kimjaacho mtu ndo kinachotoka hii mboga kawaulize wa kwenu jana na leo asubuhi wamekula ya wapi?ukimaliza uliza mkeo kakupikia ya wapi vile!
Hao viongozi wanaopora madaraka yako wewe mwananchi umewaona wapi TAnzania?wanayapora kutoka wapi?kwani mamlaka ya viongozi wa Tanzania especially rais wetu yanatoka kwa nani?hivi mpaka sasa hujajua tu Wananchi ndo mamlaka yenyewe!Madaraka na mamlaka ya hao viongozi tunawapa sisi kikatiba kama hujui hiyo ni kazi nyingine ukisema wamekupora sikuelewi?Pia kuna Bunge/ wananchi ambalo linafanya kazi yake kutunga sheria na kupitisha mambo mbalimbali,Rais lazima awe na mamlaka yaliyoainishwa Kikatiba na si vinginevyo na ndiyo maana anaitwa Rais asipokuwa na mamlaka sio Rais huyo!!! Sasa wewe unaposema hatuna mfumo wa kushughulikia uvunjaji wa sheria za nchi kwa kiongozi endapo amethibitika kutenda makosa ya kuvunja Katiba nchi ambayo aliapa kuilinda na kuitetea sikuelewi, Tatizo lako unaendeshwa kwa hisia hapa!
hapa ndipo huelewi maana ya madaraka ya wananchi.
kupora madaraka ya wananchi inaweza kutokea kwa njia nyingi lakini moja wapo ni pale wananchi wanapokosa udhibiti wa watumishi wao, wanakosa udhibiti wa mali zao na wakabaki kulalamika tu na hawana la kufanya.
wananchi wenye madaraka yao wanaogopwa na viongozi wao kutokufanya kinyume na wananchi wanavyotaka.
wananchi walioporwa madaraka linapotokea tatizo lolote wanaamini viongozi wao watakaloamua ndio mwisho.
ki msingi baadhi ya madaraka ya wananchi yamekasimiwa kwa chombo chao ambacho ni bunge hivyo ukisikia chombo chao kinalalamika kuwa serikali imezoea kukaidi maagizo ya bunge ujue chombo hicho hakina madaraka tena ya kusimamia kama katiba inavyosema.
kimsingi raisi na seriakali zikipewa madaraka makubwa wanao uwezo wa kupora madaraka ya wananchi na kuanza kufanya wao wanavyotaka na wananchi wanakuwa hawana la kufanya.
sijui wewe madaraka ya wananchi unayozungumza ni yapi?
Unaruka moto afu unakanyaga tena we vipi wananchi ndo mamlaka ya mwisho unaposema wanaporwa hueleweki????
hoja hapa sio porojo bali uonyeshe kwa vipi ?
Siongea na walevi km wewe wasio na hoja. UMEKALILISHWA kojoa lala tena usingizi wa asbh ni mtamu pia kwa watoto km wewe
Nani anasema kuwa tunataka katiba isiyompa mamlaka raisi? Au unataka awe na mamlaka ya kuingilia ndoa yako?Kuna baadhi ya watu fulani wamekuwa na hasira kuhusu mamlaka ya Rais yaliyoanishwa kwenye Katiba Inayopendekezwa ile Sura ya nane,Kuanzia Ibara ya 80 mpaka 98. Watu hao wamefikia hatua ya kutaka apunguziwe mamlaka huku wengine hasira zao zikipitiliza wakitaka hata yale aliyonayo yaondolewe yote kabisa abaki kama mtumishi wa kawaida!
Jambo la kunishangaza ni pale watu hao wanaposhindwa kuelewa kuwa mamlaka au heshima ya mfalme ni wingi wa watu wake!wanashindwa kuelewa kuwa Mamlaka ya Rais ni wingi wa kura zake,hawezi kulinganishwa na mtu yeyote katika nchi na Katiba Inayopendekezwa ambayo wananchi wataipigia kura imelizingatia hili.
