Katiba Mpya: CHADEMA wana Options zipi?

Katiba Mpya: CHADEMA wana Options zipi?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
CHADEMA wamejipambanua wazi wazi ya kuwa nini wanataka. Agenda yao ya uhuru, usawa na haki haipendezi sana miongoni mwa madhulumati na wanufaika wa hali iliyopo sasa.

Rais Samia kajipambanua kuwa hataki dhuluma bali anataka usawa na haki kwa wote. Mama ameonyesha utayari wa kuonana na makundi mbalimbali, vyama vya siasa nk. Mama hayuko mbali sana kimsimamo na Chadema.

Ni wazi kuwa wahafidhina na wanufaika wa bakshish za hali iliyopo hawajafurahishwa na misimamo yake mingi ikiwamo hii.

Wahafidhina hawa wanaomzunguka kwa kila upande, ndiyo lililo tatizo kuu. Wao wamejipanga vilivyo "piga ua" kumfanya mama kubadili mingi ya misimamo yake.

Wamechagua hata kumfarakanisha Mama kwa vyovyote, na kwa yeyote, na kwa lolote (hata kama ni la kijinga). Wanajaribu hata kumwunganisha na JK lengo likuwa kumfitinisha Mama.

Mzee Warioba yalimkuta hata akawekwa vibao hadharani walipohisi kuhatarishwa kwa maslahi yao:

IMG_20210704_080147_886.jpg

Chokochoko za kuhusu mradi wa Bagamoyo, safari za Mama nje ya nchi, misimamo mipya dhidi ya Corona, chanjo, nk yote ni katika kufanikisha mifarakano hiyo.

Dhidi ya CHADEMA wamejipanga vilivyo kuhakikisha kuwa, Mama hakutani nao kwa namna yoyote ile. Ni nia yao kuona mkutano wowote baina ya CHADEMA na Mama hautakaa ufanyike.

IMG_20210704_051559_619.jpg

Ni wazi kuwa kwa kukutana tu, Mama angeweza kupata picha tofauti kabisa na matango pori anayolishwa kwa makusudi kuhusu Chadema na kila uchao.

Nchi hii ni yetu sote. Tatizo si Mama, bali ni hawa wahafidhina na hila zao. Suluhu ya hapa tulipo ni kwa mama kuchanganya na za kwake kwenye akili anazoambiwa.

Hata hivyo Mama kesha jipambanua:

IMG_20210610_103030_594.jpg

Mama si sehemu ya ufedhuli.

Kwenye mazingira haya uchaguzi (option) pekee wa haki na unaobakia ni kwa Chadema kuendelea kudai mustakabala mpya wa katiba na kwa nguvu zaidi.

Katiba ni yetu sisi wananchi. Hatutaki kuendelea kubambikiziwa kesi, hatutaki dhuluma, hatutaki kubebeshwa mizigo ya kodi ya wengine, tunataka mihimili ya utawala iliyo na huru kamili, tunataka usawa, tunataka uwajibikaji, tunataka mawazo yetu kusikilizwa nk.

Haya si ya kupuuzwa tena wala hayawezi kuendelea kusubirishwa bila ukomo.

Amandla!

Ninawasilisha.
 
Our country is going through a state of extraordinary poignancy; this is a monumental disappointment to Bi Mkubwa and all her hypocritical allies.
 
Our country if going through a state of extraordinary poignancy; this is a monumental disappointment to Bi Mkubwa and all her hypocritical allies.

Akili za kuambiwa na akachanganye za kwake. Alipo anazungukwa na wenye kukaanga mbuyu.

They are very guilty:

They can only listen to the language of violence. We are getting there.
 
CHADEMA wamejipambanua wazi wazi ya kuwa nini wanataka. Agenda yao ya uhuru, usawa na haki haipendezi sana miongoni mwa madhulumati na wanufaika wa hali iliyopo sasa.

Rais Samia kajipambanua kuwa hataki dhuluma bali anataka usawa na haki kwa wote. Mama ameonyesha utayari wa kuonana na makundi mbalimbali, vyama vya siasa nk. Mama hayuko mbali sana kimsimamo na Chadema.

Ni wazi kuwa wahafidhina na wanufaika wa bakshish za hali iliyopo hawajafurahishwa na misimamo yake mingi ikiwamo hii.

Wahafidhina hawa wanaomzunguka kwa kila upande, ndiyo lililo tatizo kuu. Wao wamejipanga vilivyo "piga ua" kumfanya mama kubadili mingi ya misimamo yake.

Wamechagua hata kumfarakanisha Mama kwa vyovyote, na kwa yeyote, na kwa lolote (hata kama ni la kijinga). Wanajaribu hata kumwunganisha na JK ili kumfitinisha Mama.

Mzee Warioba yalimkuta hata akamwekwa vibao hadharani walipohisi kuhatarishwa kwa maslahi yao:

View attachment 1839617

Chokochoko za kuhusu mradi wa Bagamoyo, safari za Mama nje ya nchi, misimamo mipya dhidi ya Corona vikiwamo ugonjwa na chanjo, nk yote ni katika kufanikisha mifarakano hiyo.

Dhidi ya CHADEMA wamejipanga vilivyo kuhakikisha kuwa, Mama hakutani nao kwa namna yoyote ile. Ni nia yao kuona mkutano wowote baina ya CHADEMA na Mama hautakaa ufanyike.

View attachment 1839607

Ni wazi kuwa kwa kukutana tu, Mama angeweza kupata picha tofauti kabisa na matango pori anayolishwa kwa makusudi kuhusu Chadema na kila uchao.

