Ntale Wi Isumbi
JF-Expert Member
- Apr 4, 2012
- 480
- 127
Mwanzo mzuri, taratibu karibu tunaanza kuweka pembeni tofauti zetu za kiitikadi kwenye mambo muhimu ya Taifa. Hongereni wabunge na viongozi wa CDM, NCCR-Mageuzi na CUF kwa kuonyesha njia hata pale mlipotukanwa na kubezwa. Hongera JK kwa kuwa 'msikivu' anglau kwa hili la Katiba Mpya. Natumaini wabunge wa sisiemu na mawaziri hususan chikawe, wasira na lukuvi watakuwa wamejifunza kitu kutokana na hili. Nasi tunasubiri kuona na kusikia mlichojifunza na ukomavu wenu kuanzia Octoba 29 kule mjengoni.