KATIBA: CCT yawasha moto

Hongera sana cct kwa kusema ukweli katiba mpya ni ya watanzania wote bila kujali itikadi zao za chama.
 
Nani aliyeweka udini kwenye ilani na kuunadi? kwa mara ya kwanza ni kikwete!
 
Utawala wa nchi si sawa na uendeshaji misikiti kaka. Funguka mawazo na akili yako!
 
Madrasa al sul al jihad! Tekibir
 
Na lile kanisa la Rawakatale nalo limo kwenye umoja huo wa CCT?

Hapana kanisa la Rwakatare halipo kwenye CCT.
Makanisa yanayounda CCT ni

. Evangelical Lutheran Church in Tanzania (ELCT)
2. Anglican Church Tanzania (ACT)
3. Moravian Church in Tanzania (MCT)
4. Africa Inland Church Tanzania (AICT)
5. Mennonite Church in Tanzania (MCT)
6. Baptist Conventional Church in Tanzania
7. Salvation Army
8. Church of God
9. Presbyterian Church of East Africa
10. Kanisa la Biblia
11. Mbalizi Evangelistic Church
12. Methodist Church
13. Christian Brethren Assembly
14. African Brotherhood Church
15. Tanzania Yearly Meeting
 
Kanisa la getrude rwakatare halipo cct wala pct wala tag. Yeye yupo peke yake . Mwaka 2007 alipo pata ubunge alitaka kumukabidhi askofu rainwell mwenisongole lakini akapwea masharti kuwa aachie utawala wote uwe chini ya tag . Yeye akataka kumwacha mch katembo ambaye angemdai sadaka kwa urahisi lakini tag wakagoma.
Rwakatare alipo ona sadaka zinakwenda tag akakataa mpango huo mpaka leo
 
Umoja wa makanisa ya kikristo imetoa tathimini ya uchaguzi mkuu na kusema kuwa lazima katiba iandikwe upya.huu ni mwendelezo wa moto unaowaka chini kwa chini wa kudai katiba mpya,hongera sana cct sasa twasubiri bakwata nao watoe tamko

Viongozi wa Bakwata wanaweza kuitiwa mpunga pale Ikulu na kisha kupewa vijisenti na kuambiwa watoe tamko kwamba Waislamu hawaoni umuhimu wa katiba mpya kwa kuwa hii iliyopo haina matatizo yoyote na wakafanya hivyo bila matatizo yoyote.

 

Matola UNATISHA KAMA NJAA . . .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…