Mkuu zote mbili zinafanana CC, ambacho sijui ni kila moja na suala lake la kiufundi i mean performance, matengenezo n.k
Nina nissan note model ya 2005 ile yenye macho panzi Engine HR 15 cc 1490....niliagiza japan moja kwa moja mwaka 2014.
Kwa upande wangu tangu nimeagiza mpaka sasa haijanisumbua kitu chochote zaidi ya matatizo yale ya kawaida kulingana na mazingira yetu..mfano kubadilisha bush ni suala la kawaida...Hii yangu kila mwaka huwa nabadili wish bone bushes kulingana na hali ya njia zetu..hizi bushi zinapatika kirahisi tu zipo mbili kila moja nauziwa 15000/ nipo Arusha.
Kwenye injini haijawahi kunisumbua zaidi ya kubadilisha plugs tu ...Plugs zake original NGK ni35000/- kwa moja hapa Arusha....ukifunga za bei rahisi ugonjwa wa miss utakuwa ni mgeni wako wa karibu sana...yaani namaanisha kwa upande wa Engine Nissan zinataka replacemen ya genuine parts unlike toyota nasikia watu wakisema wanauziwa plug 6000/-
Hii gari ina sensors nyingi karibia nissan x trail so inapenda mtu makini na ufanye diagnosis unapohisi hali ambayo si ya kawaida...usiipeleke kwa mafundi wa chini ya muembe. Kwa ujumla injini yake inatumia umeme mwingi
pia nimewahi kubadilisha gear box mout miaka mitatu iliyopita mpaka sasa haijasumbua...
Kwa upande wa ger box kama ni auto huwa ni CVT ambayo inatumia NS2 cvt fluid kwa Arusha nanunua lita 4 sh 140,000/- mpaka 135,000/-
Ukiweka ATF nyingine gari haiondoki hapo ilipo.
Vifaa vingine vile vya service ya kawaida kama oil filter zipo mpaka za buku tatu ila mimi nafunga Original nauzwa 15000 ambayo ndiyo hiyo hiyo inavaa kwenye x trail.
Service nyingine niliyowahi kufanya ni kubadili boot rubber za ignition coil.....
Mambo mengine ni kagari kazuri kana balance nzuri sana barabarani hata kakifika 140 kph unahisi bado kanadai gia....inatulia sana barabarani..
consuption ya kawaida high way inaenda 14 km kwa lita. Kana feature ya key less kwa hyo ni mtindo wa kubonyeza tu.
Nilichojifunza Nissan ni gari ynzuri sana na imara sana ukitii masharti yake..Inavumilia taabu na dhiki.
hayo ndiyo machache ninayoweza kusema kuhusu nissan note kwa miaka 4 na nusu niliyokaa nayo..Binafsi naikubali kwani ukifunga kifaa original unasahau..Kwa ujumla nissan ukitii masharti yake unasahau watu wanaoitwa mafundi.
Karibu ulimwengu wa Nissan ujisikie tofauti[emoji16][emoji16]
Siyo watu wote mjini wafanane kwa IST...ukipaki kwenye sherehe unasahau yako ni ipi...unabonyeza remote itakayopiga hazard ndiyo hiyo yako...unazama ndani[emoji3][emoji23][emoji23] Wenye uzoefu wa Fielder wataweka hapa