Waterbender
JF-Expert Member
- Oct 2, 2018
- 7,573
- 10,063
izi A izi nishashuudia moja ivi ina uzito flan lakin sikujua ni A ngap ngap lakin nikuanzia 10 nadhan nilistuka maaan kuna dogo alikuwa na A7 2015 du ni kamtambo haswa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Update ya android 10 umeiona?imeshatoka unaweza upgrade
a7 2017 bado inazidiwa na za mwaka jana nyingi tu.atleast uanze kutaja za 2017 kidogo afadhali.izi A izi nishashuudia moja ivi ina uzito flan lakin sikujua ni A ngap ngap lakin nikuanzia 10 nadhan nilistuka maaan kuna dogo alikuwa na A7 2015 du ni kamtambo haswa
nadhan project huwa zinafel kimtindoa7 2017 bado inazidiwa na za mwaka jana nyingi tu.atleast uanze kutaja za 2017 kidogo afadhali.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu japo kwa kuchelewa kutokana na majukum ya kila siku ila niMkuu hembu Nisomee herufi ya mwisho kwenye model ya hio simu.....pengne hapo ndio tatzo lilipo... labda ulinunua unlocked....
Utaona wameandika hivi
SM-A105.
Hembu malizia hio nukta hapo juu,
Najua inaweza kua kati ya
SM-A105F/DS
SM-A105G/DS
SM-A105M/DS
SM-A105M..
Angalia ni ipi kati ya hizo....
Japo pia hizi A-series kuanzia A10 nyingi sana ni Jau,
Zinazingua network, speaker/audio quality, kamera n.k(sio zote na matatizo yanatofautiana)
Katika series walizo zingua samsung...
Basi ni hizi
Ushauri mzuri sana. Kweli JF ni kisima cha maarifa. Asante sana ndugu reyzzapHII KITU WATU WANAICHUKULIAGA POA ILA MATOKEO YAKE NDIO UMENUNUA LIJISIMU LINASUMBUA NETWORK AU UNAUZIWA SIMU ILIYOTUMIKA UKIDANGANYWA NI MPYA...
Ngoja Nikuvute taratibu ili unielewe vzr...
Si unajua Kuna hizi simu zinauzwa Na Makampuni ya Mawasiliano Mfano Tigo shop?
Ni mara nying sana Tunasikia sijui tigo Anatangaza anauza Tecno mfano spark 3, n.k n.k kwa promoshen..
View attachment 1414980
Tunajua kbsa tigo hatengenezi simu, ila anatoa chip ya sim na huduma zote kutokana na ile chip....
Sasa basi....Kinachotokea Tigo anaingia ubia na Tecno....
Tigo anamsaidia tecno kutangaza simu zake kiurahisi.....Kupitia matangazo yao, wakati huo huo tigo anauza hizo/hio simu kwenye maduka yao kwa bei rahisi zaidi ya Maduka ya kawaida na Anakupa na kifurushi zaidi...
Sharti kubwa la tigo analompa tecno ni kwamba....Lazima laini Moja Ifungwe (locked) itumie laini ya Tigo pekeee....
Hii sasa inaitwa CARRIER LOCKED..View attachment 1415038
Na hapa sasa Tigo ndipo anapofaidika.... Anajua lazima Laini yake itatumika hivyo ataongeza wateja... Hata km hukua na laini ya Tigo Utanunua kwa shart la kupata ile simu.. na sio kununua tuu lazima utashawishika kuitumia sbb wanakupa na ofa....
Kwahiyo
Tigo anafaidika kwa kupata wateja/watumiaji wengi... na
Tecno nae anafaidika kwa Kuuza simu nying na kuzitangaza kirahisi..
TUENDELEE
Sasa sbb Mtu anahitaji urahisi.....
Ameona Atapata hio simu Tigo shop kwa bei rahisi....Pili atapewa na vifurushi vya bure kwa mda flan....Basi naye anaenda kununua simu tigo shop Ambapo Lazima SIM 1 Isome laini ya tigo.....
Sasa ikafika kipnd amechoka kutumia laini ya Tigo kiulazima.....
Anachokifanya anaenda kwa wataalam Ana i UNLOCK ule Mtandao(CARRIER) uliofungwa kwa ulazima.....Kibongo bongo Tunaita Kuflash...
