Kati ya Nissan Note au Corolla Fielder

Msela Ngoto

Member
Joined
Jun 10, 2018
Posts
29
Reaction score
28
Habari za leo wanajamvi,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, nimejichanga nataka kununua gari ambalo ni Nissan Note, ila kuna mtu amenishauri nichukue Corolla Fielder.
Kwanza nianze ku declare interest, binafsi nazipenda sana hizi Nissan Note kwa muonekano kwaiyo naomba kama kuna anayejua sifa zake kiufundi anijuze.
Pili hata hii chaguo la pili Corolla Fielder pia aomba kama kuna anayejua sifa zake kiufundi anijuze.
Halafu nitachagua moja kati ya hizo mbili, naahidi kuleta mrejesho hapa jamvini.
Nakaribisha maoni yenu wadau, karibuni saana.
 
Mimi naomba nizione kwa picha kwanza, afu zingatia pia swala la Cc usije nunua sheli kwa kuvutiwa na umbo tuu...
 
Mimi naomba nizione kwa picha kwanza, afu zingatia pia swala la Cc usije nunua sheli kwa kuvutiwa na umbo tuu...
Mkuu zote mbili zinafanana CC, ambacho sijui ni kila moja na suala lake la kiufundi i mean performance, matengenezo n.k
 
Mkuu zote mbili zinafanana CC, ambacho sijui ni kila moja na suala lake la kiufundi i mean performance, matengenezo n.k
Nina nissan note model ya 2005 ile yenye macho panzi Engine HR 15 cc 1490....niliagiza japan moja kwa moja mwaka 2014.

Kwa upande wangu tangu nimeagiza mpaka sasa haijanisumbua kitu chochote zaidi ya matatizo yale ya kawaida kulingana na mazingira yetu..mfano kubadilisha bush ni suala la kawaida...Hii yangu kila mwaka huwa nabadili wish bone bushes kulingana na hali ya njia zetu..hizi bushi zinapatika kirahisi tu zipo mbili kila moja nauziwa 15000/ nipo Arusha.

Kwenye injini haijawahi kunisumbua zaidi ya kubadilisha plugs tu ...Plugs zake original NGK ni35000/- kwa moja hapa Arusha....ukifunga za bei rahisi ugonjwa wa miss utakuwa ni mgeni wako wa karibu sana...yaani namaanisha kwa upande wa Engine Nissan zinataka replacemen ya genuine parts unlike toyota nasikia watu wakisema wanauziwa plug 6000/-

Hii gari ina sensors nyingi karibia nissan x trail so inapenda mtu makini na ufanye diagnosis unapohisi hali ambayo si ya kawaida...usiipeleke kwa mafundi wa chini ya muembe. Kwa ujumla injini yake inatumia umeme mwingi

pia nimewahi kubadilisha gear box mout miaka mitatu iliyopita mpaka sasa haijasumbua...

Kwa upande wa ger box kama ni auto huwa ni CVT ambayo inatumia NS2 cvt fluid kwa Arusha nanunua lita 4 sh 140,000/- mpaka 135,000/-
Ukiweka ATF nyingine gari haiondoki hapo ilipo.

Vifaa vingine vile vya service ya kawaida kama oil filter zipo mpaka za buku tatu ila mimi nafunga Original nauzwa 15000 ambayo ndiyo hiyo hiyo inavaa kwenye x trail.

Service nyingine niliyowahi kufanya ni kubadili boot rubber za ignition coil.....


Mambo mengine ni kagari kazuri kana balance nzuri sana barabarani hata kakifika 140 kph unahisi bado kanadai gia....inatulia sana barabarani..
consuption ya kawaida high way inaenda 14 km kwa lita. Kana feature ya key less kwa hyo ni mtindo wa kubonyeza tu.

