Pre GE2025 Katiba ibadilishwe kumuzesha Rais kutimiza maono yake ya kuipaisha nchi yetu kiuchumi awamu iwe miaka 7 ukomo nafasi husika ya uondolewe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Katiba ibadilishwe kumuzesha Rais kutimiza maono yake ya kuipaisha nchi yetu kiuchumi awamu iwe miaka 7 ukomo nafasi husika ya uondolewe


Wadau hamjamboni nyote?

Nawaslisha maoni yangu nikizingatia haki yangu ya kikatiba na maslahi mapana ya taifa letu tukufu la Tanzania

Upo ulazima wa kubadili katiba yetu na kuondoa ukomo wa Rais kuhudumu & kuongeza muda wa awamu moja kuwa miaka 7 badala ya miaka 5 ya sasa

Muda uliopo kikatiba hautoshi kabisa kumuwezesha Rais aliyepo madarakani kutimiza kikamilifu maono yake na hivyo itakuwa vigumu sana kupiga hatua kimaendeleo

Uzoefu unaonyesha Viongozi waliopewa muda wa kutosha kikatiba walifanikiwa pakubwa kuziletea nchi zao maendeleo ya kiuchumi

Pia soma:
Kuelekea 2025 - CCM Zanzibar wapendekeza Rais Mwinyi atawale kwa miaka 7, wasema kufanya uchaguzi 2025 ni hasara na matumizi mabaya ya fedha za umma

Mfano mzuri

Angela Dorothea Merkel aliyezaliwa 17 Julai 1954 na kuhudumu akiwa Chancellor wa Ujerumani kwa miaka 26 kuanzia 2005 to 2021.

Helmut Josef Michael Kohl aliyezaliwa tarehe 3 April 1930 na kufariki Tarehe 16 June 2017 alihudumu akiwa Chancellor wa Ujerumani kwa miaka 17 kuanzia 1982 to 1998.

Viongozi wote hao waliiletea Ujerumani mafanikio makubwa sana kiuchumi na hii ni kutokana na Katiba ya nchi hiyo kuondoa ukomo wa kuhudumu kwenye nafasi hiyo.

Ukitazama Katiba za nchi kubwa kidemokrasia na kiuchumi hazina ukomo Kwa mfano Uingereza , Israel, Ubelgiji, Italy, Uholanzi n.k

Ni wakati muafaka muswada upelekwe bungeni kuongeza muda wa awamu moja kuwa miaka 7 badala ya 5 na kuondoa ukomo wa kuhudumu kwenye nafasi hiyo

Niwatakie ijumaa njema
 
Atawazwe kuwa Malkia kabisa atawale hadi kifo baada ya kifo Abdul anatawazwa kuwa Mfalme.
 
Kikwete angeendelea bila ukomo wa kikatiba, JPM na Samia ungewajulia wapi?
Kesho ni mbali sana kwa maisha ya binadamu, lolote linaweza kutokea,
Rejea Rais wa Iran,
 
Mwenzake miaka mitatu tu alijenga mafly over, mabarabara, sgr, JNHEP, Tanzanite bridge, Kigogo - Busisi bridge, JK Airport terminal 3, Dar es salaam bus stand n.k Huyu mpaka sasa anasema kuleni kwa urefu wa kamba😄🙌
Sasa huyo Jiwe si alikuwa anaiba pesa za wananchi na kujinufaisha yeye. Mara mia huyu kuliko yule japo simkubali baada ya kuona na yeye anajinasibu na Bashite
 
Ndugu mleta mada,nijuavyo mimi maono ya mtu hukoma pale maisha yanapo koma,hapa wazo lako ni kutaka kusema enzi za ufalme au umalkia uanza🤔
 
Tatizo mkishaapishwa tu mnawaza uchaguzi ujao Hamuwazi njia mbadala ya kumlinda mkulima na mazao

Kwa ninavyoona hata katiba mpya ikija watakuwa wameongeza vipengele vingi sana vya kuwalinda hakuna cha maana.
 
 

Attachments

  • IMG_6223.jpeg
    234.2 KB · Views: 2
Samia alisema anapenda kupita jf naanza kupata mashaka kaamua kufungua na Id kabisa
 
Halafu huyo rais awe ni Tundu Antipas Lissu .
 

View: https://www.youtube.com/live/1sdw-v-PZII?si=W4zQ2Yd1d5DdnbD-
 

View: https://www.youtube.com/live/1sdw-v-PZII?si=W4zQ2Yd1d5DdnbD-
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…