Kati ya Hawa wafuatao ni nani Rais ajaye wa Tanzania?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
2,471
Reaction score
3,768
Naamini hapa jf pana watu wenye uelewa na upeo mkubwa sana wa kuchanganua mambo.
Mawazo yanayotolewa hapa yanaweza kuvifungua macho vyama vya siasa juu ya nani wamsimamishe kama mgombea kutokana na kuonwa na macho ya wachambuzi wa mambo.
Ifuatayo ni orodha ya majina ya watu ambao wanafaa kufikiriwa na vyama vyao kwa ajili ya uteuzi wa kuwania urais wa Tanzania

1. Tundu Lissu
2. Zitto Kabwe
3. Sulemani Jafo
4. Mwigilu Nchemba
5. Freeman Mbowe
6. Luhaga Mpina
7. Mohammed Dewj.
8. Ummy Mwalimu.
9. Anthony Mtaka.
10. Magdalena Sakaya.

Haya ni baadhi ya majina ambayo vyama vinaweza kuanza kuya highlit.

Ni kwa bahati mbaya wanasiasa wengi toka Kambi ya upinzani sio maarufu miongoni mwa watanzania na wakati mwingine huwa vinachukua toka wale waliokwama CCM, ndio maana hata majina yao hapa sio mengi.
 
hakuna hata wa tano bora
 
Majaaliwa ndo muhusika mkuu,afu hujamweka katika orodha.Kweli nimeamin ajae hatotambulika kama ambavyo alikuwa hatambuliki magufuli
 
Hakuna hata mmoja hapo mwenye sifa ya kuwa Rais, huyo fala wa tozo za miamala ya simu anayejiita daktari wa kufanyiwa mitihani ndo kabisa hafai hata kuwa Mbunge
 
Ni mara kumi ya Dewji kulikoni Mbowe, Lisu na Zito. Hao ni wachumia tumbo mamb moja
 
do! kinywa changu na vidole vyangu koma! wako watu wanajipanga na wanatumia nguvu kubwa sana na muda huu wanakusanya fedha ili waweze kujenga uwezo wa kuwanunua wajumbe la watu wanawajua lakini kwa tamaa za wajumbe watawapitisha.
safari hii ni rushwa kwenda mbele nipe nikupe na wazee ambao angalau wanaweza kusimama japo kwa haki kidogo hawaonyeshi kushiriki kabisa!
 
Ondoa magaidi na genge lao wabaki wanasiasa hapo. Tutakuambia nani anafaa
 
Mbona simuoni Dr.Bashiru Ally Kakurwa au mnamuogopa ?🤣
 
Kama umewahi kufanya kazi Kampuni yeyote ya Mo ungeacha kabisa huu upambe..

Mtu analipa watu mishahara ya laki mbili ..
Unakuja kumpigia Debe urais?
Anataka mawaziri waanze kulipwa "seven hundred" watengeneze voice note wanalia🤣
 
Bora Antony Mtaka. Anaweza akatuvusha,
Mimi nikiwa waziri wake wa Ajira na Vijana.
 
2025 nitagombea kupitia CCM liwalo na liwe
Nalog off
 
Heri
Lukuvi na Simbachawene hao ndo long time mature and serious people CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…