Mdau shiriki kuthibitisha kati ya picha hizi mbili, ipi ni halisi? Bainisha tofauti tano zilizopo katika picha hizi.
- Tunachokijua
- Akili Unde (AI) ni seti ya teknolojia zinazoiwezesha kompyuta kutekeleza majukumu mbalimbali ya kina na kwa uwezo mkubwa kadri ya maelekezo ya mtumiaji, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuona, kuelewa na kutafsiri lugha inayozungumzwa na maandishi, kuchanganua data, kutengeneza picha na video na kutoa mapendekezo ya utatuzi wa matatizo mbalimbali.
Aidha teknolojia hii imekuwa muhimu katika kurahisisha ufanisi wa shughuli za kila siku, lakini inapotumiwa kwa nia ovu huweza kusababisha madhara makubwa kwa watu, mathalani uwepo wa taarifa potofu unachangiwa pia na teknolojia hii ambayo watu hutumia kutengeneza na kusambaza taarifa zisizo sahihi mfano maudhui ya picha, sauti, au video.
Mfano Akili Unde inaweza kutumika kupotosha picha au video halisi kwa kuhariri maudhui hatimaye kugeuza uhalisia. Rejea picha hizi mbili zinazofanana ambapo moja ni halisi na nyingine imehaririwa kwa akili unde.
Je, unawezaje kuzitofautisha picha hizi?
Katika kutofautisha picha halisi na iliyohaririwa kwa Akili Unde, zipo tofauti kadhaa zinaweza kusaidia kubainisha uhalisia. Kwanza uwepo wa "TZ World" katika moja ya mtambo katika picha B si halisi kwani hakuna kampuni ya uendeshaji wa shughuli za bandari yenye jina hilo bali "DP World" kama inavyoonekana katika picha A.
Pili uwepo wa watu waliovaa suti katika picha B ambao wanaonekana kusimama kwa heshima kuelekea upande mmoja na kukosa uhusiano na watendaji wengine wanaoonekana katika picha hiyo, tofauti na picha A, tofauti zingine ni pamoja uwepo wa namba 12 picha B tofauti na 16 iliyopo katika picha A, Kutofautiana kwa rangi ya meli, kuongezeka kwa begi kubwa katika picha B.
Pia katika mazingira ya bandarini yenye ukaribu na mitambo mikubwa, watu huhitajika kuvaa kofia ngumu (Helmet) pamoja na mavazi maalum, hii inaonekana kuwa tofauti katika picha B ambayo kuokana na mapungufu hayo inathibitika kuwa ndiyo iliyohaririwa kwa Akili Unde kutoka kwenye picha halisi A.