Habari wakuu.
Kama kichwa kinavyojieleza, naomba kujua ni gari ipi nzuri kwa road trip na hata uimara kati ya hizi: Toyoya IST, Vitz na Belta.
Ushauri nitakaoupata hapa ni kwa niaba ya rafiki yangu ambaye ananuia kununua gari kati ya mojawapo.
Ametazama utumiaji wa mafuta, hautofautiani sana, na hata upande wa bei, si tofauti sana.
Jambo analoomba kusaidiwa kwa wale waliowahi kuzitumia gari hizi, je ni ipi ipo imara kuliko nyingine?
Kwa wale wanaopenda kukashifu, tafadhali, naomba mkae kwanza pembeni, tuwaachie watakaotoa ushauri.
Nitashukuru kwa msaada wenu