Katiba kicheko vyama vyote

Katiba kicheko vyama vyote

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,925
upinzani_katiba.jpg


Serikali inatarajia kuandaa hati ya dharura ili kuwezesha kufanyika kwa maboresho ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba ambayo yatajadiliwa upya katika Mkutano wa Bunge unaoanza Oktoba 29 mjini Dodoma.

Tayari vyama vya upinzani na chama tawala vimekubaliana taratibu muhimu za kufuata ili maboresho hayo yaweze kupita ndani ya Bunge. Muswada huo haukuwa umepangwa kujadiliwa katika mkutano ujao wa Bunge ndio maana itabidi iombwe hati hiyo ya dharura. Hatua hiyo ni ushindi kwa vyama vitatu vya upinzani vya Chadema, CUF na NCCR- Mageuzi, ambavyo vilipinga muswada huo wakati wa mkutano uliopita wa Bunge Septemba, mwaka huu.

Muswada wa sheria hiyo uliopitishwa Septemba na Bunge ulisusiwa na wabunge wa vyama hivyo wa upinzani kwa maelezo kuwa una kasoro kwenye baadhi ya vipengele.

Hata hivyo, wabunge wa CCM waliamua kuendelea na mjadala na kupitisha muswada huo kitendo ambacho kilisababisha mvutano mkubwa uliomfanya Rais Jakaya Kikwete kukutana na viongozi wa vyama vya siasa vyenye wabunge kumaliza tofauti zao.

Mbatia asoma tamko la vyama

Akisoma tamko la vyama vya siasa mbele ya waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema hatua ya Serikali itakuja baada ya vyama vya siasa kufikia mwafaka wa vipengele vinavyotakiwa kufanyiwa marekebisho kwenye muswada huo. Mbatia alisema kuwa tayari kazi hiyo imefanyika na mapendekezo yao yameshapelekwa serikalini ingawa hakutaka kuingia kwa undani walichopendekeza katika marekebisho hayo.

Vyama vilivyokutana ni pamoja na CCM, Chadema, CUF, NCCR -Mageuzi, TLP. Pia vyama vya UDP na UPDP vilishiriki kwa niaba ya vyama visivyo na wabunge.

Mbatia alisema hatua inayofuata ni vyama kuunda kamati yao na Serikali kuunda yake ili kukubaliana kwa pamoja maeneo muhimu ya marekebisho.

Alisema lengo la hatua hiyo ni kuufanya mchakato wa Katiba kuwa shirikishi baada ya kamati hizo kumaliza kazi yake.

"Baada ya hapo, Serikali itaandaa hati ya dharura ili marekebisho yapelekwe haraka katika Mkutano wa Bunge unaoanza Oktoba 29, " aliongeza Mbatia.

Mbatia alisema wanataka kabla ya Bunge la Katiba halijaanza basi sheria husika ifanyiwe marekebisho. "Tunawaomba Watanzania hasa wabunge waunge mkono juhudi hizi za vyama na Serikali ili kuhakikisha mchakato wa Katiba Mpya unakuwa shirikishi. Wabunge waridhie marekebisho haya na kuyapitisha," alisema mbunge h
uyo wa kuteuliwa na Rais.

JK awapa goli wapinzani

CCM, ambayo wabunge wake walipitisha muswada kwa kauli moja, iliweka kando tofauti zake za kiitikadi na kimtizamo na kuungana na Chadema, CUF, NCCR- Mageuzi na vyama vingine vya upinzani.

Kitendo hicho cha CCM kilikuja baada ya Rais Kikwete kukutana na viongozi wa vyama vya siasa vyenye wabunge na vile visivyokuwa na wabunge, wiki iliyopita na kuvitaka vyama hivyo kukaa pamoja na kutoa mapendekezo ili yafanyiwe kazi na Serikali.

Kitendo hicho ni sawa na ushindi wa vyama vya upinzani kwani pamoja na kuwa wabunge wachache tofauti na CCM bado Rais Kikwete aliamua kusikiliza hoja zao.

CCM na Chadema damu damu

Katika hatua ya kuashiria kuwa vyama hivyo viko bega kwa bega, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangula na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa walishikana mikono pamoja na viongozi wengine watano wa vyama vya siasa na kutoa tamko la pamoja kuhusu kuboresha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

Tukio hilo la aina yake lilifanyika jana na kuongozwa na Mbatia, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania ambacho kilipewa jukumu na Rais kuratibu ukusanyaji wa maoni ya maboresho ya muswada huo.

Mangula alipoulizwa kama wabunge wa CCM watakuwa tayari kupitisha maboresho ya sheria hiyo itakaporejeshwa tena bungeni alisema kwa kifupi; "Siwezi kuwasemea wabunge wa CCM."