Kwa mujibu wa Katiba ya 1977 Tanzania tunao utaratibu wa kumpata Rais kupitia sanduku la kura (nguvu ya umma) ambazo humpa Mamlaka ya kuongoza na kutawala.Rais ni Mkuu wa Nchi,kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.
Kwa Tanzania Rais ni alama na taswira ya Jamhuri ya Muungano na watu wake na pia ni alama ya umoja ,uhuru wa nchi na mamlaka yake!
Sasa inawezekanaje Kiongozi Mkuu wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama vya nchi ukataka alinganishwe na mjumbe au mbunge au waziri? Hilo haliwezekani fuatilia nchi zote ambazo wamekubali upuuzi huu utaona marais wao ni kama mapambo tu na wana jina lao eti wanabaki kuwa Ceremonial hawana mamlaka ya maamuZi ya nchi wapo wapo tu, hili halikubaliki Tanzania Rais ni MAMLAKA hata UKAWA wanalijua hili ndo maana wanajaribu kuungana wakiamini kuwa watashinda nafasi ya Urais nao wawe na kiongozi mwenye mamlaka katika nchi.
Mungu Ibariki Tanzania!
Nawasilisha!
Rais wa nchi ndo kiongozi mkiu wa nchi na amiri jeshi mkuu na hapo unasemaje?
Hujajibu swali langu. Nini kitakachotokea rais mteule akitokea chama A halafu chama chenye wabunge wengi bungeni ni chama B? Rais atachagua waziri mkuu na mawaziri wengine kutokea chama kipi? Je bunge litawakubali hao mawaziri? Watashirikiana nao vema?Nyie wanaCCM tatizo lenu mnadhani kwamba mko peke yenu nchi hii na kwamba upinzani haukui. Think again!Tunataka katiba imara inayoangalia all posibilities ili iweze kukaa as long as possible bila kubadilishwa. Katiba ni sacred!Huna hoja hapa wala huelewi ndo walewale Rais abaki Amiri jeshi mkuu Nonsense!!! Then what nini utendaji wake katika Serikali hujaisoma Katiba ya 1977 na hii Inayopendekezwa hujaisoma nenda kasome tena kwa kuelewa acha kutumika!
Hujajibu swali langu. Nini kitakachotokea rais mteule akitokea chama A halafu chama chenye wabunge wengi bungeni ni chama B? Rais atachagua waziri mkuu na mawaziri wengine kutokea chama kipi? Je bunge litawakubali hao mawaziri? Watashirikiana nao vema?Nyie wanaCCM tatizo lenu mnadhani kwamba mko peke yenu nchi hii na kwamba upinzani haukui. Think again!Tunataka katiba imara inayoangalia all posibilities ili iweze kukaa as long as possible bila kubadilishwa. Katiba ni sacred!
Hujajibu swali langu. Nini kitakachotokea rais mteule akitokea chama A halafu chama chenye wabunge wengi bungeni ni chama B? Rais atachagua waziri mkuu na mawaziri wengine kutokea chama kipi? Je bunge litawakubali hao mawaziri? Watashirikiana nao vema?Nyie wanaCCM tatizo lenu mnadhani kwamba mko peke yenu nchi hii na kwamba upinzani haukui. Think again!Tunataka katiba imara inayoangalia all posibilities ili iweze kukaa as long as possible bila kubadilishwa. Katiba ni sacred!
sio tu kukaa bila kubadilishwa bali kuna jambo linatutafuna nchi hii sana.
watu wanaunda makundi ya kusaka uraisi na hapa wapo watendaji wazuri katika makundi haya lakini wapo wahuni tu watoto wa mjini wanaokaa vijiweni kusikiliza dili, ziwe za utapeli au nini na wao wanajiingiza katika makundi haya na kupiga kelele kama nini.
