Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 38,657
- 44,759
🖕Mawazo ya mjinga
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
🖕Mawazo ya mjinga
Maprof wengi wameisaidia nini Kenya!?Na hii comment ni kigezo kingine kwamba Tz tuna wajinga wengi sana.
Julius alitaka kuwa padre,akakatazwa na askofu wa kizungu na kumtaka aende kwenye siasa....sijui unaunganisha dots!!.. habari za kutukomboa achana nazoUsimlaumu Julius aliyesaidia babu zetu kuwa huru nakupunguza ujinga kwenye bongo zao!!
Siyo jukumu lake kuhakikisha watanganyika wanakuwa ma professor,
Wewe ulifukuzwa shulee au ubongo upoza???
Kwanza tuulize hao tulio nao wamelifanyia nini taifa hili? Pili, kwani mwl. Nyerere ndio anafanya watu wasisome level hiyo au ninukiritimba wa ma lecturer wengi kuzuia wengi wasitoboe.. Maana wengi wao Hawa support wanafunzi wengi ipasavyo, nikama wanataka wabaki wao tu ktk usomi😁😁Tukiambiwa Tanzania ni Nchi ya wajinga hatutakiwi kubisha.
Yaani Taifa lenye watu takribani Milioni 65 linakuwa na Maprofesa 226 huku Full Professors Wakiwa 63 na Associate Professors Wakiwa 163 tuu,na hizi ni takwimu za 2023.
Tukilinganisha na Wenzetu Kenya wao wana maprofesa 1,619 Kwa takwimu za 2019.Kati Yao Full Professors Wakiwa 710 na Associate Professors Wakiwa 979.
Kiufupi Tanzania ni ya Mwisho level Moja na Burundi Kwa kuwa na jamii yenye Elimu Duni(Mbumbumbu) Kwa Kanda ya hapa Africa Mashariki..
Anaetakiwa kubeba aibu hii kwa sehemu kubwa ni Hayati Mwalimu Nyerere maana huyo bwana yeye hakutaka kabisa ku priotise Elimu Kwa sababu anazozijua yeye na in short ni sababu za Kisiasa kuogopa challenges kutoka Kwa Wasomi ndio sababu aliwatia kizuizini na wengine wakakimbilia uhamishoni.
Hakuna shule Mpya alijenga ukiacha za wakoloni Wala kuhangaika kuwaendeleza watu kielimu.Kitu pekee alichofanya ni kuwapa watu Elimu ya UPE waweze kusoma na kuandika Kwa level ya basic education tuu.
Wanyime watu Elimu Ili uweze kuwatawala.Hii tabia imekuwa inafanywa sana na Viongozi wa lile Dhehebu.Bila JK na Sasa Samia kupanuka Elimu ,Tanzania itaendelea kuwa na watu wajinga ambao wanalishwa propaganda na Watawala.
Mathalani JK ndio alianzisha na kukuza sana shule za Sekondari Kila kata,akaalika private sector kuwekeza kwenye Elimu na awamu yake ndio kulianzoshwa vyuo vikuu vingi sana.
Baada ya hapo Rais Samia nae Kwa Sasa anajenga maelfu ya miundombinu ya Elimu,amewaondoa Watoto wa kike kunyimwa Elimu Kwa visingizio vya mimba na anajenga Veta Kila Wilaya na vyuo vikuu Kwa Kila Mkoa ambao hauna Chuo Kikuu walau tuweze kushindana na Dunia badala ya kuogopa Wageni.
My Take
Dunia ya Sasa bila Elimu na maarifa ni kunidanganya,tupeleke Watoto kupata Elimu badala ya kuogopa Wageni Kwa visingizio visivyo na msingi.
---
Dodoma. Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Dk Oscar Ishengoma amehoji idadi ya maprofesa wanaozalishwa nchini na wale wanaostaafu, huku Serikali ikisema hadi kufikia mwaka 2022, Tanzania ilikuwa na maprofesa 226.
Mbunge ataka juhudi za kuongeza maprofesa
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga, amesema: “Profesa ni ngazi ya kitaaluma, ambayo mhadhiri au mtumishi wa taasisi za elimu ya juu huifikia baada ya matokeo ya kazi za kitaaluma ikiwemo kufanya machapisho na ufundishaji,” amesema na kuongeza;
“Hivyo kupanda cheo kwa mwanataaluma kunatokana na jitihada za mhusika katika ufundishaji, kufanya tafiti na kuchapisha maandiko yake katika majarida yanayokubalika kitaifa na kimataifa.”
Kipanga amesema kuongezeka kwa idadi yao kunategemea zaidi jitihadi za mtu binafsi katika utekelezaji wa majukumu yake na kukubalika kwa jitihada hizo kwa wanataaluma wenziwe kwa kuzingatia miongozo waliyojiwekea.
