Kati ya IST, Vitz na Belta ipi bomba?

Kati ya IST, Vitz na Belta ipi bomba?

Aputwike

Senior Member
Joined
Aug 9, 2016
Posts
172
Reaction score
189
Habari wakuu.

Kama kichwa kinavyojieleza, naomba kujua ni gari ipi nzuri kwa road trip na hata uimara kati ya hizi: Toyoya IST, Vitz na Belta.

Ushauri nitakaoupata hapa ni kwa niaba ya rafiki yangu ambaye ananuia kununua gari kati ya mojawapo.

Ametazama utumiaji wa mafuta, hautofautiani sana, na hata upande wa bei, si tofauti sana.

Jambo analoomba kusaidiwa kwa wale waliowahi kuzitumia gari hizi, je ni ipi ipo imara kuliko nyingine?

Kwa wale wanaopenda kukashifu, tafadhali, naomba mkae kwanza pembeni, tuwaachie watakaotoa ushauri.

Nitashukuru kwa msaada wenu
 
Tupia budget ya “rafiki” yako, matumizi makuu kwa siku, mkoa alipo, ananunua yard, kwa mtu Tanzania au import?

By the way, hapo kwenye vyote iwekwe hivi:

IST>Vitz>Belta>Platz>Passo
 
Tupia Bugdet ya “Rafiki” yako, Matumizi makuu kwa siku, Mkoa alipo, Ananunua yard, kwa mtu TZ au import?

BTW Hapo kwenye vyote iwekwe hivi:

IST>Vitz>Belta>>>>>>>>>>>>>>>>>>>Platz>>>>>>>>Passsssso
Asante sana mkuu
 
Belta ina space ya kutosha Sana ndani na hata ukubwa wa engine ni mdogo kama ilivyo IST.
Kama vipi chukua hiyo IST ili mambo yasiwe mengi
 
Back
Top Bottom