Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aliyepo akivuruga, aondoke baada ya miaka 5. Hiyo siyo sababu ya kutamani walioishiwa mawazo baada ya miaka yao 10 ya utawala. Tanzania ina watu milioni zaidi ya 50.huyo unaedhani yupo ama anafaa ana masilahi gani kwako kama raia na taifa kwa ujumla ? uchumi unaserereka tu kila siku, kazi kupika data, imeishia kuwa serikali ya matamko, mabank yanafunga kwa kushindwa kujiendesha, uhuru wa maoni kuminywa, demokrasia ya maandishi lakini kivitendo sio, watu kutekwa, kuuwawa, kupigwa risasi ndicho unachokitaka ?
what a shame.
Wana bodi salaam, Hakika ingependeza tena tungemuona JK kwenye harakati za kuwania tena hii nafasi, sio kwamba ni mkamilifu sana au kwenye uongozi wake hakuwa na dosari, ila dosari za awamu ya tano zimezidi kuvuka mipaka.
sawa mkuu, katiba ninayo, upo sahihi uliposema kinachokatazwa ni zaidi ya vipind viwil mfululizo... lakini kwa kuzingatia hakuna hilo katazo, ingefaa kifungu kiwekwe kwani mgombea husika akitaka kugombea kusiwe na maneno maneno.Mkuu, kwani kwasasa Katiba inakataza Marais wastaafu wasigombee tena Urais au Ubunge? Isome kwanza Katiba. Kinachokatazwa ni kuchaguliwa zaidi ya vipindi viwili mfululizo.
Mimi nimemwelewa mtoa mada vizuri. Ulishasikia uwasilishaji wa ujumbe kupitia "sarcasm"? Ndio huu.Inaonekana watanzania wengi uwezo wa kufikiri unapungua siku hadi siku.
Hii mada ni ushahidi tosha.
maamuzi magumu huku wananchi wanalima lami ?Ukiona Rais akingia madarakani akawa anapendwa na kusifiwa kwa mapambio, hujuwe huyo sio Rais wa maamuzi magumu.
Huyu tuna mpango wa kumuongeza miaka saba hii mitano haitoshiYaani. Bora wamuache Mzee apumzike tu. Alikuwa na madhaifu yake lakini hata kwa Yale mazuri aliyofanya alidhihakiwa. Hata huyu kipindi chake kitapita.
Tuanzie kwenye vyama slaa arudishiwe ukatibu wakeWana bodi salaam,
Katiba yetu sio Msahafu/Biblia, nikiwa na maana muda wowote inaweza fanyiwa marekebisho pale inapohitajika kwa maslahi ya taifa yenye tija. Hili tumekuwa tukiliona likitokea kwani kufikia sasa katiba yetu imeshafanyiwa marekebisho mara kadhaa, pia nadhani hili linaweza kuendelea.
Naam, ninaona kuna haja ya kurekebisha katiba yetu, ili maraisi wastaafu waruhusiwe kugombea tena nafasi hiyo, pale watakapohisi wanaweza kufanya hivo, baada ya wao kujitosa kwenye kinyang'anyiro sisi wananchi ndio tutawapima kama tunaweza kuwaamini na kuwapa tena mamlaka ya kuliongoza taifa letu ama la.
Kwa hapa kwetu tunao maraisi wastaafu watatu ambao ni Mzee Mwinyi A.H, Mzee Mkapa B.W, na Mzee Kikwete J.K. kwa uhalisia Mzee Mwinyi amezeeka kwa umri wake (miaka 90 na kuendelea), lakini kwa hawa wawili bado nguvu zipo, zaidi kwa JK bado anaonekana anaweza kabisa kuongoza zipo.
Hakika ingependeza tena tungemuona JK kwenye harakati za kuwania tena hii nafasi, sio kwamba ni mkamilifu sana au kwenye uongozi wake hakuwa na dosari, ila dosari za awamu ya tano zimezidi kuvuka mipaka.
Enzi za JK;
-Wafanyakazi waliboreshewa maslahi, walipanda madaraja kwa wakati na kupata stahiki zao
-Demokrasia ilikuwepo ya kweli, hivi kwa ungozi huu wa JPM , kina slaa wangepata mwanya wa kuandaa mkutano wa kisiasa nchi nzima, sijui mambo ya kushukuru wanachi kwa kuwapigia kura ? mambo ya list of shame mnazi mmoja ? wangekaripiwa kwa makatazo, na wangeishia kuswekwa jela kwa kesi za uchochezi, lakini JK hakuwa anahaingaika nao, anawaacha wanatoa ya moyoni maisha yanaendelea.
