Jamani naomba tusiwatuhumu BAKWATA maana hawajaongea tukawasikia kwa hili. pia tusiwadhanie vibaya, maana wanaweza kuja na hoja nzuri za kuleta ushawishi na mafanikio.
Ila kila mmoja wetu anapaswa kukumbuka kuwa tanzania ni nchi. na nchi ina watu na watu wamegawanyika katika makundi na taasisi mbalimbali. Makundi hayo hayawezi kutengwa hata kidogo katika jambo muhimu kama hili, hata wafungwa, makahaba, wezi na wachawi wana haki ya kuchangia katika hili, sembuse taasisi za kidini?
Mtu yeyote anayetaka kusema kuwa viongozi wa dini hawana haki ya kutoa tamko huyo amefilisika kisera. Viongozi wa dini wanaongoza watu walewale tunaokutana nao kwenye siasa, makazini, kwenye mabunge, kwenye chaguzi n.k ndio hao walio makanisani, misikitiki na kwenye matambiko. Sasa tunawekaje mipaka katika hili?
Lakini pia Taasisi hizi zimeundwa na zinafanya kazi tanzania kwa mujibu wa sheria za tz ambapo katiba ndio sheria mama. Hivyo taasisi yeyote ya kidini inayojishaua kuwa haijiingizi kwenye mchakato wa katiba kwa namna moja au nyingine hiyo ni taasisi mfu. maana Katiba ndio inaruhusu uwepo wa taasisi hizi hapa nchini. Sasa kujitoa na kuwaachia mafisadi si sawa na kumsaliti mama yako mzazi?
MIMI NAWAPONGEZA VIONGOZI WA DINI AMBAO WAMESHATOA MATAMKO YAO NA NAWAOMBA WALE AMBAO HAWAJATOA WATOE HARAKA KABLA MAMBO HAYAJAHARIBIWA NA MAFISADI. NA HAPA UNAFIKI LAZIMA UWEKWE PEMBENI