Nilichojifunza Nissan ni gari ynzuri sana na imara sana ukitii masharti yake..Inavumilia taabu na dhiki.

hayo ndiyo machache ninayoweza kusema kuhusu nissan note kwa miaka 4 na nusu niliyokaa nayo..Binafsi naikubali kwani ukifunga kifaa original unasahau..Kwa ujumla nissan ukitii masharti yake unasahau watu wanaoitwa mafundi.
Karibu ulimwengu wa Nissan ujisikie tofauti[emoji16][emoji16]

Siyo watu wote mjini wafanane kwa IST...ukipaki kwenye sherehe unasahau yako ni ipi...unabonyeza remote itakayopiga hazard ndiyo hiyo yako...unazama ndani[emoji3][emoji23][emoji23] Wenye uzoefu wa Fielder wataweka hapa
 
Heshima yako mkuu Boeing 747 , nashukuru sana kwa kunipa somo mdau.
kwanza nikupongeze kwa kuchukua muda wako na kutoa elimu kama hiyo KONGOLE kwako.
turud kwenye mada, najua Nissan zinatumia mfumo wa CVT ila sijaua kama hii Note ninayotaka kuagiza maana nia ya 2009 kama inayo ama la.
nataka yenye engine ya HR15 coz ndo uwezo wangu ulipo maana zile za HR12 parefu kidogo ila ni more economy.
napenda kujua yako ni ya toleo gani mdau.?
natanguliza shukrani..
 
Nissan note yangu ni ya mwaka 2005.....
Nadhani ndiyo production ya kwanza ya nissan note mwaka huo..series zilizofuata kuanzia 2006- 2009 kama ni cc 1500 na ni auto, basi ni CVT...
Coz engine hii ya HR 15 na gear box yake ya CVT imetumika kwenye model kama Note, Tiida, Nissan Wingroad na baadhi ya Nissan blue bird sylf..

So kama ni auto tegemea kuwa ni CVT.....ukizingatia masharti yake inapiga mzigo tu.
 
Mkuu Boeing 747
Ahsante kwa muongozo wako, bado napenda kujua kuhusu Xtronic CVT ni nini hasa.??
 
Mkuu Boeing 747
Ahsante kwa muongozo wako, bado napenda kujua kuhusu Xtronic CVT ni nini hasa.??
Hiyo Xtronic CVT sijaifahamu
Nafahamu CVT pekee...maana yake ni CONTINOUS VARIABLE TRANSMISSION.....yaani gear box ya cvt ni tofaut na automatic za kawaida ambazo unakuta zina gia mfano moja mpaka nne au tano na gari inachagua gia kulingana na uendeshaji wako..na automatic ya kawaida huwa dereva au hata abiria anaweza kusikia mshtuko pale gari inapobadili gia.

Ila kwenye CVT huwa tofauti...cvt ina-act kama gia moja ambayo hubadilika umbile kuyokana na uendeshaji...hivyo huwezi kufeel kuwa gari inabadilisha gia...hivyo mwendo wa gari huwa smooth sana..

Angalia hapa upte elimu zaidi ya cvt transmission
 
Nimeangalia video mkuu, safi sana. nimejifunza kwamba CVT unavyoita wewe au Xtronic CVT wanavyoita wenyewe Nissan.
swali langi lipo hapa, Toyota wanatumia mfumo wa VVTi (Variable Valve Timing with intelligent) Je Nissan wanatumia mfumo gani.???
 
Sifahamu kwa Nissan nyinginezo ila hii injini ya HR15 inatumia mfumo wa EFI.......Electeoninc Fuel Injection..
Hakuna VVTi hapa. Nadhani teknolojia ya vvti iko developed na toyota.
 
Sifahamu kwa Nissan nyinginezo ila hii injini ya HR15 inatumia mfumo wa EFI.......Electeoninc Fuel Injection..
Hakuna VVTi hapa. Nadhani teknolojia ya vvti iko developed na toyota.
Nimekupata mkuu,

Ndo maana nikasema Toyota wanatumia mfumo wa VVTi katika kubana matumizi ya ulaji wa mafuta, so nikataka nijue na Nissan nao wana mfumo gani.??
Anyway bado najarib kufuatilia kwa ukaribu nikipata jibu sitakuwa mchoyo, nitaleta hapa kwenye uzi huu..
 
ebhane bora corolla fielder
inashea kila kila kitu na corolla zingine kama
-runx,police,allex,spacio nk..
engine ikiwa 2nz au 1nz bora zaidi i mean mafundi mpaka wa vijijini hawataishindwa
spea kila kona sio mpaka upige picha urushe kwa whatapp sample
utakuwa nayo huru muda wowote unauza tena ukiitunza ina soko
ina boot kubwa kidogo lifanane na la probox au succed..


sijasema NOTE ni mbaya ila tatizo mafundi wetu wa kibongo hawana taaluma sana na magari ya tofauti na toyota...labda kama uko dar es salaam angalau...ila ni vyema uchukue fielder kuepuka kuvutana vutana barabarani....
 
