Kati ya Spika mstaafu Pius Msekwa na Spika Dkt. Tulia nani anasema ukweli kuhusu Ubunge wa Halima Mdee na wenzake 18?

Kati ya Spika mstaafu Pius Msekwa na Spika Dkt. Tulia nani anasema ukweli kuhusu Ubunge wa Halima Mdee na wenzake 18?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mzee Msekwa: Halima James Mdee na wenzake 18 walifukuzwa uanachama wa Chadema kwahiyo hawana chama. Uwepo wao bungeni ni kinyume cha katiba ya JMT ya 1977 niliyoshiriki kuitengeneza.

Dr Tulia Ackson: Halima James Mdee na wenzake 18 ni wanachama wa Chadema hivyo ni wabunge halali kwa mujibu wa katiba ya JMT ya 1977 PAMOJA na marekebisho yake.

Kati ya maspika hawa wawili yupi anasema UKWELI kutoka ndani ya moyo wake huku akimuhofu Mungu wa mbinguni?

Maendeleo hayana vyama!

Pia soma
 
Tulia ni pazia tu pale bungeni. Yuko controlled na ikulu. Eti anasubiri mchakato wa ndani was chama uishe. Watu walishavuliwa uanachama hata kukata Rufaa wamekata sita tu. Walitakiwa waende mahakamani ndio waweke injunction. Spika kilaza kweli, Yani anasubiri Rufaa huku kavuliwa uanachama.
 
Tulia Ni pazia tu pale bungeni. Yuko controlled na ikulu. Eti anasubiri mchakato wa ndani was chama uishe. Watu walishavuliwa uanachama hata kukata Rufaa wamekata sita tu. Walitakiwa waende mahakamani ndio waweke injunction. Spika kilaza kweli, Yani anasubiri Rufaa huku kavuliwa uanachama.
spika kilaza sana ila anajifanya matawi ya juu
 
Tulia Ni pazia tu pale bungeni. Yuko controlled na ikulu. Eti anasubiri mchakato wa ndani was chama uishe. Watu walishavuliwa uanachama hata kukata Rufaa wamekata sita tu. Walitakiwa waende mahakamani ndio waweke injunction. Spika kilaza kweli, Yani anasubiri Rufaa huku kavuliwa uanachama.

Ww na certificate yako ya marketing and banking unajua zaidi ya Dr wa sheria ? Nenda mahakamani basi
 
Wamekoma lini uanachama wao? Na wamekoma Kwa Sababu gani?

Kwanza mchakato wa kuwapa viti maalum haukuwa sahihi. Maana Kuna wagombea was viti maalum na wagombea was majimbo. Wengi walioenda huko ni wagombea wa majimbo na sio viti maalum.

Pia chama huwa kina peleka orodha ya majina ya wagombea viti maalum lakini Hawa hawakuwepo kwenye oridha. Pia chama kiliwafuta uanachama baada ya kwenda kinyume na msimamo wa kutotambua matokeo ya uchaguzi mkuu.
 
Dr wa n
Ww na certificate yako ya marketing and banking unajua zaidi ya Dr wa sheria ? Nenda mahakamani basi

Dr wa mirathi ananizidi Nini? . Shida mnaogopa title isiyokuwa na lolote. Tuna madoctor wangapi wameandikiwa thesis?.

Kuwa doctor haimanishi anajua kila kitu. Mambo mengi yanamshinda. Doctor mzima utasemaje unasubiri mchakato wa chama wakati chama kilishawavua uanachama?. Walitakiwa kusubiria Rufaa wakiwa nje ya bunge na sio ndani ya bunge maana sio wanachama.
 
Bwashee ujue tu kuwa hatuna Bunge Bali kuna kikao cha CCM pale mjengoni. Tulia ni Speaker tu radio iko Magogoni jumba jeupe.
 
Tulia Ni pazia tu pale bungeni. Yuko controlled na ikulu. Eti anasubiri mchakato wa ndani was chama uishe. Watu walishavuliwa uanachama hata kukata Rufaa wamekata sita tu. Walitakiwa waende mahakamani ndio waweke injunction. Spika kilaza kweli, Yani anasubiri Rufaa huku kavuliwa uanachama.
Tulia ni daktari wa sheria.

Usisahau hilo bwashee mchumi!
 
Mzee Msekwa: Halima James Mdee na wenzake 18 walifukuzwa uanachama wa Chadema kwahiyo hawana chama. Uwepo wao bungeni ni kinyume cha katiba ya JMT ya 1977 niliyoshiriki kuitengenez...
1. Huko ni kwenda mbali sana.
2. Jibu la hili swali liko kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania [Ibara 71(1)(e)].
3. Kama walifukuzwa bila kufuata utaratibu, chombo pekee chenye mamlaka ya kujua kama walifuata utaratibu au la si Spika wa Bunge, bali ni mahakama [kwa mujibu wa Ibara 107A(1) & 108(2)].
4. Sasa alichokifanya Spika wa Bunge, alitumia kifungu gani cha Katiba au sheria kujipa hayo mamlaka ya kuwaruhusu waendelee kama wabunge halali?
5. Hata ingekuwa mfanyakazi kuachishwa kazi kinyume cha sheria, Spika wa Bunge asingemrejesha kazini huyo mfanyakazi, bali mfanyakazi aliyefukuzwa kinyume cha utaratibu wa kazi angeenda mahakamani. Huu ndio utaratibu unaofahamika wa kupata haki kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom