Kuweka tumaini kubwa kwenye katiba kwamba ndio itamaliza matatizo yetu yote, ni kujidanganya.
Sina hakika na siamini kama vyama vyetu vyenyewe ikiwa katiba zao zimetoa nafasi kwa viongozi wake wawe ni wa kudumu na kwamba hawawezi kutoka mpaka waseme basi,, Si kweli, zaidi sana wanakosa kitu kinaliwa UZALENDO!
Katiba ni sheria mama, ambayo kawaida ndio hutoa adhabu ya nini mtu apewe kulingana na makosa aliyofanya kikatiba, lakini katiba siyo dawa ya mtu kumfanya awe mzalendo!
Uzalendo ni zaidi ya Katiba! Tufanyeje hapa!
Katiba ni suluhisho la kudhiibiti mianya iliyowazi kwa iliyopo sasa na kuwafanya matapeli wengi wa kikatiba kuacha utapeli wao
Katiba haiwezi kushindana na uzalendo ikashinda!
Kama watu kwenda jela kwa sababu wameiba, bado wapo na hawataisha licha kwamba hata hii katiba iliyopo imetoa adhabu kali.
Kama watu kubuni mbinu za kuiba kura licha kwamba kuna katiba yenye meno kama msumeno, wataendelea!
Kwa nchi za wenzetu, mtu kuhusishwa tu na wizi na ama sikendo chafu juu yake, hata kama katiba haitaji makosa hayo kuwa ni uhaini, ataachia madaraka na saa nyingine atajiona ni mtu bure katika jamii hiyo!
Tufanyeje ili katiba sasa ije na dawa ya uzalendo kwa Taifa? Ama tuwafundishe kwanza watoto wetu uzalendo kwa nchi yao ndio tuwe na Katiba?
Ni kipi kilipaswa kianze badala ya mwenzake.