Kwa tourism ngazi ya diploma ni bora tu usome IT, sababu kubwa tour guide hauhitaji diploma ili uwe favoured kwenye soko la ajira, kuna "machalii" wamejazana arusha mjini, moshi na mto wa mbu pale wana certificates tu za miezi sita mpaka mwaka, jumlisha na course za lugha mbalimbali na familiarity ya pori,
Hao huwezi kuwapata hata kwa kuwakimbilia sababu kubwa kwa tour guide haihitaji makaratasi sana, inataka uwe mzuri kwenye field (porini) i.e hata mtu asie na cheti cha darasa la saba anaweza kuwa local tour guide mzuri kukuzidi wewe wa diploma.
Kwa Tourism in general kama kusoma ni bora ukachukue degree (kama una vigezo) hapa utajipa uwanja mpana wa kuingia kwenye management zaidi.