Kati ya Tandale na Manzese ni wapi unapoweza kuchagua kuishi?

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
7,799
Reaction score
14,215
Mmeshindaje ndugu zangu. Ikitokea ukaambiwa uchague sehemu moja ya kuishi kati ya Tandale na Manzese ni wapi utapokuwa tayari kwenda kuishi? Na kwanini? Pia ningependa mtu au watu waeleze utofauti wa sehem hizo mbili ki miundo mbinu, kimazingira, kibiashara na pia sehem inayoongoza kwa kuwa na maeneo mengi ya kula bata. Karibuni!
 
Mmeshindaje ndugu zangu. Ikitokea ukaambiwa uchague sehem moja ya kuishi kati ya Tandale na Manzese ni wapi utapokuwa tayari kwenda kuishi? Na kwanini? Pia ningependa mtu au watu waeleze utofauti wa sehem hizo mbili ki miundo mbinu, kimazingira, kibiashara na pia sehem inayoongoza kwa kuwa na maeneo mengi ya kula bata. Karibuni!
Hii sawa na kuuliza Tiptopu na Manzese, Uzuri na Manzese, Kwa mfuga mbwa Manzese Argentina na Manzese.
Wakati Zote ni Manzense. Au kwako wewe Manzense ni eneo gani hasa.
 
Tandale ni Makao Makuu ya Uchawi na Manzese ni Makao Makuu ya Ukabaji kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Tandale kuna Mbu wengi na Manzese kuna Inzi wengi hasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Malaya wa Tandale unaweza Ukawakopa ila wa Manzese Malipo Kwanza.

Uzuri wa maeneo yote Mawili Tandale na Manzese ni kwamba hata ukiwa tu na Tsh 1,000/= unaweza Ukala chakula na Ukashiba ila hakikisha tu Dawa za Flagili hakiko mbali nawe na hukai mbali sana na kilipo Choo.

Tegemea kukutana na Paka wengi wasiokuogopa Tandale na Kukutana na Mbwa wengi Manzese ambao hutowaona muda wote ila ule wako wa Kupika na Kula Chakula chako utawaona.

Tegemea kukutana na Mashabiki wengi sana wa Simba SC, Liverpool FC na Manchester United FC Tandale na wa Yanga SC, Arsenal FC na Manchester City FC Manzese.

Wana CCM wengi utawakuta Tandale na Wapinzani wengi ( hasa CHADEMA ) utakutana nao Manzese.

Kodi za Kupanga za Tandale ni Nafuu ila zina Masharti hasa hasa ukiwa Bachela ila Kodi za Manzese ni juu kidogo ila uzuri wake hupangiwi aina ya Mgeni wa Kumuingiza ndani mwako.

Maduka mengi ya Tandale Condoms ni adimu sana ila Maduka ya Manzese utazikuta nyingi mno.

Misiba mingi inapatikana Tandale ila Majeneza mengi yanapatikana na Kuuzwa Manzese.

Ukitaka ujue kuitafuta Pesa ishi Tandale ila ukitaka ujue Kuhonga vyema ishi Manzese.

Ukitaka kuyajua Matusi mapya kaishi Tandale na ukitaka kuyazoea yale uliyoyasikia tokea ukiwa Mdogo kaishi Manzese.

Magonjwa Sugu ya Tandale ni Gono, Kaswende na Malaria tu ila kwa Manzese ni TB, UTI na UKIMWI kwa sana.

Tandale Kuchunguliwa wakati Unaoga ni Jambo la Kawaida ila kwa Manzese kupigwa Chabo ukiwa Faragha na Mwenza wako si jambo la Kuuliza au hata Kushangaa.

Kwa Mtu wa Kupenda Kujichanganya na kujua hadi Kuzoea Maisha na kuwa Mvumilivu Kimaisha na kwa Wanadamu wenzako maeneo yote haya Tandale na Manzese ni mazuri tu kwa Kuishi.

Binafsi napapenda pote tu Ndugu na nimepamisi mno hivyo nakushauri Kapange katika Nyumba iliyo mpakani mwa Tandale na Manzese.
 
Tandale ni Makao Makuu ya Uchawi na Manzese ni Makao Makuu ya Ukabaji kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Tandale kuna Mbu wengi na Manzese kuna Inzi wengi hasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Malaya wa Tandale unaweza Ukawakopa ila wa Manzese Malipo Kwanza.

Uzuri wa maeneo yote Mawili Tandale na Manzese ni kwamba hata ukiwa tu na Tsh 1,000/= unaweza Ukala chakula na Ukashiba ila hakikisha tu Dawa za Flagili hakiko mbali nawe na hukai mbali sana na kilipo Choo.

Tegemea kukutana na Paka wengi wasiokuogopa Tandale na Kukutana na Mbwa wengi Manzese ambao hutowaona muda wote ila ule wako wa Kupika na Kula Chakula chako utawaona.

Tegemea kukutana na Mashabiki wengi sana wa Simba SC, Liverpool FC na Manchester United FC Tandale na wa Yanga SC, Arsenal FC na Manchester City FC Manzese.

Wana CCM wengi utawakuta Tandale na Wapinzani wengi ( hasa CHADEMA ) utakutana nao Manzese.

Kodi za Kupanga za Tandale ni Nafuu ila zina Masharti hasa hasa ukiwa Bachela ila Kodi za Manzese ni juu kidogo ila uzuri wake hupangiwi aina ya Mgeni wa Kumuingiza ndani mwako.
Umemaliza mkuu, umeongea ukweli mtupu kwa asilimia 100% bigup sana, nimekaa manzese miaka 17, ujasema uongo mkuu.
 
Ishi Tandale inayopakana na Sinza kwa Kanumba utanishukuru
Mmeshindaje ndugu zangu. Ikitokea ukaambiwa uchague sehem moja ya kuishi kati ya Tandale na Manzese ni wapi utapokuwa tayari kwenda kuishi? Na kwanini? Pia ningependa mtu au watu waeleze utofauti wa sehem hizo mbili ki miundo mbinu, kimazingira, kibiashara na pia sehem inayoongoza kwa kuwa na maeneo mengi ya kula bata. Karibuni!
 
Hii sawa na kuuliza Tiptopu na Manzese, Uzuri na Manzese, Kwa mfuga mbwa Manzese Argentina na Manzese.
Wakati Zote ni Manzense. Au kwako wewe Manzense ni eneo gani hasa.
Hapana hizo sehemu ni mbili tofauti na kila moja inajitegemea. Ndo maana kuna Tandale yenyewe, tandale uzuri nk. Pia kuna manzese yenyew na hizo zingine ulizozitaja hapo juu.
 
Back
Top Bottom