Utafiti usio rasimi:
Kati ya watu 5 walionunua NISSAN 3 walijuta;
Kati ya watu 5 walionunua TOYOTA 1 alijuta.
 
exactly...
ndo maana nimemshauri achukue toyota fielder..na tatizo sio nissan mbovu la mafundi hatuna
Point yako ina msingi sana na ina ukweli usiopingika.....Mafundi ndiyo wanafanya magari mengine yaonekane mabovu kitu ambacho si kweli..
Mimi na nissan note yangu sijawahi kujuta coz nazingatia masharti yake na fundi wangu ni mmoja...na nikipeleka garage nakuwa ninejiridhisha mwenyewe kuwa hitilafu ni nini..

Jambo la kuongezea.....magari ya siku hizi teknolojia imekuwa sana...si toyota...si nissan...si suzuki na kampuni nyingine.... model nyingi za kijapani kuanzia 2005 wame..advance sana kwenye teknolojia ya injini kwa lengo la kubana mafuta na kupata nguvu kubwa..

Hivyo kwa fundi kilaza hata Toyota za leo anaweza asiweze kubadilisha hata plug tu....mafundi hawataki kusoma.

Bado nakubaliana kuwa atoyota is still the best kulingana na nchi yetu na upatikanaji wa spare.

dunia inekuwa kijiji...spare za gari nyingi hasa za kijapani zile common kama Toyota na Nissan zinapatikana kirahisi bora tu uwe na hela.

Kama huna hela nadhani hata vitz old model utaiona ni chungu kwa upatikanaji wa spare.

Mwisho unaponunua gari sikiliza ushauri, angalia bajeti yako, angalia matumizi yako, angalia unaishi wapi ili upate spare husika kirahisi, na mwisho kabisa angalia kipendacho roho.
Na gari za siku hizi ikikusumbua hazihitaji nyundo...fanya diagnosis...gundua kifaa chenye hitilafu...ukishakinunua unaweza hata kukibadilisha mwenye ukiwa nyumbani.
!
 
Mkuu New Nytemare habari yako mdau,

Ebana kwa kiasi fulani nakubaliana na wewe, hii mentality imeshajengeka sana kitaan kwamba ukitaka kununua gari nunua Toyota by defaulty, lakini zipo brand za Toyota kwa mfano Oppa had leo nyingi zipo juu ya mawe. lakin tunaambiwa kwamba spea zake bei rahisi.
wapo watu wanamilik benz A class had leo tunaziona road na maisha yanaendelea kama kawaida
 
Utafiti usio rasimi:
Kati ya watu 5 walionunua NISSAN 3 walijuta;
Kati ya watu 5 walionunua TOYOTA 1 alijuta.
Mkuu Bila bila

Sitofautiana sana na wewe, ni jambo lililo wazi kwamba spea za Nissan ni bei ya juu tofauti na Toyota.
Sasa kama Plug original za Nissan NGK zinauzwa elfu 35 kwa moja wakati za Toyota zinauzwa elfu 6 - 10 Kwa moja kwa nini mtu asikwambie Nissan ni gari mbaya.??
 
Mtaalam Boeing 747

Ama kwa hakika umeongea ya kutoka moyoni kabisa.
Gari za Toyota zinasifika kwa Reliability wakati agri za Nissan zinasifika kwa Durability.
sasa hapo nadhani kabla hujanunua gari kwanza tujitafakari tunahitaji nini kwanza ili usije ukavamia msitu na wembe.
mwisho wa siku bajeti yako kwenye maintenance ni factor muhimu sana kabla ya kununua gari.
 
tatizo ni mafundi hapa bongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…