Kama kuna kitu ambacho wapenda mabadiliko nchini wanapaswa kujitolea kwa nguvu zao zote ni upatikanaji wa katiba mpya ya nchi kwanza.
Katiba ndio ingini ya kuleta mabadiliko, huwezi kuleta mabadiliko nje ya katiba ya nchi. Katiba safi ya nchi ndo itakayozalisha tume safi ya uchaguzi, viongozi safi, uchumi safi, matumizi safi na maisha bora kwa kila mtu.
Wapinzani kukubali kushiriki kwenye uchaguzi kwa kutumia katiba ya zamani ni sawa na kukubali kushindwa uchaguzi kabla ya uchaguzi. Kushiriki uchaguzi kwa kutumia katiba hii ya zamani ni sawa na kuhalalisha wananchi kuwasindikiza watu wachache kupata ubunge na udiwani usiokuwa na tija kwa wanachi walio wengi.
Wabunge wa aina hii huwa wananufaika wao tu na familia zao kwakuwa hawawezi kuleta mabadiliko yenye manufaa mapana kwenye majimbo yao.
Wakijitahidi saaaana watawaletea wananchi wao bahashishi ndogo ndogo tu kama soda, madawati, computers mashuleni, kitanda kimoja labor ward, n.k. Kwa uchache wao hawawezi kuchangia kuinua hali za maisha ya wanajimbo hata kama wangekuwa na utashi wa kufanya hivyo. Hoja zao bungeni zinazimwa kama mshumaa unavyozimwa.
kushiriki uchaguzi kwa kutumia katiba mpya kunazalisha hasara kubwa kwa wananchi kuliko faida. Jasho la wananchi wanaoshiriki kuzalisha wabunge na madiwani wachache tu kwenye vyombo vya maamuzi huwa halirudi. Vyama vya upinzani acheni kuwatumia wananchi kama mitaji yenu na familia zenu huku mkifahamu katiba iliyoko haiwezi kuwapatia wananchi mabadiliko wanayoyataka.
Ni bora vyama vya siasa kuacha kushiriki chaguzi nchini ya katiba hii sasa ili kuepuka kuwatumia wananchi ambao makusudi yao ni tofauti na wanachokipata baada baada ya uchaguzi.