Katiba ikibadilishwa, mtasingizia nini tena?

Katiba ikibadilishwa, mtasingizia nini tena?

Ujue sisi uelewa wetu mdogo sana. Kama katiba ingempa nguvu mwananchi basi viongozi wa nchi wangeogopa kuleta unyumbu maana wangeogopa kupewa adhabu na raia. Alafu si Kila anayeingia madarakani ni mzalendo, wengine wanaenda kujinufaisha wao na jamaa zao. Kama tutakua Na katiba yenye kumpa raia wa kawaida, heshima itakuwepo kwenye uongozi. Ndio maana tulishuhudia madudu kwenye secta nyingi lakini tulishindwa kufanya maamuzi kwakua hatuna nguvu kikatiba. Leo hii jecha kafuta uchaguzi na matokeo yake zanzibar kwa sababu ya katiba. Sasa mnashindwaje kuelewa umuhimu wa katiba? Au ndo tuseme nyie ni Ccm kindakindaki
Ndugu yangu katiba is all about formalities of ruling, ni do's and dont's za uongozi. Rwanda ni nchi yenye katiba mbovu pengine kuliko zote barani Afrika, lakini kazi kubwa aliyofanya Paul Kagame haina uhusiano wowote na katiba, alichofanya ni kuhakikisha zile economic goals zinafikiwa, hajagusa kabisa katiba. Kwanini tunapoteza nguvu nyingi kwenye siasa wakati we are still so poor?. Kuna fursa nyingi sana za kimaendeleo, hizo ndizo zingekuwa mijadala badala ya kujenga dhana kuwa katiba ndio kila kitu, sio kweli hata kidogo. Utumbuaji majipu una uhusiano gani na katiba? Tatizo letu lipo kwenye uchumi na sio siasa. Tatizo letu kubwa lipo kwenye uwezo wetu mdogo wa kuvumbua talents za watu katika nyanja zote za maisha. Tatizo letu lipo kwenye dharau dhidi ya taaluma za watu na sio katiba. Tunayo matatizo ya msingi ambayo kama yatapatiwa uvumbuzi na uhakika wala hautaizungumzia hiyo katiba.
 
Haujaelewa hasa ninachommanisha, kama tatizo ni Katiba mbaya, ni kwa nini nchi ambazo zinatumia Katiba kama yetu zimeendelea, tena sana Tu?
Ndio maana nakumbia tatizo sio katiba mbaya peke yake, ila katiba nzuri ni moja ya ingredients za kuleta maendeleo! Kwa maana nyingine hata ukiwa na katiba nzuri namna gani bila kufanya vitu vingine maendeleo hayatakuja yenyewe! Lakini hili haliwezi kuwa sababu ya kutokuwa na katiba nzuri. Wewe una mawazo kama wale wazee wa vijijini wanaosema ''kama sigara zinaleta kansa mbona fulani alivuta mpaka akazeeka bila kupata kansa. Haya sio mawazo ya mtu aliyeenda shule akaelimika.
 
Tatizo lenu ni kwamba mnafikiri Katiba ni mashine ambayo unabonyeza kitufe basi inafanya abc, HAPANA!
Katiba ni Karatasi yenye maandishi ambayo unayasoma na inahitaji binadamu sasa kuyatii na kuyafanya yale yalioandikwa kwende hiyo karatasi, na sasa hapo ndipo tatizo lilipo huyo Binadamu atakaye tii na kufwata hayo maandishi kwenye karatasi atatokea wapi? Ni huyu huyu yaani tuliyeopo hata TanZania au atatokea Mars?
Inaelekea wewe ndio unafikiria hivyo! Kwa watu wenye uelewa wa katiba katu hawawezi kufikiria katiba ni kitufe cha kubonyeza ulete maendeleo. You have got theiir arguments wrong!
 
Ndio maana nakumbia tatizo sio katiba mbaya peke yake, ila katiba nzuri ni moja ya ingredients za kuleta maendeleo! Kwa maana nyingine hata ukiwa na katiba nzuri namna gani bila kufanya vitu vingine maendeleo hayatakuja yenyewe! Lakini hili haliwezi kuwa sababu ya kutokuwa na katiba nzuri. Wewe una mawazo kama wale wazee wa vijijini wanaosema ''kama sigara zinaleta kansa mbona fulani alivuta mpaka akazeeka bila kupata kansa. Haya sio mawazo ya mtu aliyeenda shule akaelimika.



