Nimeishi mataifa kadhaa hapa EAC.....
Tofauti kubwa ya Dar na Nairobi ni kwamba, kwa Nairobi maisha ni ya mwendo kasi, yaani kila mtu yupo mbioni kusaka hela, fursa ni nyingi sema zinapaswa kwa mtu jasiri usiye mwoga mwoga au kuona aibu.
kasoro ya Nairobi ni kukosa ule mshikamano wa kijamii, yaani kila mtu yuko kivyake, kila mnapokutana asilimia kubwa ya mazungumzo yenu ni biashara tu.....kwa kweli japo mimi Mkenya ila hayo maisha kuna wakati huwa nayaona kama soul less, haipaswi tuwaze hela sana.
Kwa Dar, pia penyewe niliona pana kasi ya kiaina lakini sio balaa kama Nairobi, kuna mshikamano baina ya watu kwenye jamii.