Kwanza kabisa hakuna harrier 240 mkuu.
Kwenye swala la kubrand magari makampuni mengi hasa Toyota hutumia namba ambazo zinauhusiano na Ujazo (displacement) ya engine katika gari husika au aina ya combustion kama ni Diesel au Petrol. Pia hutumia trim codes kama VX, LX,GX,GL,SX n.k kutofautisha matoleo tofauti ya gari.
Lexus ni division (tawi) la Toyota linalotengeneza gari za aghali zaidi ila zenye manjonjo kwa ajili ya matajiri au wateja wanaopenda vitu vya kipekee.Hasa huyauza ulaya hayo magari. Trimcodes za Lexus ndio kama RX,RC,GS, LS,IS hutofautisha matoleo tofauti ya Lexus.
Mfano halisi:
Toyota Mark X utakuta imeandikwa nyuma 250G ama 300G! Ile namba 250 ni kifupisho cha displacement ya engine ama cc za gari ambazo ni 2500cc na ile G inawakilisha Gas (Petrol). Muda mwengine wanatumia herufi (i) kuwakilisha petrol. Kwa gari za diesel wanatumiaga (D). Kwahio kwa anaejua Nomenclature ya gari za Toyota direct anaelewa ile gari ni ya ukubwa flani bila kufungua bonnet.
Muda
Gari ya Lexus huwa wanaziandikaga trim code kisha namba.
Mfano:
Lexus IS250
ile IS inamaana yake nimesahau ila ni .....sedan yenye 2500cc
Zingine kama RX300 unakuta ni Lexus yenye ukubwa wa 3000cc.
Kuhusu kufanana kwa gari za Toyota na Lexus ni sawa kwa sababu mzalishaji ni mmoja ingawa kwa matoleo ya kisasa wamejitahidi kuzitofautisha kabisa. Unakuta Harrier ni gari ya soko la Japan ila gari hio hio wanaifanyia maboresho zaidi iendanw na soko la ulaya kisha kuipa sticker tofauti ya Lexus kisha inauzwa soko la ulaya kwa aghali zaidi. Ndio maana umeona zinafanana.
Harrier inaandikwa 240G kumaanisha ni gari ya 2400cc na ya petrol!
Lexus yake inaitwa RX350 au RX300