Katiba ifanyiwe marekebisho, marais wastaafu waruhusiwe kugombea tena

Kwa Jk huyu aliyekuwa antukanwa kila siku???? Wengi walimchukia kwa kupitia dini, sasa kapitikana mwenye dini husika tupige kazi, tumuache ampumzike mzee wetu JK
 
kipindi hicho sisi wanyonge tuliumia sn enzi za Jk usiturudishe utumwani Misri tena ...nadhani mtoa mada alikuwa mnufaika wa enzi za Jk sasa mirija imekatwa anaanza kuleta hbr za kulialia ...fanya kazi kijana enzi za kuiba ziliisha ni mwendo wa kula kwa jasho lako
 
ni wenye akili finyu tu ndio hufikiri ujinga huu, virais vibabu babu hatuvitaki hapa nchini...inchi ina vichwa vingi na vingi vinazaliwa na utashi mpya ambao watangulizi hawana hata idea. Nakushauri utulie hukohuko na mawazo ya kale hayo...sisi tunasonga mbele aisee
 
Aliyepo akivuruga, aondoke baada ya miaka 5. Hiyo siyo sababu ya kutamani walioishiwa mawazo baada ya miaka yao 10 ya utawala. Tanzania ina watu milioni zaidi ya 50.

Kwa akili yako, unaamini Mkapa na Kikwete wanakuzidi wewe na mimi na mwingine na hakuna mwingine?
 
Wana bodi salaam, Hakika ingependeza tena tungemuona JK kwenye harakati za kuwania tena hii nafasi, sio kwamba ni mkamilifu sana au kwenye uongozi wake hakuwa na dosari, ila dosari za awamu ya tano zimezidi kuvuka mipaka.

Unajua tatizo ni nini Mkuu? Ukitoka kumeza chloroquin, utaona limao ulilokula jana ni tamu sana huenda hata kuzidi chungwa ulilokula juzi.
 
Mkuu, kwani kwasasa Katiba inakataza Marais wastaafu wasigombee tena Urais au Ubunge? Isome kwanza Katiba. Kinachokatazwa ni kuchaguliwa zaidi ya vipindi viwili mfululizo.
sawa mkuu, katiba ninayo, upo sahihi uliposema kinachokatazwa ni zaidi ya vipind viwil mfululizo... lakini kwa kuzingatia hakuna hilo katazo, ingefaa kifungu kiwekwe kwani mgombea husika akitaka kugombea kusiwe na maneno maneno.
 
Inaonekana watanzania wengi uwezo wa kufikiri unapungua siku hadi siku.

Hii mada ni ushahidi tosha.
Mimi nimemwelewa mtoa mada vizuri. Ulishasikia uwasilishaji wa ujumbe kupitia "sarcasm"? Ndio huu.
 
Yan hawa waliotuletea haya mateso uwaweke tena!??
Kama kuna mjomba ako kat ya hao....na kakwambia ulete mjadala
Mtuacheeee jamani stress tulizonazo znatosha
 
Yaani. Bora wamuache Mzee apumzike tu. Alikuwa na madhaifu yake lakini hata kwa Yale mazuri aliyofanya alidhihakiwa. Hata huyu kipindi chake kitapita.
Huyu tuna mpango wa kumuongeza miaka saba hii mitano haitoshi
 
Tuanzie kwenye vyama slaa arudishiwe ukatibu wake
 
maamuzi magumu huku wananchi wanalima lami ?
Hata lami inaweza ikakuzalishia kipato kama utafikiri nje ya box. Ukishidwa kupambanuwa hili, hata ije serikali ya malaika haitakusaidiaka.
 
kwanza hata muonekano wake ..una muonyesha kuwa nimtu makini anayejitambua na Mwenye weledi wakufikiri ...alikuwa amefaulu mnooo kuitangaza Tanzania kimataifa ..ktika wakati wa utawala wake niyeye tu aliyefanikiwa kuwaleta waliokuwa maraisi wa mareakani wastaafu (George bush ..Clinton) na Obama ambaye alikiwa anakaimu na fasi ya uraisi kwa wakati huo "" hapa inaonyesha wazi kuwa Jamaa alikuwa kiunganishi mzuri wa taifa letu dhidi ya mataifa na alikuwa na akili ya kibiashara pia ....
 
nimemulewa mnoo mtoa mada ..yaani anaona niangalau nchi hii kuongozwa tena na watu hao endapo watu wengine wakuiongoza nchi watakuw hawapo ..kuliko nchi kuendelea kuongozwa na huyu mtusi
 
nimemulewa mnoo mtoa mada ..yaani anaona niangalau nchi hii kuongozwa tena na watu hao endapo watu wengine wakuiongoza nchi watakuw hawapo ..kuliko nchi kuendelea kuongozwa na huyu mtusi
mtusi ni hatari kwa afya mkuu...... nchi inaserereka kusikojulikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…