CHADEMA wamejipambanua wazi wazi ya kuwa nini wanataka. Agenda yao ya uhuru, usawa na haki haipendezi sana miongoni mwa madhulumati na wanufaika wa hali iliyopo sasa.
Rais Samia kajipambanua kuwa hataki dhuluma bali anataka usawa na haki kwa wote. Mama ameonyesha utayari wa kuonana na makundi mbalimbali, vyama vya siasa nk. Mama hayuko mbali sana kimsimamo na Chadema.
Ni wazi kuwa wahafidhina na wanufaika wa bakshish za hali iliyopo hawajafurahishwa na misimamo yake mingi ikiwamo hii.
Wahafidhina hawa wanaomzunguka kwa kila upande, ndiyo lililo tatizo kuu. Wao wamejipanga vilivyo "piga ua" kumfanya mama kubadili mingi ya misimamo yake.
Wamechagua hata kumfarakanisha Mama kwa vyovyote, na kwa yeyote, na kwa lolote (hata kama ni la kijinga). Wanajaribu hata kumwunganisha na JK lengo likuwa kumfitinisha Mama.
Mzee Warioba yalimkuta hata akawekwa vibao hadharani walipohisi kuhatarishwa kwa maslahi yao:
Chokochoko za kuhusu mradi wa Bagamoyo, safari za Mama nje ya nchi, misimamo mipya dhidi ya Corona, chanjo, nk yote ni katika kufanikisha mifarakano hiyo.
Dhidi ya CHADEMA wamejipanga vilivyo kuhakikisha kuwa, Mama hakutani nao kwa namna yoyote ile. Ni nia yao kuona mkutano wowote baina ya CHADEMA na Mama hautakaa ufanyike.
Ni wazi kuwa kwa kukutana tu, Mama angeweza kupata picha tofauti kabisa na matango pori anayolishwa kwa makusudi kuhusu Chadema na kila uchao.
Nchi hii ni yetu sote. Tatizo si Mama, bali ni hawa wahafidhina na hila zao. Suluhu ya hapa tulipo ni kwa mama kuchanganya na za kwake kwenye akili anazoambiwa.
Hata hivyo Mama kesha jipambanua:
Mama si sehemu ya ufedhuli.
Kwenye mazingira haya uchaguzi (option) pekee wa haki na unaobakia ni kwa Chadema kuendelea kudai mustakabala mpya wa katiba na kwa nguvu zaidi.
Katiba ni yetu sisi wananchi. Hatutaki kuendelea kubambikiziwa kesi, hatutaki dhuluma, hatutaki kubebeshwa mizigo ya kodi ya wengine, tunataka mihimili ya utawala iliyo na huru kamili, tunataka usawa, tunataka uwajibikaji, tunataka mawazo yetu kusikilizwa nk.
Haya si ya kupuuzwa tena wala hayawezi kuendelea kusubirishwa bila ukomo.
Amandla!
Ninawasilisha.