Wakusoma 12
JF-Expert Member
- Jul 3, 2017
- 4,035
- 11,462
Ndugu zangu bado tupo katika majonzi makubwa kama taifa ya kumpoteza kiongozi mkuu.
Yote juu ya yote Mungu atatusimamia nalo litapita.
Nachotaka kusema hapa ni huu utaratibu wa katiba kumtambua makamu wa Rais kama rais iwapo Rais aliyepo madarakani atafariki. Hii ni hatari kwani itatokea siku moja makamu asiye mwaminifu, lakini pia tunafahamu fika namna ilivyokuwa kazi ngumu kupata urais katika nchi za Kiafrika.
Hivyo kulingana na hali hii makamu wa Rais anaweza kutumiwa kama ngao na baaadhi ya watu wasio waaminifu na kumdhuru Rais ili kujitwalia madaraka. Hivyo kwa kutambua umuhimu wa nafasi nyeti ya urais ni bora makamu wa rais aruhusiwe tu kuwa Rais kama kipindi cha rais aliyekufa kitakuwa hakizidi mwaka mmoja na iwapo rais atafariki akiwa madarakani na muda wa uongozi wake utakuwani bado unazaidi ya mwaka mmoja mbele ili kukamilika basi, serikali ya mpito iundwe na kiongozi wake awe makamu wa Rais na ahitishe uchaguzi wa Rais ndani ya miezi 6.
Tunajifunza kutokana na makosa.