KWELI Kati ya picha hizi moja imetengenezwa kwa AI na nyingine ni halisi

KWELI Kati ya picha hizi moja imetengenezwa kwa AI na nyingine ni halisi

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Wakuu salama hapa,
Hizi picha mbili zinanichanganya kutambua ni ipi ni halisi ni ipi imetengenezwa kwa AI, naomba msaada wa kuzitofautisha wakuu.
Snapinsta.app_469705964_593428933230366_1366847342913692378_n_1080.jpg

Snapinsta.app_469681356_2730663867117876_6776511070365299968_n_1080 (1).jpg
 
Tunachokijua
Akili mnemba (AI) ni seti ya teknolojia zinazoiwezesha kompyuta kutekeleza majukumu mbalimbali ya kina na kwa uwezo mkubwa kadri ya maelekezo ya mtumiaji, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuona, kuelewa na kutafsiri lugha inayozungumzwa na maandishi, kuchanganua data, kutengeneza picha na video na kutoa mapendekezo ya utatuzi wa matatizo mbalimbali.

Licha ya kuwa na lengo zuri teknolojia hii ya Akili Mnemba (AI) ikiwa ni pamoja na kurahisisha na kuongeza ufanisi wa kazi ambazo huweza kufanya kwa muda mfupi na kwa usahihi, lakini wapo watu wasio wema wamekuwa wakiitumia katika kupotosha taarifa mbalimbali katika Jamii. Hivyo ni vema kila mara kujifunza mbinu zitakazokuwezesha kutambua maudhui aidha ya maandishi, picha, video au sauti zilizotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Mnemba ili kuepuka kupotoshwa.

Kati ya picha hizi mbili, mojawapo imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Mnemba na nyingine ni halisi.

Tutazame uhalisia wa picha hizi.

JamiiCheck imebaini kuwa ni kweli kati ya picha hizo mbili moja kati ya hizo imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili mnemba na nyingine ni picha halisi. Na picha hii ndiyo iliyotengenezwa kwa kutumia akili mnemba.
snapinsta-app_469705964_593428933230366_1366847342913692378_n_1080-jpg.3186133


Picha hii imebainika kuwa na mapungufu kadhaa yanayobainisha kuwa imetengenezwa kwa AI, sehemu ya mapungufu hayo ni pamoja na kutokuwepo kwa hali ya uoto katika sehemu ya pembezoni mwa mto ambapo kwa kawaida katika sehumu kama hiyo yenye maji huchochea uwepo wa uoto (mimea), lakini pia uwepo wa mwanga unaoonekana kuwa wa jua ilihali anga la eneo hilo linaonekana kugubikwa na wingu zito jeusi la mvua ambalo husababisha uwepo wa mwanga hafifu.

Tofauti na picha halisi ambayo vitu vilivyopo katika picha hiyo niabainisha uhalisia wa mazingira halisi, mfano uwepo wa ardhi yenye unyevunyevu mwingi ikiwa na hali ya uoto wa kijani tofauti na picha isiyo halisi, Pia uwepo wa nyaya umeme zilizopita juu ya mto, huku pembeni ya mto upande wa kulia mwa picha kukiwa na watu kadhaa kadhalika kukiwa na mwanga unaoendana na hali ya anga isiyokuwa na wingu zito.
snapinsta-app_469681356_2730663867117876_6776511070365299968_n_1080-1-jpg.3186134

Aidha kifaa cha kutambua maudhui yaliyotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili mnemba, kimeitambua picha ya kwanza kama picha iliyotengenezwa kwa Akili mnemba kwa asilimia 99
screenshot-2024-12-29-072739-png.3187467


Huku picha nyingine ikitambuliwa kwa asilimia 1% tu na kifaa hicho kikibainisha kuwa picha hiyo haijatengenezwa kwa Akili Mnemba.
screenshot-2024-12-29-072930-png.3187468
Picha ya kwanza imetengenezwa na haina uhalisia. Imeondoa vitu vingi tunavyotegemea kuviona kwenye eneo la maji na imeboreshwa zaidi
 
Hakuna uoto wa asili uliozunguka maji yakiwemo majani nk. Pia hakuna mifugo watu na ukiangalia huo msitu umefanywa mziti sana
 
picha zote zipo sawa na nihalsi sema zimepgwa muda na msimu tofauti
 
Zote mbili kama hiyo ya pili tazama uwiano wa mawe na hao watu na umbali mwonekano wa miti pia
 
Back
Top Bottom