Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,703
- 1,724
Kwa mara nyingine napenda kuungana na Watanzania wenye mapenzi MEMA kuhusu Muungano wetu kuwapongeza wajumbe wote wa tume ya kutunga katiba ya Jamhuri ya Muungano, wengi tumefurahishwa hasa katika muundo MUAFAKA wa muungano wetu na vilevile pongezi maalum zimuendee mwenyekiti wake ambaye hachoki kufafanua maoni ya wananchi wengi kuhusiana na muundo huu.Ninacho omba sasa tume hii itakapo tunga KATIBA isituchanganye wananchi kwa kutaja Tanganyika mara Tanzania Bara kama ilivofanya kwenye rasimu yake, angalia vifungu hivi. SURA YA KWANZA SEHEMU YA KWANZA; Mipaka, Alama, Lugha,Utamaduni na Tunu za Taifa:- 1 (1)- Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambao kabla ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi huru. 2 - Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara ikijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la Zanzibar ikijumuisha sehemu yake ya bahari. 3 (2)- Sikukuu za Kitaifa zitakuwa ni; (a) Siku ya Uhuru wa Tanganyika, itakayoadhimishwa tarehe 9 Disemba, (c) Siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, itakayoadhimishwa tarehe 26 Aprili. SURA YA SITA; Muundo wa Jamhuri ya Muungano:- 57 (1) Jamhuri ya Muungano itakuwa na muundo wa shirikisho lenye serikali tatu ambazo ni (a) Serikali ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, (b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na (c) Serikali ya Tanzania Bara.(3) Muundo, madaraka na mambo mengine ya kiutendaji yahusuyo Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yataainishwa katika Katiba za Washiriki wa Muungano. My take:-Ikiwa sura ya kwanza inatamka kuwa Jamhuri ya Muungano ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar sasa hili jina la Tanzania Bara la NINI? Ni kutubabaisha tu.