma 4 ivi yaan jana walikuwa wafe si chini ya bqo 8
 
AS Vita bado ni timu hatari sana, hapa nionacho ni kwamba watu hamtaki kukubali kwamba Simba imekuwa timu kali kabisa ikaipiku Vita. Kama ukisema Vita imeporomoka, basi useme tu timu zote Afrika zimeporomoka kasoro Simba
Unakionaje na kiwango cha Soka cha timu ya Taifa ya Congo DRC
 
Yanga bwana ,basi Misri mpira umeisha ,Al ahly na Zamarek wanapigania nafasi ya Pili
 
Ninachoona pia ligi yetu imeongezeka ubora,yaani huu mpira waliocheza AS Vita hata wangekutana na timu kama Mtibwa au KMC bado hata kama ni kushinda wangeshinda kwa mateso makubwa
 
Ifike hatua tukubali tu kuwa ubora wa Simba umeongezeka mara dufu zaidi ya hao Vita Club na wapinzani wengine

Tukianza kusema ooh hao Vita wameuza wachezaji wao, basi tukumbuke hata hawa Simba wameondokewa na watu kama kina Okwi, Kotei, Haruna Niyonzima, Rashid Juma Mtabigwa, Zana Coulibaly nk ambao walikuwa muhimili muhimu ktk wakati wanawafunga Vita hapa kwa Mkapa na kutinga robo fainali.

Na kubwa zaidi Simba walishondokewa na Kocha Patrick Aussems ambae alikuwa nguzo muhimu kwa mafanikio ya Simba kufika robo finale
 
Kila timu itakayocheza na Simba kwa sasa itaonekana mbovu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…