Na hapa ndipo linapokuja swali sasa Katiba nzuri ni ipi? Na lengo la Katiba ni nini? Kwa maana kwangu mimi hata katiba hii tuliyonayo ni nzuri pia kwa maana imetumika kuziendeleza nchi nyingi Duniani ambazo leo hii wengi wetu tunazitamani, hivyo swali linabakia kuwa Katiba nzuri ni ipi?
 
Na hapa ndipo linapokuja swali sasa Katiba nzuri ni ipi? Na lengo la Katiba ni nini? Kwa maana kwangu mimi hata katiba hii tuliyonayo ni nzuri pia kwa maana imetumika kuziendeleza nchi nyingi Duniani ambazo leo hii wengi wetu tunazitamani, hivyo swali linabakia kuwa Katiba nzuri ni ipi?
Katiba nzuri ni ile inayotokana na matakwa ya wananchi wengi na inapatikana kwa utaratibu ulio wazi na wa kidemokrasia.
 
Katiba nzuri ni ile inayotokana na matakwa ya wananchi wengi na inapatikana kwa utaratibu ulio wazi na wa kidemokrasia.



Na hapo pia ndipo kosa kubwa lilipo na tunapokosea Waafrika, tunataka kuiga kila kitu bila ya kuelewa haya mambo vizuri!
Unawezaje kusema Katiba nzuri ni ile iliyopatikana kwa matakwa ya Wananchi kwenye nchi kama yetu ambayo nina Uhakika zaidi ya asilimia 75% hawajui hata maana ya Katiba, achilia mbali hata kuliandika neno lenyewe, hayo maoni watayatoaje? Unawezaje kupata maoni kuhusu jambo fulani ktk kwa mtu asiyeelewa hata maana ya hicho kitu anachopaswa kukitolea maoni?

Kuna sababu kwa nini nchi nyingi zilizoendelea zilianza na Katiba kama ya kwetu kwanza, ambapo viongozi ndiyo walikuwa waanaamua na kujenga kwanza msingi na nchi kusimama yaani Elimu kwanza kwa wananchi wote, Afya, Chakula bora cha Uhakika kwa kifupi kuondoa umaskini kwanza kwa wananchi baada hapo sasa baada ya wananchi kuwa na uelewa ndiyo wakaanza na mambo ya haki na usawa kwa wote, sijui kupiga kura kwa wanawake na walemavu na nyongeza nyingine, kwanza haya mambo huja automatic kama wananchi wakishakuwa na mahitaji ya msingi wenyewe huanza kudai mabadiliko kwenye jamii zao lkn TanZania wanaodai mabadilko ya Katiba ni maelite wachache sana, ambao lengo kuu wala siyo kumkomboa MTZ kama ilivyokuwa Kenya bali ni kuingia madarakani!

Sasa sisi tunataka kwenda kinyume na Dunia utakuwa ni muujiza kama tukifanikiwa kwa maana ktk Historia ya Dunia hii hakuna aliyefanikiwa, na ndiyo maana unaona nchi kama Kenya leo hii pmj na kuwa na Katiba kama Marekani lkn hivi juzi wanasiasa wao wameiba Dola bilioni Moja na hii hata wakati wa Chama kimoja haikuwezekana na Katiba mpya haijawazuia watawala kuiba, leo hii Kenya hata wanajadili kufikiria upya madaraka ya Raisi waliyoyaondoa na wanataka kuyarudisha!

Sasa ni kwa nini? Ni kwasababu walianza mbele badala ya nyuma, hivyo hata hapa Tanzania Katiba mpya haitabalisha chochote zaidi ya kuifanya nchi masikini zaidi!

Hivyo mimi nasema tuanze na mambo ambayo yametufanya tushindwe kuendela na kubakia kuwa masikini na ktk haya mambo Katiba haimo, na kubadilisha Katiba hakutasaidia kitu, ushahidi upo Dunia nzima kuanzia Afrika Kusini , Kenya n.k leo hii Mwananchi wa AK ana hali ile ile au si ajabu mbaya zaidi klk wakati AK inaongozwa na Katiba kama yetu!
 
Kwa maana leo hii ukimuuliza Mbongo kwa nini nchi yake masikini unapata jibu haraka Katiba mbovu, kwanini watoto hawasomi jibu Katiba mbovu, kwa nini mafisadi wanaitafuna nchi jibu Katiba mbovu, kwa nini UKIMWI unamaliza watu jibu Katiba mbovu, kwa nini ajali zinamaliza watu jibu Katiba mbovu yaani kila kitu jibu lake ni Katiba mbovu!

Sasa swali langu mkipata hiyo katiba mnayoitaka, mtakuja na singo gani nyingine ya kusingizia?
Najua lazima mtaipata kwa maana historia yetu inatuonyesha hivyo kwamba kila wkt tulikuwa tunatafuta kisingizio cha kushindwa kwetu kuendelea kama jamii nyingine Duniani.