-Mishahara ilikuwa inatoka kwa wakati, longolongo hazikuwepo
-Ajira zilikuwepo, japo hapa naomba nikiri kwamba aliweza kuajiri kwa kiasi chache kulingana na uhitaji na bajeti. Nikiri tatizo la ajira limekuwa sugu hata huko nchi za watu japo tatizo sio kubwa kama nchi za ulimwengu wa tatu mfano Tanzania. Hata USA, England, Germany na kwingineko hili tatizo lipo lakini huwezi kulinganisha na bongo.
-Uhuru wa habari ulikuwepo.
-Alijitahidi kujenga mahusiano mazuri na wapinzani, kuwaita kukaa nao pamoja na kujadili baadhi ya mambo yenye maslahi kwa nchi. Mara ngapi kina ZZK, Mbowe, Slaa, Lipumba wameenda ikulu na kunywa chai na mheshimiwa JK huku wakijadili mambo ya taifa letu ? vipi kwa huyu wa sasa ?
-Walau uchumi ulikuwa wastani, mambo yalikuwa yanaenda sio kama sasa, pesa ilikuwepo kwenye mzunguko. kwa kipindi hiki mambo yamebadilika sana.
-Miradi ya maendeleo ilikuwepo na ilifanyika vizuri kabisa, mifano mnayo.
Kwa kifupi hayo niliyoorodhesha hapo na mengine mengi ni baadhi ya mazuri ya JK, nchi ilikuwa na usawa, kila mtu alikula kwa namna yake, haki za binadamu zilizingatiwa n.k
Kwa nini katiba isirekebishwe hiki kipengele cha wastaafu waruhusiwe kugombea tena kikawekwa? hakika JK akijitosa tena atashinda kwa kishindo kikubwa sana.
Huyu mzee wetu ni mwanasiasa haswa, master mind, anajua afanye nini kwa wakati gani, hakurupuki na anapokea ushauri, kwa kifupi yupo smart sana na maamuzi anayoyafanya.
huyu hapana, mpaka sasa keshaharibu sanaKwa maana JPM ifika 2025 apewe tena nafasi!!!!
Hata lami inaweza ikakuzalishia kipato kama utafikiri nje ya box. Ukishidwa kupambanuwa hili, hata ije serikali ya malaika haitakusaidiaka.maamuzi magumu huku wananchi wanalima lami ?
kwanza hata muonekano wake ..una muonyesha kuwa nimtu makini anayejitambua na Mwenye weledi wakufikiri ...alikuwa amefaulu mnooo kuitangaza Tanzania kimataifa ..ktika wakati wa utawala wake niyeye tu aliyefanikiwa kuwaleta waliokuwa maraisi wa mareakani wastaafu (George bush ..Clinton) na Obama ambaye alikiwa anakaimu na fasi ya uraisi kwa wakati huo "" hapa inaonyesha wazi kuwa Jamaa alikuwa kiunganishi mzuri wa taifa letu dhidi ya mataifa na alikuwa na akili ya kibiashara pia ....
nimemulewa mnoo mtoa mada ..yaani anaona niangalau nchi hii kuongozwa tena na watu hao endapo watu wengine wakuiongoza nchi watakuw hawapo ..kuliko nchi kuendelea kuongozwa na huyu mtusiMawazo ya aliyekufa hayo! Unatamani kuongozwa na Mkapa na Kikwete ili walete jambo gani? Anapoambaiwa imetosha maana yake siyo kwamba amezeeka, NO! Tafsiri yake ni kwamba hana jipya kichwani!
Wewe unamtamani MKapa kwa lipi? Kikwete kwa lipi? Ushoga na urafiki uishie nje ya mfumo wa serikali, bhana!
mtusi ni hatari kwa afya mkuu...... nchi inaserereka kusikojulikana.nimemulewa mnoo mtoa mada ..yaani anaona niangalau nchi hii kuongozwa tena na watu hao endapo watu wengine wakuiongoza nchi watakuw hawapo ..kuliko nchi kuendelea kuongozwa na huyu mtusi