Kwani majina ya mtu yanakuwa kwenye paji ya uso wake, shati zake na suruali zake? Tunaweza kutambua ni katiba ya viongozi tawala kwa sababu ndio walioondoa maadili ya viongozi: (1) uadilifu, (2) uwajibikaji na (3) uwazi. Wangewezaje kuyaingiza hayo wakati wameharibu? Kesi ya ngedere anapelekewa nyani!!
Ndio hao wenye akaunti nje zenye pesa chafu wakiongozwa na mzee wa vijisenti. Kuhusu zuio la kuweka pesa ng'ambo ya nchi wanasema: Sheria zitatungwa za namna ya kuweka fedha nje. Kwani ni watanzania wangapi wa kawaida wanaweza kuweka fedha nje ya nchi? Hao wanaokula mlo mmoja?
Tuache ushabiki, nchi hii ni yetu sote.