Tulianza na utumwa kwamba watu wetu wenye nguvu waliuzwa utumwani hivyo tukakosa watu wa kufanya kazi ndiyo maana tukawa masikini, ikaja Ukoloni Wazungu walitunyonya wakatuibia kwa kutusainisha mikataba ya kilaghai ndiyo maana tukawa masikini, tukapata Uhuru ikaja Wazungu wanatuibia kwa kutumia Ukoloni mamboleo ndiyo maana tumebakia kuwa masikini, ikaja Globalization wakulima wetu wanashindwa kushindana kwa sababu Wazungu wanasubsidies Wakulima wao ndiyo maana tumebakia masikini!

Sasa hiyo singo imeisha na tumepata nyingine ya Katiba kwamba tuna Katiba mbovu ndiyo maana tumebakia masikini ikumbukwe kwamba hii Katiba inayoitwa mbovu inatumika jamii nyingi Duniani kama Uchina, Singapore, Vietnam, ilitumika kujenga Korea Kusini, ikajenga Taiwan, ikaendeleza Ujerumani, Japan, Uingereza, Chile, Afrika Kusini lkn kwetu imeshindwa,

Sasa swali langu Je hiyo mpya italeta miujiza gani kama kwa miaka zaidi ya 200 ingawaje tuliyoyapitia wengine wameyapitia pia kama Ukoloni, Utumwa, Katiba mbovu lkn leo hii wako mbele sana kiuchumi!
Tatizo hata hiyo katiba yenyewe wanayo dai ni mbovu hawaifahamu, wao wanaskia wanasiasa wa vyama vyao wakiongea baadhi ya vifungu majukwaani pasipo kujua wanasiasa hao wanapigia deme vyama vyao na maslahi yao na sio maendeleo ya nchi hii.
 
Kila rais wa Tanzania anaonekana mwizi, alipoondoka Mwinyi madarakani watu wakasema ndugu zake wa karibu wanafanya biashara chafu. Mkapa naye alipoondoka watu wakaongea sana. Kikwete kaondoka watu wanaongea sana. Magufuli akiondoka naye hatakuwa salama. Hatujawahi kuwa na shukrani kwa viongozi wetu hata kidogo. Huu ni udhaifu wa bara zima la Afrika na sio sisi tu, hivyo sishangai kuwa sababu ya msingi ya mabadiliko ya katiba inayoiona wewe ni kumthibiti rais tu. Hiyo sababu haina nguvu ya kimantiki. Rais ni taasisi yenye majukumu mengi, anaweza kiongozi akawa msafi lakini kazungukwa na wezi. Tuwahurumie marais wetu, tunawabebesha mzigo mkubwa sana wa lawama, tunajenga negative image ya cheo cha urais kitu ambacho sio cha kiungwana.
Mkuu sijui kama ulinisoma vizuri
Katiba ndo kila kitu, katiba ndo inaweka system za utendaji, katiba ndo inamcontrol Rais, katiba ndo inamfanya rais asijifanyie mambo tu atakavyo au anavyojisikia yeye, bila katiba inamaana tunategemea utashi wa Rais tu. Hebu nijibu wewe una maoni gani kwa ile mifano michache niliyotoa kuhusu JK. Nijibu halafu twende sawa
 
Mkuu sijui kama ulinisoma vizuri
Katiba ndo kila kitu, katiba ndo inaweka system za utendaji, katiba ndo inamcontrol Rais, katiba ndo inamfanya rais asijifanyie mambo tu atakavyo au anavyojisikia yeye, bila katiba inamaana tunategemea utashi wa Rais tu. Hebu nijibu wewe una maoni gani kwa ile mifano michache niliyotoa kuhusu JK. Nijibu halafu twende sawa
Ujumbe wangu ni mmoja tu, kila rais anaonekana mwizi dikteta na mambo kama hayo. Magufuli anayesifiwa leo akitoka madarakani watu watamuandama pia. Unaweza kubadilisha katiba na bao usiwe na efficiency, kumbana rais kukawa bado hakujaleta tija yoyote ile. Tuwekeze akili na nguvu zetu nyingi kwenye kuzitumia fursa za kiuchumi na changamoto zilizomo kwenye hizo fursa, tuweke pembeni siasa za katiba na mabadiliko yake, ambazo uzoefu unaonyesha kuwa zinakula muda mwingi ambao ungeweza kutumiwa kwa ajili ya kufanya mambo ambayo ni productive kwa taifa zima
 
Back
Top Bottom