Kati ya Mpunga na Mchele, kipi kinawahi kuharibika?

Bongotunacheza

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2018
Posts
983
Reaction score
2,306
Habari zenu wadau. Naomba kujua tafadhali. Kipi bora kati ya hivi : 1. Ninunue mpunga nikoboe zitoke kilo elfu moja niweke ndani kwa ajili ya matumizi ya familia. Au ninunue mpunga, niweke ndani then niwe nakoboa debe kumi kumi za mpunga kila baada ya miezi miwili au mitatu.

Debe moja la mpunga = Shilingi ELfu SITA. Linatoa kilo kumi na 4 hadi kumi na tano za mchele.

Debe mia = shilingi laki sita ambazo ni = kilo elfu na mia 2 hadi elfu moja na mia tano za mchele.

wataalamu naomba mnielekeze tafdhali. Nataka kujua kama kipi kinawahi kuharibika kati ya mpunga na mchele

with much thanks in advance
 
We ndugu familia yako inapenda ubwabwa sana aisee... nunua mchele mkuu uifadhi.
 
Kama uko sehemu mashine za kukobolea zipo nunua mpunga hifadhi, Mchele sio wa kuhifadhi ni WA kuuza na kuliwa, kilo 1000 kwa matumizi ya familia sheikh una shule Nini?
 
Nunua mchele kitu pure paka mafuta ya kula weka ndani ,anza kula chele,miaka miwili hadi nne bila kuharibika,nina kilo zangu 300 kwa mwaka huu sina hofu
 
🤣🤣🤣 hapana mkuu naweka stock
 
Mchele unaharibika mapema. Mpunga ukitunzwa vizuri hata miaka miwili mitatu ukaa vizuri tu.
 
Habari zenu wadau. Naomba kujua tafadhali. Kipi bora kati ya hivi : 1. Ninunue mpunga nikoboe zitoke kilo elfu moja niweke ndani kwa ajili ya matumizi ya familia. Au ninunue mpunga, niweke ndani then niwe nakoboa debe kumi kumi za mpunga kila baada ya miezi miwili au mitatu.

Debe moja la mpunga = Shilingi ELfu SITA. Linatoa kilo kumi na 4 hadi kumi na tano za mchele.

Debe mia = shilingi laki sita ambazo ni = kilo elfu na mia 2 hadi elfu moja na mia tano za mchele.

wataalamu naomba mnielekeze tafdhali. Nataka kujua kama kipi kinawahi kuharibika kati ya mpunga na mchele

with much thanks in advance
Mkuu unataka kuifadhi kg 1200 za mchele kwajili ya kula tu,umeambiwa nchi inataka kuingia vitani au
 
Nunua mchele kitu pure paka mafuta ya kula weka ndani ,anza kula chele,miaka miwili hadi nne bila kuharibika,nina kilo zangu 300 kwa mwaka huu sina hofu
Kilo 100 zitahitaji mafuta ya kupaka lita ngp?
 
Back
Top Bottom