Hili Neno tumelisikia sana hasa miaka ya nyuma kdg
'Nataka ni flash simu yangu Itumie laini zote'
Ku UNLOCK ni kufungua kitu...View attachment 1415044
CARRIER ni ule mtandao...
Kwaio unafungua tray(Mara nying ni SIM 1)ya simu iliyokua imefungwa kwa mtandao flani ili ile tray isome Laini ZOTE.
Hii sasa ndio CARRIER UNLOCKED...View attachment 1415047
Hicho ndio kinachotokea Hata huko ulaya/usa n.k
Samsung Anaingia ubia na Makampuni ya simu km Verizon, AT&T, T-Mobile n.k n.k...
Mtumiaji akichoka kutumia ile simu anataka aiuze nje ya USA inabidi aipeleke waka i Unlock ili isome laini zote la sivyo Ndio zile ikija huku simu haisomi laini mpk uipeleke kwa wataalam...
KWA NN NASEMA IEPUKE?
Kwanza Ijulikane kbsa ku flash simu iliyokua imefungwa ni illegal....Hata hao tigo ukiwaambia masuala ya ku flash watakumaind....
Wenzetu ulaya wao wana mda maalumu kutokana na mkataba... ni angalau miaka miwili Ndio unaweza uka i unlock na sheria isikubane...
Maana kinyume na hapo Ni hasara....
Haiwezekani unitumie mm nikuuzie simu kwa bei chee na kukupa vifurushi vya bure halaf laini yangu ambapo mm ndio nategemea nipate faida huitumii...
Sasa Unapo i flash kuna mawili....
Either Isisome laini kbsa au isome kwa shida...
Kwa ufupi mara nyingi zinazingua network...
NA HIKI NDIO SBB NAKUAMBIA ZIEPUKE...
Unaweza utumie unaona iko poa lkn ukipata simu nyingne km hio hio ambayo ni free utaona utofaut mkubwa...
Au ukabadilisha tu mazingira unaona simu yako inasumbua network nakat za wenzako zinapga kazi...
Wengi washakutana na hili tatzo hasa kpnd kile tunatumia visimu vya vodafone au vile vibatan vya tigo..
UTAJUAJE HII SIMU NI UNLOCKED?
Simple Tu...
simu nyingi zinazokua Locked na mtandao flan...
Zinakua na symbol flan za ule mtandao mfnView attachment 1414985View attachment 1415000
Huku futuhi unakuta imeandikwa tigo juu au nyuma ya simu...
Nyingne ukiiwasha inaakuandikia Vodacom n.k n.kView attachment 1415005
Kwa zile za US utakua mfano simu imeandikwa au ukiwasha inaandika
VERIZONI, T-MOBILE AU AT&T ukiona hivyo tuu jua Ni unlocked....View attachment 1415042
Sasa nying za sikuhz hawaandiki...
Ukiona hivyo njia rahisi ni kusoma Model number...Ambayo inakua nyuma ya simu au ingia ndani kwenye about phone....
kwa Samsung S-series Model # Yake Utaona
Imeandikwa hivi SM-G.... hapo kwenye hivyo vidoti Vinne Ni namba kutokana na simu husika....
Mfano wewe nimekwambia Kwa hela hio Unaweza ukapata S9+,
Basi model namba yake PIGA UA
itaanza hivi SM-G965., Kwenye hicho kidoti cha mwisho sasa, NAMBA au HERUFI itakayomaliziwa hapo ndio muhimu kujua km simu ni Free au Carrier unlocked sasa
Mfano km hio S9+ ilikua locked kwa Mtandao wa Verizoni Utaona imeandikwa hivi
SM-G965V, Kama ni T-Mobile Utaona imeandikwa SM-G965T km ni AT&T utaona
SM-G965A.
Nzuri ambayo haijawa locked.....
Wanaita
Global/international - Model/version..
LAZIMA MWISHO IISHIE NA....F/DS/FDView attachment 1415056View attachment 1415059
kwahio Itakuwa hivi
SM-G965F/DS/FD....
Inaweza ikawa chochote kati ya hivyo vitatu.. ila mara nyingi ni F au DS au vyote kwa pamoja yaani .....F/DS
Ukiona kwenye hio model Amekuandikia DS
Hii inamaanisha hio simu ni Dual Sim(laini mbili) Na hio F For Free..