Alipobanwa zaidi kuhusu ushiriki wa CCM kwenye umoja wa vyama hivyo. Alisema: "CCM haijawahi kuandaa rasimu yake ya Katiba, ila nachojua ni kwamba kila chama kilipewa nafasi na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoa maoni yake na CCM ni miongoni mwa vyama hivyo. Katiba Mpya ni kitu kizuri kwa taifa letu."

Serikali yakubali ombi la tume

Serikali imekubali ombi la Tume ya Mabadiliko ya Katiba la kuongezewa muda wa mwezi mmoja kutokana na ugumu wa kazi ya uchambuzi wa maoni yaliyotolewa na wananchi na asasi mbalimbali.

Habari zilizopatikana kutoka vyanzo vya habari ndani ya Serikali na kuthibitishwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe zilisema kuwa awali kabla ya kuomba muda huo, tume hiyo ilikutana na Rais Kikwete ili kuomba kuongezewa muda.

Maana yake ni kuwa Tume hiyo iliyoanza kazi Mei Mosi, mwaka jana ilitakiwa kukamilisha kazi yake Novemba Mosi, mwaka huu hivyo sasa kazi yake itakamilika Desemba. Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana, Chikawe alisema, " Kwa nini wakataliwe kama wanaona muda hauwatoshi." Kwa mujibu wa Waziri Chikawe, muda waliomba unakubalika kisheria na kwamba wanaweza kuongezewa hadi miezi miwili.

Alipoulizwa kama haoni muda huo utasababisha kuchelewesha mchakato mzima wa Katiba, Waziri Chikawe alisema, haoni kama kuongezwa kwa muda huo kutaathiri chochote. "Nataka kuwahakikishia Watanzania hakuna haja ya kuwa na wasiwasi mchakato utaendelea kama kawaida kitakachoongezeka ni mwezi mmoja hivyo badala ya rasimu ya pili kukabidhiwa kwa Rais Novemba sasa itaenda mpaka Desemba,"alisema Waziri Chikawe.

Imeandikwa na Tausi Mbowe, Fidelis Butahe na Editha Majura.

Chanzo: Mwananchi

 
"Katiba bora inakuja Tanzania kwa sababu Rais Kikwete amesikiliza malalamiko ya vyama vya upinzani". Kweli?.

The draft constitution doomed to failure, before the Constitutional Review Commission (CRC) even start.

attachment.php

Viongozi wa vyama vya Siasa,(kushoto)Isaack Cheyo(UDP) Nancy Mrikaria(TLP) Fahmi Nassoro Dovutwa (UPDP),James Mbatia NCCR-Mageuzi,Profesa Ibrahim Lipumba(CUF),Philip Mangula(CCM) na Dk Willibrod Slaa(Chadema)wakiwa wameshikana mikono baada ya kikao cha pamoja jijini Dar es Salaam jana.
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    33 KB · Views: 1,592
hapo tutawaelewa ila bado bungeni hawa wabunge wao ni vigeugeu
 
hiki ndicho tukipendacho watanzania mshikamane ktk mambo ya kitaifa !!!big up kikwete naomba fanya na babu seya atoke basi .kaz kwenu wabunge wa ccm mliojivunia wingi wenu bungen kupitisha kasoro za kuliangamiza taifa !!!jk uko juu sana na dhamira yko ya kwel ya kuleta katiba bora imejidhihirisha !!!!
 
"Katiba bora inakuja Tanzania kwa sababu Rais Kikwete amesikiliza malalamiko ya vyama vya upinzani". Kweli?.

The draft constitution doomed to failure, before the Constitutional Review Commission (CRC) even start.

attachment.php

Viongozi wa vyama vya Siasa,(kushoto)Isaack Cheyo(UDP) Nancy Mrikaria(TLP) Fahmi Nassoro Dovutwa (UPDP),James Mbatia NCCR-Mageuzi,Profesa Ibrahim Lipumba(CUF),Philip Mangula(CCM) na Dk Willibrod Slaa(Chadema)wakiwa wameshikana mikono baada ya kikao cha pamoja jijini Dar es Salaam jana.
Wale wote wasioitakia mema nchi yetu roho zao zinawauma sana, hongera sana JK. Unaweka historia.
 
Good MOVE; Wasiwasi wangu ni kwa Wabunge wa CCM na hasa Naibu Spika, aliyejaa kiburi, majivuno na kila aina ya Ulevi wa Madaraka. Wabunge wa CCM wasitumie uwingi wao kukwamisha marekebisho haya. Ikibidi uwekwe utaratibu ili tuwajue wanaopinga na watakaopinga marekebisho haya. Katiba ni Waatanzania.

