JKT ni kamandi moja wapo ya JWTZ. JKT ni kamandi ya askari wa ziada(Reserves)
Safi mkuu short and clear.......JKT ni sehemu ya JWTZ.....
SHERIA YA KUANZISHWA KWA JESHI LA KUJENGA TAIFA NA MAREKEBISHO YAKE
Jeshi la Kujenga Taifa lilianzishwa kwa sheria ya ‘Nationa Service Act No 16' ya mwaka 1964. Sheria hii inatoa uwezo wa Jeshi la Kujenga Taifa kuandikisha vijana wa kulitumikia taifa. Aidha, sheria hii imeendelea kufanyiwa marekebisho kutokana na mahitajio, baadhi ya marekebisho hayo ni:-
a.
Marekebisho ya mwaka 1966
Tangu lilipoasisiwa JKT lilikuwa linaandikisha vijana wa kujitolea wenye elimu ya chini tu. Ilipofika mwaka 1966, ilionekana kuwa, kuna umuhimu wa vijana wasomi wenye elimu zaidi ya kidato cha nne kulitumikia JKT. Hivyo, sheria ilirekebishwa ili kulipa JKT nguvu za kisheria ili liweze kuandikisha vijana wenye taaluma zaidi ya kidato cha nne kwa mujibu wa sheria (Compulsory service).
b. Marekebisho mengine ni ya mwaka 1975 wakati JKT lilipounganishwa rasmi na JWTZ, hivyo kulifanya JKT kuwa moja ya Kamandi zilizo chini ya JWTZ. Sambamba na marekebisho hayo, shughuli za JKT ziliwekwa bayana kuwa ni:-
(1) Kuwafundisha vijana wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulitumikia Taifa katika nyanja za
kijamii, maendeleo ya uchumi na ulinzi wa Taifa.
(2) Kutoa mafunzo ya msingi ya Jeshi kwa vijana kwa lengo la kuwawezesha vijana hao kufikia sifa
ya kujiunga katika vyombo vya Ulinzi na Usalama kama JWTZ, Polisi, Usalama wa Taifa na Magereza.
(3) Kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa Taifa.