Kati ya samadi ya ng'ombe, mbuzi, kuku, nguruwe, Sungura nk. ipi ni bora zaidi shambani?

Kati ya samadi ya ng'ombe, mbuzi, kuku, nguruwe, Sungura nk. ipi ni bora zaidi shambani?

Namie nimeambiwa pia hii ya popo, kwamba inastawisha vizuri sana...ila ya kuku inaunguza mazao.
Kila mbolea inaunguza ndio maana kwa mbolea za vinyesi huwa tunashauri /tunashauriwa kuweka wiki 2 hadi 3 shambani kwanza na uivuruge vzur na udongo kabla hujapanda

Kinachofanya mmea uungue ni zile reaction zinazofanywa na wadudu kwenye mbolea huzalisha joto ambalo ndio huunguza mmea

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
kwenye viazi mviringo hata ukipandia haileti shida (hasa maeneo yenye ubaridi kama njombe au rungwe)
 
Nilienda sehemu nikakuta wanaweka mbolea ya kuku shambani wanaiacha mpaka miezi miwili kabla ya kupanda. Hii mbolea ni kali mno ila kama nilivyosema ina utaalamu wake

Kama kuchanganya ya ngombe na nguruwe au iyo noah umemanisha nini? Nadhani ukiwa unapendelea kuweka hii mbolea shambani utaona matokea chanya. Changanya utuletee mrejesho. .
Unaweza kuiweka mbolea ya kuku mahali ambapo jua linapiga muda wote na kisha unaimwagia maji kidogo na kuivundika Kwa kuifunika Kwa nailoni ili joto lake lisipotee Kwa urahisi. Unaweza iacha Kwa miezi mitatu...pia kuigeuza mara Kwa mara kunaifanya iive mapema na kupungua ukali( nitrogen)
 
Samadi ya ngombe ina long lasting effect ukiwa unaweka shambani rutuba yake inaweza kaa hata miaka mitatu. Samadi ya nguruwe ina nguvu ya kukuza mimea dakika sifuri tu nayo ukiweka shamba la mahindi utashangaa kijani chake. .

Samadi za kuku zina utaalamu wake utaunguza mazao usipokuwa makini ukaweka tu, na maa nyingine kutokana na pumba kwenye samadi ukakuta unachoma badala ya kustawisha mmea. Unaweka samadi ya kuku unakuta inaleta msururu wa sisimizi. .

Hapa ninafunga vibata juzi nimefagia kama mtu anahitaji mbolea niko manzese. .
Umenipa kitu kipya hapa, home tunajimwagiaga tu kwenye mboga
 
Kwa mazao ya muda mfupi kama mboga mboga mbolea ya kuku mbuzi sungura inafaa zaidi maana inakupamatokeo ya haraka lakini haidumu shambani

Mbolea ya Ngombe ni ya muda mrefu na hutumika kwa muda mrefu, inafaa zaidi kwa mahindi mtama nk

Sina uzoefu na samadi ya kitimoto
 
Samadi ya ngombe ina long lasting effect ukiwa unaweka shambani rutuba yake inaweza kaa hata miaka mitatu. Samadi ya nguruwe ina nguvu ya kukuza mimea dakika sifuri tu nayo ukiweka shamba la mahindi utashangaa kijani chake. .

Samadi za kuku zina utaalamu wake utaunguza mazao usipokuwa makini ukaweka tu, na maa nyingine kutokana na pumba kwenye samadi ukakuta unachoma badala ya kustawisha mmea. Unaweka samadi ya kuku unakuta inaleta msururu wa sisimizi. .

Hapa ninafunga vibata juzi nimefagia kama mtu anahitaji mbolea niko manzese. .
Asante hapa nimekukubali maana kuna Mboga zangu zilikuwa zinastawi vizuri nikaweka Mbolea ya Kuku matokeo yake hazistawi tena vizuri zinaelekea kukauka.
 
Asante hapa nimekukubali maana kuna Mboga zangu zilikuwa zinastawi vizuri nikaweka Mbolea ya Kuku matokeo yake hazistawi tena vizuri zinaelekea kukauka.
Mbolea ya kuku ni vyema ukaiacha kwanza ioze vizuri hlf ndo uitumie...kama una nylon, unaimwagia maji halafu unaifunika iive haraka...wiki mbili mpaka tatu joto litaanza kupungua hapo ndo unaweza kutumia...
 
Ya binadamu ni kiboko...kitambo Kuna kota tukiishi,Kuna chambers zile za maji mafachu zilifurika, Kuna Mzee Mmoja ni staff pale tupo nae kota,akapanda maboga pale, aisee yalikua ya afya na mazuri na meengi mno,Kila siku wanakuja kujumua.
 
Back
Top Bottom