Dragunov Sniper
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 2,795
- 9
Fikiri kwanza kabla ya kutenda, No research No Right to speak, Kimya Kingi kina mshindo mkuu. Hii ni baadhi ya misemo inayonifanya nije na usemi kuwa Katiba Inayopendekezwa Haizuiliki. Nimeisoma kwa kina na utulivu, nikafuatilia mijadala mbali mbali kuhusu katiba hii nikaona kuwa walio wengi na wenye mapenzi mema na nchi hii hawawezi kuikataa katiba Inayopendekezwa. It is really very unique, in the sense that it has taken into consideration almost every group of people as Dr. Kikwete puts it; INATAMBUA watu wenye ulemavu, wavuvi, wafugaji, watoto, wazee, vijana hadi Baraza la vijana,wasanii na wanawake ndio kabisaa. Wanawake wamepewa haki ya kumiliki ardhi suala ambalo lilikuwa kama ndoto kwa baadhi ya makabila. Kweli ni Katiba inayojali maslahi ya walio wengi na ya Taifa kwa ujumla. Katiba imeweka miiko ya vionngozi kama ilivyokuwa katika enzi za Azimio la Arusha. Sasa wewe unakataa Katiba hii ili upate ipi.
Kweli sasa imefika wakati Watanzania tukomae na kufanya maamuzi ya kiutu uzima. Tuache ushabiki wa vyama, imani na itikadi mbali mbali. Tuzidi kuisoma katiba Inayopendekezwa, nakushukuru Dada yangu Daktari Asha Rose Migiro kwa kutugawia hizo nakala. Sasa hata tukisema tupige kura tutapigia kitu tunachokifahamu. Kama mtu mmoja alivyosema UKITAKA KUJUA UHONDO WA NGOMA UINGIE UCHEZE. Nawe ukitaka kuipigia kura Katiba Inayopendekezwa uisome. Kwa walio na ujuzi wa mambo ya mitandao, katiba hiyo imo, soma hata kwa kupitia simu yako ya kiganjani.
Kutokana na uzuri niliouona kwenye Katiba Inayopendekezwa nami nasema kama Joshua alivyosema CHAGUENI SASA NANI WA KUMTUMIKIA, MIMI NA NYUMBA YANGU TUTAMTUMIKIA BWANA, kwa note hiyo hiyo nami nadriki kusema kuwa CHAGUENI SASA LA KUFANYA, MIMI NA NYUMBA YANGU NA WATANZANIA WENYE AKILI TIMAMU NA WAZALENDO TUTAIPIGIA KURA YA NDIYO KATIBA INAYOPENDEKEZWA.
ASANTENI KWA KUNIUNGA MKONO WAZALENDO WENZANGU.
Hivi kwa nini usiingie katika historia ya Nchi hii kupitisha Katiba Inayopendekezwa!!! MUNGU IBARIKI TANZANIA