Kati ya Kahama na Morogoro wapi panafaa kuishi kwa mtu anayeanza maisha?

Kati ya Kahama na Morogoro wapi panafaa kuishi kwa mtu anayeanza maisha?

Popconi

New Member
Joined
Nov 5, 2022
Posts
2
Reaction score
1
Habari wana jukwaa,

Naomba kwa mwenye uzoefu na hizi manispaa mbili, Kahama na Morogoro, wapi panafaa kuishi kwa mtu anaeanza maisha mwenye kipato cha kati? Yaani mtumishi wa serikali.
 
Morogoro
Nimekaa hapo miaka miwili
Gharama za maisha ni nafuu
Vyakula bei ni nafuu na pia vipo kwa wingi
Usafiri pia hauna changamoto kubwa kuanzia Bajaj, bodaboda na daladala
Makazi kodi ni za kawaida kuanzia 50000 unapata pa kujisitiri vizuri tu
Ukitaka kwenda kupoza mwili, sehemu Zipo
Pia ni njia kuu ya kwenda mikoani na nje ya nchi
Nenda Morogoro.
 
Mimi nahisi inategemeana na upambanaji wako nje ya hicho "kipato".
Moro maisha yko very cheap lakini mzunguko wa fedha kias chake sio mkubwa (kutegemeana na eneo).
Kahama gharama ya maisha iko juu but mzunguko ni mkubwa all year round.
So inategemeana na njaro zako mkuu. Kama wewe n wale wa kukumbatia mshahara, chap kwa haraka nenda mji kasoro bahari.
Kama wewe ni wale wa kumeza bomu, usingoje nenda kahama.
Kama nmekosea sehem nakubali kusahihishwa
 
Yes mkuu
Kuna star park, terminal pub bila kumsahau kubwa la maadui aka kwa sheyani samaki samaki
Pia Kuna mto mawe, rock garden kwa wale wapenda utulivu, unaenda kutuliza akili na mwili huku unavuta hewa Safi, jioni unaenda kula kuku choma pale kwa wahindi Safi kabisa
Yes, Moro is one of the best places to stay based on my opinions.
Sijawahi fika kahama
Nipo Mpanda huku Sasa hv, naona utofauti mkubwa sana

,
 
Kama ni mwajiriwa na unapenda boashara nenda kahama.
Mzunguko wa pesa mkubwa sana
Wafanyabiashara wanasema kahama kuna pesa
 
Nenda kahama kwa mtafutaji pale rahisi kutoka mzunguko wa pesa upo karibu mwaka mzima, na biashara za kahama hata mtaji mdogo unaweza kuanza nao na ukafanya vizuri, Morogoro mzunguko wa pesa wa kawaida, halafu wanategemea msimu wa mazao, na ukiona sehemu vyakula ni vingi jua pesa hapo ni ngumu au hapo ufanye biashara ukiwa na mtaji mkubwa
 
Vijana buana mna shida sana

Back
Top Bottom