Kati ya Youtube na Spotify, Apple Music, Deez au Audiomark ni wapi wasanii wanalipwa zaidi?

Hii biashara ya kuuza nyimbo Africa ni changamoto sana...
 
Hii biashara ya kuuza nyimbo Africa ni changamoto sana...
Ni kweli lakini tatizo huwa ni moja,watu wanaifanya kama ulaya wakati huku Africa na tuna sifa za "kipekee za kikwetukwetu".
Nikupe mfano huu, ni ngumu sana kwa mbongo kuingia katika tigopesa/m.pesa yake ahamishe pesa kwenda katika platform labda mdundo au wasafi kipindi kile kisha ndio anunue music,tena a download au ku strean akitumia bundle lake😃.
Lakini hizo zote ukizificha kwa namna flani ikawa katika mfumo wa mara moja matokeo yanaweza kukushangaza,kwa mfano
Platform inafanya makubaliano na sp kama voda katika bundle maalumu la internet linalompa mteja access ya kustream au kudownload nyimbo kadhaa katika platform yenu pamoja na Mb kidogo za kuingia katika few social media.Inakuwa SP ndio anagawana na wewe pay,nimetoa mfano wa haraka.
 
Ukiskip tangazo hailipwi, Mpaka uangalie tangazo Ndio hela inaingia
 
Ukiskip tangazo hailipwi, Mpaka uangalie tangazo Ndio hela inaingia
Ko wanaolalamika Ngoma zao kushushwa view YouTube , tunawasaidiaje sasa , Ngoma zenyewe hazna matangazo, Alli kiba kalalama , konde boy pia nandy
 
Ko wanaolalamika Ngoma zao kushushwa view YouTube , tunawasaidiaje sasa , Ngoma zenyewe hazna matangazo, Alli kiba kalalama , konde boy pia nandy
Mimi sio mtu wa IT, lakini ninavyojua hili suala la kusema mtu "kaibiwa views" linatutia aibu,tunaonekana kama mbumbumbu, hakuna mtu anaweza hack youtube then aanze kupunguza views za mtu mwingine, iko hivi kwa nilivyojisomea na kufahamu: view inahesabika kama mtu ataangalia video kwa sekunde zisizopungua 30, na server wakati huo zipo nyingi zinakuwa zina update kila view bila kuchuja kwa wakati huo huo baadae, mfumo "algorithm" unapitia views ambazo ziko chini ya sekunde 30, au ambazo zinaonekana kama ni za kujazia na "robots" zinaondolewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…