Katiba inasemaje kuhusu asiye mbunge kupeleka hoja binafsi bungeni?

Lukolo

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
5,143
Reaction score
3,199
Wanasheria nisaidieni, mimi siyo mbunge lakini nina hoja kibao ambazo nimejaribu kuziwasilisha kwa wabunge wangu kila mmoja nikimpa ya kwake, lakini mmojawapo aliichakachua, ikakosa nguvu bungeni, na mwingine amekosa ujasiri wa kuiwasilisha kwa kuwa ni CCM, na watatu ni wa upinzani, nimemwandikia wala hajataka kunijibu. Lakini hoja zangu ninaziona ni za msingi na zinahitaji mjadala bungeni na hata nje ya bunge. Je kuna kifungu cha sheria kinachoniruhusu kwenda bungeni kuwasilisha hoja hizo?
 
Hoja yeyote huwasilishwa bungeni na serikali au mbunge hakuna mtu mwingine anaruhusiwa kuwasilisha .Hoja yako mpe mbunge wako .
 
Kwani wananchi hawawezi kutunga bunge lao? Na wakaliita bunge letu wenyewe raia.
Watanzania kuweni wabunifu, musisubiri wabunge na serikali yenu ikufikishieni kila kitu.
Serikali inajua kuuza ardhi zenu musiwe na sehem ya kuishi na kujipatia chakula,
Kuuza bahari yenu musile samaki.

Wabunge, na serikali yenu ni mataptap. Mataptap mbele busara nyuma. Wabunge wenyewe akili zao zenyewe kama akina MAVISAVISA na KING KONG III wa jf.

Ndio maana wengine tumeikimbia nchi, munakuwa watumwa nchini kwenu, kunyanyaswa nchini kwenu looo
 
Hapo ndipo unapokuja umuhimu wa lobbyist/ special interest groups kuwabana wabunge kupeleka hoja bungeni.
An elect tusaidie mtu binafsi atapelekaje hoja bungeni (sio kwenye viwanja vya bunge, ndani ya bunge ijadiliwe). Sijaufahamu utaratibu huu kama upo.
 
Last edited by a moderator:
An elect atuambie ni ibara ipi ktk katiba inaruhusu mtu binafsi kupeleka hoja yake bungeni?
 

An elect atuambie ni ibara ipi ktk katiba inaruhusu mtu binafsi kupeleka hoja yake bungeni?
Dah, naona huyu An elect ameamua kujikausha. Nani mwanasheria mwingine atusaidie. Tundu Lissu hayumo humu JF?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…