Dragunov Sniper
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 2,795
- 9
Kwa mara ya wanza katika historia hapa nchini kwetu, Katiba Inayopendekezwa katika IBARA YA 4-(4) LUGHA YA TAIFA NA MAWASILIANO MBADALA tunaona kuwa Katiba hiyo imewajali watu wenye ulemavu wakiwemo viziwi, bubu n.k kwa kuziweka lugha zao za utambulisho zikiwemo lugha ya alama, lugha ya alama mguso, maandishi yaliyokuzwa na nukta nundu kwenye sehemu muhimu za umma na katika vyombo vya habari vinavyotangaza habari zake kitaifa kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
kutokana na hili, Serikali itaweka mazingira yatakayowezesha kuwepo kwa mawasiliano mbadala kwa watu hao na jamii.
Jamani hata hili nalo hamlioni kuwa ni jambo jema kwa wenzetu wenye ulemavu mpaka tuiseme hii katiba haifai? Itakuwa dhambi na kufuru kuisemea vibaya, nashauri Watanzania wenzangu tuwe wazalendo na tuisome hii katiba na tutagundua mambo mengi mazuri yalojificha ambayo baadhi ya watu wamekuwa wakiyananga kupitia baadhi ya wanasiasa wasioitakia mema nchi hiii.
Nawasilisha.