Ninahisi Mwanakijiji anamaanisha kuwa, kila kukicha wana zidi kutokea watu ambao wanataka kutuaminisha kuwa hakuna Rais bora kama Kikwete, na haswa kipindi hiki tunapoelekea kwa uchaguzi. Hata Makamba alisema Kikwete ndio mtaji wa CCM (REDET study). Na wengine wamehongwa ili watutishe kuwa atakayejitokeza kupingana na Kikwete 2010 basi atakufa ghafla.
Kama ni hivyo, na kama wote tunajiaminisha Kwelikweli kuwa this guy ni chaguo la Mungu, maana huwezi kuwa na sifa hizi zote afu ukaishia kwa vipindi viwili tu, Basi ndio maana Mwanakijiji anasema, tumpe Ruhusa (tubadili katiba) atuongoze maisha.
Vinginevyo kama kuna watu mbadala na tunajua wapo (what if this man dies - Mungu apishe mbali), tunawahitaji wajitokeze! Ili hizi blah blah za vibaraka hawa uchwara ziishe. Nchi inaongozwa kidemokrasia bwana, na hata kama sisi hatutaki, the wind of change itatuswaga na kutulazimishe tuelekee huko.