Kati ya Nissan Note au Corolla Fielder

Ni kweli spea za nissan ni gharama ila ukifunga umefunga...hizi plug nilifunga August 2016 nimezitoa mwezi uliopita November 2018...zimepiga miaka miwili...na ninezitoa huku fundi akilalamika mbona bado zinadai[emoji3]

Ila kwa upande wangu nikaona inatosha na zimesharudisha mpaka chenchi.[emoji23]
 
Ni kweli kabisa mdau,
wazungu wanasema "Dont hate the game, hate the player" sisi tunalaumu gari za Nissan wakati matunzo na matengenezo yake hatuziwezi sidhani kama imekaa vizuri hii..
 
Bongo bado hatuna mafundi....kuna injini za toyota D4 nasikia mafundi wengi wanaziogopa sana.
Nikupe uzoefu wangu, nimeshawahi kutumia Mazda huko awali had watu wananiuliza ebana tunaambiwa hizi gari vimeo sana sasa mbona wewe hata siku moja hatukusikii au kuona gari yako inasumbua.?
jibu langu likawa moja tuu: Watu wengi tunapenda sana kuamini maneno ya kuambiwa..
 
Huo ndiyo ukweli...unakutakuta mtu anakukatisha tamaa gari fulani siyo gari...ukimuuliza unewahi kuimiliki kwa miaka mingapi?anaaza povu.

Sunia ya leo magari ya mjapan karibu yote yanafanana hivyo ni swala tu la kuzingatia masharti na uwe na hela ya spea husika.
Bado nasisitiza hakuna gari kimeo endapo utatii mashrti yake.
 
kweli kabisa kaka, had leo naziona volkswagen za engine nyuma ambazo hazitumii radiator watu wanazitumia kwa aliyeitunza lakin.
bado mtu anaonekana mjanja kwa sababu ameitunza halaf ameiremba kwaiyo ina compete na magari mapya mtaan.
Gari kama gari haina tatizo, tatizo lipo kwa mtumiaji.
 
exactly...
ndo maana nimemshauri achukue toyota fielder..na tatizo sio nissan mbovu la mafundi hatuna
Kwa ushauri wangu Toyota fielder hutajutia na kulingana na mazingira ya hudumu kwa Fielder huduma ziko njenje japo kama pochi nene na maintanaince ya Nissan Note ilivyo na inavyohitaji umakin bado ni gari zuri
 
Kwa ushauri wangu Toyota fielder hutajutia na kulingana na mazingira ya hudumu kwa Fielder huduma ziko njenje japo kama pochi nene na maintanaince ya Nissan Note ilivyo na inavyohitaji umakin bado ni gari zuri
Ameomba ushauri mwaka juzi we unamshauri leo?
 
Opa ilivyo ngumu mpaka ifikie kuwa juu ya mawe ujue mmiliki hata hela ya kulisha tumbo lake ni mtihani😁😁😁!!!

Gari ni kama demu, lazma uhudumie mwanzo mwisho otherwise likikushinda ndio utajikuta umelipaki juu ya mawe ila licha ya yote ukiona mtu kashindwa kuhudumia Toyota yoyote ya <1.8L basi jua kabisa hataka aweze kumiliki gari ya brand tofauti
 
Back to topic mie naipenda Fielder personally sababu i like the VAN shaped Cars and it has been a dream toka nimeiona. Nina mwana mmoja wa TAKUKURU ana hio gari i drove it once. Ni gari zuri kwa kweli liko well insulated na eco mode yake inasoma 12ltr per km on town trips hapo with AirCon ON.

Lina plenty space kwa ndani japo lipo chini sana ila with big tyres inaweza kuwa msaada. Ni gari ambayo ukitaka kuipimp muonekano inakaa poa sana na mvuto maradufu hasa ukipiga sport rims.

Kuhusu Note imekaa kama Toyota Sienta ama FunCargo. The form factor sijaipenda kabisa katika design za hizo gari which means hata notw haina mvuto kwangu kabisa.
 
Nissan note uwe una compare na toyota fun cargo au ractis ndio gari zilitrngenezwa kushindanishwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…