Amesema hadi kufikia mwaka 2022 tulikuwa na jumla ya maprofesa 226, kati yao 163 wakiwa ni maprofesa washiriki (Associate Professors) na 63 ni maprofesa kamili (Full Professors).
Amesema suala la kustaafu linahusu zaidi vyuo vikuu vya umma ambapo umri wa kustaafu ni miaka 65.
Amesema kwa takwimu za mwaka 2022 idadi ya maprofesa kamili waliostaafu ni wanne na wanaotarajia kustaafu kwa mwaka 2023 ni watano, mwaka 2024 ni wawili na mwaka 2025 ni sita.
Kipanga amesema maprofesa washiriki waliostaafu kwa mwaka 2022 ni mmoja na wanaotarajiwa kustaafu kwa mwaka 2023 ni 18, mwaka 2024 ni wanne na mwaka 2025 ni sita.
Katika swali la nyongeza Ishengoma ametaka umri wakustaafu kwa maprofesa kuongezeka kutoka miaka 65 hadi 70, huku pia akihoji kama kuna mpango wa kuongeza maslahi kwa maprofesa ili kuvutia vijana wengi kusoma kufikia ngazi hiyo ambako kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wanahitajika 161 lakini wapo tisa tu.
Akijibu swali hilo nyongeza, Kipanga amesema kuwa suala la kuongeza umri limechukuliwa kwa ajili ya kufanyiwa kazi na suala la maslahi wamekuwa wakiendelea kuongeza.
Mwananchi
Kwanza tuulize hao tulio nao wamelifanyia nini taifa hili? Pili, kwani mwl. Nyerere ndio anafanya watu wasisome level hiyo au ninukiritimba wa ma lecturer wengi kuzuia wengi wasitoboe.. Maana wengi wao Hawa support wanafunzi wengi ipasavyo, nikama wanataka wabaki wao tu ktk usomi😁😁
Mimi ndio professor wa watu wote wa hovyo hapa Tanzania. Asante sana kwa kunipa credit.Ujajibu swali, unaona jinsi gani wewe ni mtu wa hovyo?
Hivi hayawani maana yake niniKwamba wakatoliki ndio wamezuia maprofesa!
Wewe mtoa mada hayawani kweli.
Katoliki imetoa viongozi wengi africa mf kaunda, mugabe n.k ni kwa sababu ya organization yao kielimu.Julius alitaka kuwa padre,akakatazwa na askofu wa kizungu na kumtaka aende kwenye siasa....sijui unaunganisha dots!!..
Ina maana nyingi, moja wapo ni:Hivi hayawani maana yake nini
Hahahaha eti kwa Siri...mkoloni na wazungu wenzie walikua kitu kimojaKatoliki imetoa viongozi wengi africa mf kaunda, mugabe n.k ni kwa sababu ya organization yao kielimu.
Wapo wakatoliki wengi waliosupport harakati za uhuru (kwa siri-kwa kuhofia kupoteza kazi, kwa sababu za kibinadam inaeleweka, na pia kwa wazi). Sasa habari za wao kuandaa watu ili wakandamize elimu kwa waislam, ni muono mfupi sana.
Siyo kweli,hayawani ni wanyama wa poriniIna maana nyingi, moja wapo ni:
mtu asiye na haya!
Mimi ndio professor wa watu wote wa hovyo hapa Tanzania. Asante sana kwa kunipa credit.
Itoshe kusema [emoji1241] tuna maprofesa wa hovyo sana kwanzia kabudi , lipumba, mkumbo ++Wajinga Huwa mnajua mchango wa mtu msomi ni kugawa pesa.
Huyo kabudi amefundisha Wataalamu wengi wa sheria sawa sawa na Lipumba Kwa Wataalamu wa Uchumi,ndio mchango wao.
katika mijadala, epuka sana kutumia neno 'si kweli'. Kwanini? Unajivua nguo kuonyesha jinsi hujui na una kiburi cha ufahamu. Unapotumia neno hilo, ina maanisha una hakika, pasi na shaka usemacho ni sahihi.Siyo kweli,hayawani ni wanyama wa porini
Hayawani neno la kiarabu ambalo kiswahili kimeazima,maana yake wanyama wa mwitunikatika mijadala, epuka sana kutumia neno 'si kweli'. Kwanini? Unajivua nguo kuonyesha jinsi hujui na una kiburi cha ufahamu. Unapotumia neno hilo, ina maanisha una hakika, pasi na shaka usemacho ni sahihi.
Google maana ya neno hayawani, kisha uje ututake radhi hapa.