Kati ya Pierre Liquid na Dudubaya, nani mwanzilishi wa neno Konki?

Kati ya Pierre Liquid na Dudubaya, nani mwanzilishi wa neno Konki?

ntamaholo

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
12,938
Reaction score
6,942
Wadau salam.

Mungu buana, mwache aitwe Mungu. Na akitaka kukupaisha atakupitisha njia ambazo hutoamini macho yako.

Pierre katoka huyo, na kitendo cha Makonda kumponda ndo kimemtoa ile mbaya, sasa hakamatiki kabisa. Hata mimi nimemfahamu leo kwa kuwa Makonda alimchana live, hbr zake zikaanza kutrend, ikabidi niulize tu, Pierre ni nani?

Nimepewa majibu, nikaingia YouTube, kuna mengi kumhusu tena kitambo. Hivyo makonda alichofanya, ni kumpiga chura teke atumbukie majini.

Back to topic.

Pierre na Dudubaya, wote wanatumia neno #KONKI# japo kwa style tofautitofauti. Wakati Pierre anachomeka maneno kama fire, Dudu yeye anaitaja mara tatu na kumalizia neno master.

Je, nani mwanzilishi wa neno hili?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitaja neno konki hata katoto ka miaka miwili kanamalizia dudubaya
 
😂 haha Mkuu tuko wengi mimi mwenyewe niliona Uzi hapa JF nikawa najiuliza huyu Pierre ni nani? Nikaingia YouTube,
Ila Makonda Jinga sana na sifa zake za Kijinga..
 
Asili ya neno konki ni arusha,mara ya kwanza kusika kwenye vyombo vya habari ni katita wimbo wa Wa Gnako na Godzilla (tumewaka) warawara alisikika akisifia pombe kuwa ni konki.Maana ya konki arusha kitu kikali kizuri mfano bangi ikiwa kali nzuri,machalii husema hii dawa ni konki au pombe ikiwa kali nzuri utasikia hii pombe konki pia ni kawaida kusikia mirungi ikisifiwa hii veve ni konki.Baada ya hapo ndipo mlevi wa taifa akachukua neno konki na kulitumia kwenye harakati zake za ulevi,alisikika akisema liquid konki fire,akiwa kwenye furaha ya ulevi alitamka liquid konki fire nakufa.Baada ya hapo ndio umaarufu ukamfwata na dudu baya bila kuchelewa akachukua neno konki na kulitumia kwenye michambo yake akaongezea master.Naamini dudu baya akiulizwa maana ya neno konki hatambui.
 
Asili ya neno konki ni arusha,mara ya kwanza kusika kwenye vyombo vya habari ni katita wimbo wa Wa Gnako na Godzilla (tumewaka) warawara alisikika akisifia pombe kuwa ni konki.Maana ya konki arusha kitu kikali kizuri mfano bangi ikiwa kali nzuri,machalii husema hii dawa ni konki au pombe ikiwa kali nzuri utasikia hii pombe konki pia ni kawaida kusikia mirungi ikisifiwa hii veve ni konki.Baada ya hapo ndipo mlevi wa taifa akachukua neno konki na kulitumia kwenye harakati zake za ulevi,alisikika akisema liquid konki fire,akiwa kwenye furaha ya ulevi alitamka liquid konki fire nakufa.Baada ya hapo ndio umaarufu ukamfwata na dudu baya bila kuchelewa akachukua neno konki na kulit

Konki imetokana na Conc kifupi cha concentration hakuna mwenye jina lake hapo.
 
Back
Top Bottom