Na ukiona Mwisho Hajaweka HERUFI kaweka NAMBA..
Mfano SM-G9650, jua hio simu sio Locked ila Ni mahususi kwa kuuzwa Nchi/ukanda au bara Flani...
Mfano Europe, Asia, South korea, China n.k...
Kwaio haiko locked ila imetengenezwa kwa kuuzwa maeneo maalum...
Kwa samsung Note-series utaona
Imeandikwa hivi SM-N....
Mfano Note 9 Unatakiwa uchukue yenye
SM-N965F/DS
Kwa Samsung Joy a.k.a J-Series Utaona
Imeandikwa hivi SM-J....
Kwa Samsung Alpha a.k.a A-Series utaona
Imeandikwa hivi SM-A....
Hii ni kwa simu zote za samsung HASA MATOLEO ya miaka hii, Global model...
Inatakiwa iishie na ......F/DS
Ila ukipata Model inayoishia na .....0, U au H(kwa simu za zamani)
hizo sio mbaya angalau zinakuwaga vizuri,
Au yyt inayoishia na namba...
Ila sio hayo ma T,V & A.... Japo nazo waweza upate ambayo imekua unlocked vizuri ila PIGA UA jua hio simu ni Used sasa....
Mara nyingi Ukipata Samsung Yenye Laini mbili basi usiwe na shaka ni hii inshu....
ILA ukiona tuu Samsungu Kwa nyuma Chini Imeandikwa jina la Simu......
Mfano Galaxy S6+, Galaxy S7, Galaxy S7 plus,
Galaxy S8+, Galaxy S9+ n.k n.kView attachment 1415062View attachment 1415066
Ambazo zimejaa sana na tunaona watu wengi wakiziuza.....
Hio kimbia ni Unlocked.....
Kama sivyo basi Hio simu ilifanyiwa repair...
Hio sio original case yake.
International model Samsung HAWAANDIKI Jina kwa nyuma zaidi ya Brand
Inatakiwa uone neno SAMSUNG tuu kwa juu....
Chini labda uone neno DUOS kwa zile za laini mbili au yale maelezo meng kwa maandishi madogo....ambayo yanakua ya model, imei n.k...View attachment 1415069View attachment 1415075
USHAURI WA BURE....
Ukiona mtu anauza simu hasa hizi high end(Unaona kbsa ni ya gharama) halafa anakuambia
"EXCHANGE ALLOWED"
Halaf haweki conditions zozote/Mashart yoyote....
ANZA KUTUMIA UBONGO WAKO VIZURI
Huyo anachotaka ni simu imuondokee by any means......chochote atakachopata sio hasara kwake bali kwako....
Kwa ufupi : kua makini sana na simu za exchange....
TUPO DUNIANI KWA JUKUMA MAALUM..
TIMIZA JUKUMU LAKO...
Hizo simu ni Jangaaaaa....Nimewahi nunua samsung s4 ilikuwa ya VERIZON yaan sikuwahi pata mateso kiasi kile sitasahau. Yaan kuna muda network ilikuwa inapotea au data inajiwasha hata sijaiwasha.
Kukaa na chaji sasa dakika 30 ni nyingi inazimika. Kuna kipindi inazima yenyewe tuu. Yaan niliishi na ile simu kama vile nina mwiba mguuni.
Mimi niliwahi kununua iPhone 5 fake, mateso niliyoyapata sio ya nchi hiiNimewahi nunua samsung s4 ilikuwa ya VERIZON yaan sikuwahi pata mateso kiasi kile sitasahau. Yaan kuna muda network ilikuwa inapotea au data inajiwasha hata sijaiwasha.
Kukaa na chaji sasa dakika 30 ni nyingi inazimika. Kuna kipindi inazima yenyewe tuu. Yaan niliishi na ile simu kama vile nina mwiba mguuni.
2 mifogo ni km 4 hivi na kuendeleaHizo simu ni Jangaaaaa....
kwanza ukiona tuu imefika huku, jua kwa ulaya ANGALAU imetumika miaka 2.
10s pekee ndo chipset ya mtk
Zipo 2
Ivi kuna Mediatek na nyingine zipi?Zipo 2
1) Samsung A10s inatumia MTK P22
2) Samsung A31 inatumia MTK P65
Mediatek, Snapdragon, Exynos...Ivi kuna Mediatek na nyingine zipi?