Ahsanteni sana Wanamageuzi, Ahsante sana Rais kwa DHAMIRA yako njema juu ya KATIBA MPYA YA TANZANIA
 
hofu ya Mungu ikitawala, watawala hutenda haki. Mungu ibariki Tz
 
namsifu JK na serikali yake kwa haya maamuzi....
sasa niwakati wa Le Mutuz kufanya maamuzi magumu ya kurudisha card ya CCM kwa "wenyewe"
 
Wale wote wasioitakia mema nchi yetu roho zao zinawauma sana, hongera sana JK. Unaweka historia.
Mtu asiyeitakia mema Tanzania atakuwa ni 'shetwani'.

Mkuu Ritz , historia ni matukio yaliyopita na katika matukio hayo unaweza kupata matukio mabaya na mazuri.

Ni kweli Rais Kikwete ana andika historia lakini historia anayoiandika itakuja kumhukumu negatively baadaye katika maisha yake.

Swala la muungano ambalo kwa sasa liko kwenye centre stage katika mchakato huu mbovu ndilo litakalo muhukumu negatively Rais Kikwete.

Mchakato wa katiba umeanza hata bila kuridhia kama wananchi wanataka muungano, serikali mbili au tatu badala yake wanalazimishwa na Rais Kikwete, Tume ya Katiba na vyama vya siasa kwa kuchaguliwa aina ya serikali.

Bora Katiba itapatikana 2015+ lakini baada ya muda, tutarudi tena hapa Jf kuanza debate ya mchakato wa marekebisho ya katiba baada ya muungano wa serikali mbili au tatu wanazolazimishwa wananchi kusarambatika.
 
'Kijani na njano" walikataa nini na sasa wanaenda kupitisha nini!!
 
Ritz
===>Hivi hawa wabunge wenu (CCM) huwa wanafikiria nini wanapokuwa pale bungeni?
===>Spika (naibu) hajisikii aibu kuona muswada huu unarudishwa tena bungeni kwa marekebisho?
===>Wabunge wenu hawajisikii vibaya kuona mnapitisha mambo ambayo hayana tija kwa watanzania kama mlivyopiyisha kodi ya line za simu?
 
Last edited by a moderator:
Inahitaji uwe mwendawazimu kuishabikia masisiem!!
 
Ritz
===>Hivi hawa wabunge wenu (CCM) huwa wanafikiria nini wanapokuwa pale bungeni?
===>Spika (naibu) hajisikii aibu kuona muswada huu unarudishwa tena bungeni kwa marekebisho?
===>Wabunge wenu hawajisikii vibaya kuona mnapitisha mambo ambayo hayana tija kwa watanzania kama mlivyopiyisha kodi ya line za simu?
Rais Kikwete alishaweka signature yake kisheria na kubadilisha mswada kuwa sheria. Kile kilichopitishwa na wabunge kwa sasa ni sheria

Hakuna mswada unaorudishwa bungeni labda kama hufahamu maana ya mswada na sheria.

Kwa kukusaidia zaidi, haya ni maboresho zaidi ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya Sheria za Tanzania ambayo ilipitishwa 2012 kama yalivyokubaliwa na Rais Kikwete alipokutana na viongozi wa upinzani 21/01/2012 Ikulu Dar.
CHADEMA-Ikulu-leo.jpg
 
Ng'wamapalala
Rais Kikwete alishaweka signature yake kisheria na kubadilisha mswada kuwa sheria. Kile kilichopitishwa na wabunge kwa sasa ni sheria

Hakuna mswada unaorudishwa bungeni labda kama hufahamu maana ya mswada na sheria.

Kwa kukusaidia zaidi, haya ni maboresho zaidi ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya Sheria za Tanzania ambayo ilipitishwa 2012 kama yalivyokubaliwa na Rais Kikwete alipokutana na viongozi wa upinzani 21/01/2012 Ikulu Dar.
===>Hata mkisema au kutoa ufanunuzi wa aina gani,bado wabunge wa CCM wameonyesha udhaifu na upeo mdogo sana wa kimawazo,ni wabinafsi sana na wanafikiria kujaza matumbo yao na familia zao tu.
 
Kumbukumbu tumezihifadhi kwamba tangu mwanzo, maCCM mnaburuzwa katika suala zima la Katiba mpya.
 
Big up JK, Huwa nayakubali sana maamuzi ya JK kama haya.Tatizo ni kwamba anao watu wengi ambao hawaitendei haki nchi.
 
Back
Top Bottom