sio tu kukaa bila kubadilishwa bali kuna jambo linatutafuna nchi hii sana.
watu wanaunda makundi ya kusaka uraisi na hapa wapo watendaji wazuri katika makundi haya lakini wapo wahuni tu watoto wa mjini wanaokaa vijiweni kusikiliza dili, ziwe za utapeli au nini na wao wanajiingiza katika makundi haya na kupiga kelele kama nini.
wananyemelea nafasi alizopewa raisi za uteuzi na akipata hawa hawana utaalamu wowote wao wanatafuta pa kupigia dili.
wakikaa nyuma mtu ni vigumu kuwageuka hawa fitina na kila kitu kichafu wanakijua na hawa ndio wamekuwa chimbuko kubwa la utendaji mbovu wa serikali nyingi zinazolea mifumo ya kuwaingiza watu wajanjanja tu kwenye uongozi.
tutengeneze mifumo ambayo raisi akichaguliwa kwanza kuna vyombo vya kuangalia anayoyafanya na hawa wahuni waone kuwa hawana nafasi.
hebu angalia mashirika ya serikali yanavyokufa, hivi kweli hapa tanzania kuna mtu binafsi mtanzania wa kuwa na mtaji kuliko serikali yetu? kama hakuna iweje watu binafsi wapate watendaji bora na waendeshe makampuni kwa faida na mashirika ya serikali yanakufa?
jibu la haya yote ni kuweka uongozi wa nchi katika mihimili mitatu na mtendaji yeyote anayeingia katika utendaji wa umma anaona akifanya uzembe au ndivyo sivyo wapo wa kumbana.
tunaposema kuzuia mtu mmoja ua kundi la watu kushikilia vyombo vyote kimsingi haina maana ya kusema huyu akitoka kundi hili basi yule atoke kundi lile.
hapa ni kila chombo kuwa na mambo yake na yanayojitegemea na kundi la watu au mtu fulani lisiwe na ushawishi au maamuzi ya moja kwa moja katika chombo au mhimili mmoja usiwe na peremende au bakora za kuwanyamazisha au kuwashughulikia mihimili mingine. na tutafute jinsi ya kufanya uongozi wa juu kwa kila chombo cha juu kiutawala kuwajibika kwa wananchi hivyo wanachombo wakati wote wanajua wanatakiwa kuwaridhisha wananchi.
hapo inakuwa haijalishi watendaji wanatoka wapi.
Hujajibu swali langu. Nini kitakachotokea rais mteule akitokea chama A halafu chama chenye wabunge wengi bungeni ni chama B? Rais atachagua waziri mkuu na mawaziri wengine kutokea chama kipi? Je bunge litawakubali hao mawaziri? Watashirikiana nao vema?Nyie wanaCCM tatizo lenu mnadhani kwamba mko peke yenu nchi hii na kwamba upinzani haukui. Think again!Tunataka katiba imara inayoangalia all posibilities ili iweze kukaa as long as possible bila kubadilishwa. Katiba ni sacred!