wananyemelea nafasi alizopewa raisi za uteuzi na akipata hawa hawana utaalamu wowote wao wanatafuta pa kupigia dili.
wakikaa nyuma mtu ni vigumu kuwageuka hawa fitina na kila kitu kichafu wanakijua na hawa ndio wamekuwa chimbuko kubwa la utendaji mbovu wa serikali nyingi zinazolea mifumo ya kuwaingiza watu wajanjanja tu kwenye uongozi.
tutengeneze mifumo ambayo raisi akichaguliwa kwanza kuna vyombo vya kuangalia anayoyafanya na hawa wahuni waone kuwa hawana nafasi.
hebu angalia mashirika ya serikali yanavyokufa, hivi kweli hapa tanzania kuna mtu binafsi mtanzania wa kuwa na mtaji kuliko serikali yetu? kama hakuna iweje watu binafsi wapate watendaji bora na waendeshe makampuni kwa faida na mashirika ya serikali yanakufa?
jibu la haya yote ni kuweka uongozi wa nchi katika mihimili mitatu na mtendaji yeyote anayeingia katika utendaji wa umma anaona akifanya uzembe au ndivyo sivyo wapo wa kumbana.
tunaposema kuzuia mtu mmoja ua kundi la watu kushikilia vyombo vyote kimsingi haina maana ya kusema huyu akitoka kundi hili basi yule atoke kundi lile.
hapa ni kila chombo kuwa na mambo yake na yanayojitegemea na kundi la watu au mtu fulani lisiwe na ushawishi au maamuzi ya moja kwa moja katika chombo au mhimili mmoja usiwe na peremende au bakora za kuwanyamazisha au kuwashughulikia mihimili mingine. na tutafute jinsi ya kufanya uongozi wa juu kwa kila chombo cha juu kiutawala kuwajibika kwa wananchi hivyo wanachombo wakati wote wanajua wanatakiwa kuwaridhisha wananchi.
hapo inakuwa haijalishi watendaji wanatoka wapi.
Nani anasema kuwa tunataka katiba isiyompa mamlaka raisi? Au unataka awe na mamlaka ya kuingilia ndoa yako?
....inayompa rais madaraka ya kuteua mpaka mkuu wa wilaya baada ya kushauriana na 'kamati ya uteuzi' anayoiteua mwenyewe baada ya kushauriana na wasaidizi wake anaowateua mwenyewe pia!?Lukindo, kweli hayo maneno aliyatoa Mwl. ndiyo maana alisistiza Kiongozi wa nchi ni lazima awe na msimamo unaoongozwa na misingi ya katiba ya nchi katika kutoa maamuzi.
Nakushangaa Lukindo kwa kusema Nafikiri unachotaka kutwambia ni kuwa rais akiamka asubuhi na kuamua kuahirisha uchaguzi mkuu iwe sawa tu maana ana mamlaka hayo! Usituambie unafikiri, soma Katiba inasema je?Ndiyo maana Baba wa Taifa alikemea tabia hiyo.Maneno yako uliyoyasema sii ya kikatiba bali ni mawazo yako ambayo hayapo kwenye Katiba ya nchi, hivyo nasisitiza kuwa nchi inaongozwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo kulingana na Katiba ya nchi na sii vinginevyo.
Mzee unaongea nini hasa maana una mambo kibao afu mchanganyiko!nikuulize swali hivi Tz hakuna mihimili 3?
Hii sio debate.. Utakuwa na tatizo kama utaiita hii ni debate.. Ndo maana ckupata shida kuandika niliyoyaandika.. Ungemsaidia kumjibia kwa kutaja hizo nchi ambazo zimeathirika kwa mfumo huu wa kupunguziwa madaraka..
Vinginevyo huna sababu ya msingi ya kuandika ulichoandika..
Nikicheck avatar yako tu nakuelewa wewe ni mtu wa namna gani!!! Hata sipati shida ya kuargue na wewe maana nafasi ya Urais katika nchi hujaielewa vizuri.