KATIBA: CCT nao watoa tamko!


Will attach the image file, nilijua wanaotumia simu watadai hawaioni
 
Hadi raha haya mapambano ya wana science wa dot.com mafisadi hadi kucha zinatoa jasho teh teh!
 
This is exactly what i told the fellas the other day.
Kama kauli hiyo hiyo ikitolewa na kiongozi wa dini yake ina make sense zaidi,basi why not BAKWATA na wengineo wasiwawakilishe waumini wao wenye kuamini kauli zao kwenye mchakato.Ili tupate katiba mpya kwa amani kama watanzania.
 
Tanzania au Tanganyika kwanza na imani baadae!

Nimependa sana tamko hili,ila nijuavyo mimi ni kwamba serikali na JK wote wametia pamba masikioni!

Kubaka kwao hoja ya katiba mpya kumewafanya wakurupuke na speed ya ajabu isiyokuwa na umakini wowote kutaka kuleta illusion kwenye katiba!

Haiwezekani watu walio simama kidete kusema hakuna haja ya katiba mpya,...kombani,werema leo ndo wanakimbia wakiwa wamebeba muswada wa mapendekezo ya katiba mpya,...ni uongo na udanganyifu mkubwa kwa watanzania!

Kama fisi usivoweza kumuamini fisi kukulindia bucha, huwezi waamini kombani/werema + JK kwamba watakupa katiba mpya au kusikia kilio cha nini kifanyike sasa, sidhani ila so far CCT wametimiza wajibu wao, hawana lawama!
 
Na wale wasio na dini lini watatoa tamko! Na mtu mmoja mmoja ni lini wataanza kutoa matamko? Haya matamko yanapoteza mulekeo yaani kila kitu ni Tamko ni km zile tume zisizo na ufanisi ziundwazo kila siku.
 
Well said CCT, u've done ur part very well. Let's wait and see...

It will be superb if our BAKWATA will also come with something of their own on this matter.
 

Cha kupoteza anacho tena kikubwa tu, ni ulinzi wa ufisadi wa swahiba zake na mali zake pia.
 
Wakiurekebisha mswada uendane na milio thabiti ya waTANZANIA itawatesa sana! Wakiuacha bila kuruhusu vilio vya watanzania viamue kweli njia na uzima, TANZANIA itakwisha. Nawaomba MODS maneno haya yabaki kama kumbukumbu. Mwenyezi Mungu atubariki.
 
jamani ccm muone aibu kutuchagulia tume ya katiba sisi wananchi. tunataka tume ichaguliwe na wananchi wenyewe kwa kupitia wawakilishi wao. katiba si mali ya ccm, si mali ya rais kikwete. kama kweli wana masikio hawa binadamu tunaomba waskie kilo cha wananchi
 
Huwezi kuzuia propaganda za udini kwani wajinga duniani hawataisha hata kama nao ni viongozi wana aina fulani ya ujinga wakati watu tunazungumzia mambo ya kitaifa utawasikia mara yeye askofu anaongea kama nani mara or kama anataka siasa avue majoho, hilo halitutishi sisi tutaunga mkono mtu yeyote anaetetea maslahi ya nchi bila kujali ni kiongozi wa dini wa wacheza madogoli haituhusu ila kwa wajinga hiyo kwao ni isue
 
Na wale wasio na dini lini watatoa tamko! Na mtu mmoja mmoja ni lini wataanza kutoa matamko? Haya matamko yanapoteza mulekeo yaani kila kitu ni Tamko ni km zile tume zisizo na ufanisi ziundwazo kila siku.
Wewe ni mjinga wa mwisho unafikiri askofu kazungumza kama yeye amewakilisha watu!! kuhusu mtu mmoja mmoja kutoa maoni ndicho hawa viongozi wanapigia kelele kwamba kuwe na uhuru na muda wa kutosha kwa watu kutoa maoni yao!! sasa ambacho kinakusumbua hapa ni nini?

Crapiest!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!11
 
Hongera sana bishop Valentino Mkiwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania kwa ujumla kwa kuona udhaifu huo naomba mtetee wananchi kwa hali na mali haijalishi itawaghalimu nini
 
CCM wamekuwa vipofu wa kuona ukweli na uhalisi wa mambo. Huwezi ukahodhi matakwa ya wananchi na kulete gheresha ukitarajia kukidhi matakwa yao. Hiyo "katiba gheresha" haitamaliza kiu ya wananchi ya kutaka katiba mpya. Hitaji litakuwepo tu mpka wananchi watakapopata kile wanachokitaka. Au wanataka tuwe tunaandika katiba kila mwaka? Doesn't make sense.
 
Tuendelee tukaikomboe nchi, ni lazima ipatikane katiba ya kuridhisha matakwa ya watanzania wa sasa na vizazi vijao! Hawa CCM waache kutuwekea giza.
 

Jamani naomba tusiwatuhumu BAKWATA maana hawajaongea tukawasikia kwa hili. pia tusiwadhanie vibaya, maana wanaweza kuja na hoja nzuri za kuleta ushawishi na mafanikio.
Ila kila mmoja wetu anapaswa kukumbuka kuwa tanzania ni nchi. na nchi ina watu na watu wamegawanyika katika makundi na taasisi mbalimbali. Makundi hayo hayawezi kutengwa hata kidogo katika jambo muhimu kama hili, hata wafungwa, makahaba, wezi na wachawi wana haki ya kuchangia katika hili, sembuse taasisi za kidini?
Mtu yeyote anayetaka kusema kuwa viongozi wa dini hawana haki ya kutoa tamko huyo amefilisika kisera. Viongozi wa dini wanaongoza watu walewale tunaokutana nao kwenye siasa, makazini, kwenye mabunge, kwenye chaguzi n.k ndio hao walio makanisani, misikitiki na kwenye matambiko. Sasa tunawekaje mipaka katika hili?
Lakini pia Taasisi hizi zimeundwa na zinafanya kazi tanzania kwa mujibu wa sheria za tz ambapo katiba ndio sheria mama. Hivyo taasisi yeyote ya kidini inayojishaua kuwa haijiingizi kwenye mchakato wa katiba kwa namna moja au nyingine hiyo ni taasisi mfu. maana Katiba ndio inaruhusu uwepo wa taasisi hizi hapa nchini. Sasa kujitoa na kuwaachia mafisadi si sawa na kumsaliti mama yako mzazi?

MIMI NAWAPONGEZA VIONGOZI WA DINI AMBAO WAMESHATOA MATAMKO YAO NA NAWAOMBA WALE AMBAO HAWAJATOA WATOE HARAKA KABLA MAMBO HAYAJAHARIBIWA NA MAFISADI. NA HAPA UNAFIKI LAZIMA UWEKWE PEMBENI
 
Na wale wasio na dini lini watatoa tamko! Na mtu mmoja mmoja ni lini wataanza kutoa matamko? Haya matamko yanapoteza mulekeo yaani kila kitu ni Tamko ni km zile tume zisizo na ufanisi ziundwazo kila siku.

Toa upuuzi wako hapa. Upuuzi huo kautoe kwenye mbao za chama.
 
Nchi hii ni yetu sote. Tuache ubinafsi, ni lazima tukae kwa pamoja na kuamua tunataka Tanzania ya namna gani. Kwa kushirikisha watu wenye nchi yao katika mchakato wa katiba mpya kutaleta amani na utulivu.
 
Kaka hapo umenena wala hapo hakuna unafiki!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…