Nchi hii ni yetu sote. Tatizo si Mama. bali hila za wahafidhina. Suluhu ya hapa tulipo ni kwa mama kuchanganya na za kwake kwenye akili anazoambiwa. Hata hivyo Mama kesha jipambanua:

View attachment 1839602

Mama si sehemu ya ufedhuli huo.

Kwenye mazingira haya uchaguzi (option) pekee wa haki na unaobakia ni kwa Chadema kuendelea kudai mustakabala mpya wa katiba na kwa nguvu zaidi.

Katiba ni yetu sisi wananchi. Hatutaki kuendelea kubambikiziwa kesi, hatutaki dhuluma, hatutaki kubebeshwa mizigo ya kodi ya wengine, tunataka mihimili ya utawala iliyo na huru kamili, tunataka usawa, tunataka uwajibikaji, tunataka mawazo yetu kusikilizwa nk. Haya si ya kupuuzwa tena. Hayawezi kuendelea kusubirishwa tena na bila ukomo.

Amandla!

Ninawasilisha.

Cc: BAK Missile of the Nation JokaKuu Pascal Mayalla johnthebaptist
Umechanganua vizuri. Bado naamini Rais SSH ana nia nzuri ya kukutana na vyama vya upinzani na hilo litatokea.

Kwa upande wa CHADEMA wanapiteza muelekeo kama ifuatavyo:
1. Wanampangia Rais aanze kukutana nao wao kabla ya makundi mengine. Kila uchao Rais akikutana na kundi fulani wao wanaona wamepuuzwa.

2. CHADEMA wanataka wakutane wao kama Chama na siyo kupitia UMOJA wa Vyama vya upinzani. Wao wanajiona ndiyo wapinzani halisi wa Serikali.

3. Kadri Rais anapochelewa kuwaita ndiyo kauli za kifedhuli zinazidi kuongezeka kutoka kwa Mbowe, Lissu na hivi karibuni Mdude

4. Wanataka Katiba Mpya kama kipaumbele wakti Rais ana vipaumbele vyake na vya Chama chake hususan kuimarisha uchumi.

Nawashauri watulize bongo chini waweke mikakati mipya
 
Tulipo tunahitaji busara zaidi za wastaafu hasa JK. Tuliwahi kutafuta busara zake kwenye sakata la umakamu. Kuna haja ya kutafuta busara zake kwenye hili pia:

Ikibidi Chadema waangalie uwezekano wa kuonana JK. Huyu ni mwingi wa busara na mwuungwana. Zaidi sana wahafidhina anawamudu.

Vinginevyo tuko njiani tunaelekea njia panda.

Cc: Stuxnet Mmawia imhotep
 
Barua uliandika umoja wa vyama?
Rais aliwajibu umoja wa vyama?
Au hukuelewa kuwa Chadema wamejibiwa na Rais kuhusu barua yao
 
Umechanganua vizuri. Bado naamini Rais SSH ana nia nzuri ya kukutana na vyama vya upinzani na hilo litatokea.

Kwa upande wa CHADEMA wanapiteza muelekeo kama ifuatavyo:
1. Wanampangia Rais aanze kukutana nao wao kabla ya makundi mengine. Kila uchao Rais akikutana na kundi fulani wao wanaona wamepuuzwa.

2. CHADEMA wanataka wakutane wao kama Chama na siyo kupitia UMOJA wa Vyama vya upinzani. Wao wanajiona ndiyo wapinzani halisi wa Serikali.

3. Kadri Rais anapochelewa kuwaita ndiyo kauli za kifedhuli zinazidi kuongezeka kutoka kwa Mbowe, Lissu na hivi karibuni Mdude

4. Wanataka Katiba Mpya kama kipaumbele wakti Rais ana vipaumbele vyake na vya Chama chake hususan kuimarisha uchumi.

Nawashauri watulize bongo chini waweke mikakati mipya

La kheri kutambua kuwa mchanganuo umetulia. Hata hivyo nisiache kukujibu na hata kuendelea kukazia:

1. Mama Samia ana nia njema ya dhati ya kuona haki, usawa na uhuru wa watu vina tamalaki.
2. Mama ana nia njema ya kukutana na makundi yote yakiwamo Chadema ambapo Mama alishathibitisha hilo kwa barua.
3. Mitizamo ya Mama na Chadema kimsingi haiko tofauti, wala Chadema haina tatizo na Mama.
4. Yote #1 - #3 ni mwiba mchungu mno kwa wahafidhina wa CCM waliopo pia serikalini, ambapo wengine wao ni watuhumiwa wa maovu katika awamu ile.
5. Wahafidhina hawa lengo lao ni kuhakikisha misimamo na ajenda za mwendazake zinaendelea bila mwendazake.
6. Wahafidhina hawa wanamshinikiza Mama kuendelea kuzuia mikutano ya kisiasa na kuchelewesha pasipo kikomo kurejelewa kwa mchakato wa katiba mpya.
7. Wahafidhina hawako tayari kuona mkutano wa Mama na Chadema ukifanyika. Kufanikisha hilo wamepanga kuuchelewesha bila ukomo, wakitegemea uvumilivu Chadema utawashinda.
8. Mama ana nia njema ila wahafidhina hawa wana nia ovu sana. Katuni hii nisiache kuiweka tena kwani inaeleza zaidi hali ilivyo:

IMG_20210704_051559_619.jpg

Yaangalie macho ya Mama hapo vizuri na waangalie wahafidhina, kuuelewa mchezo mzima.
9. Mama hawezi kuwamudu mahafidhina hawa peke yake. Wamechagua kumfarakanisha yeye katika hali zote. JK angeweza kumsaidia kuwadhibiti kwani wote anawamudu.
11. Chadema wanataka katiba mpya, lakini kwa kuzuia pia mikutano ya kawaida ya kisiasa limeweka wazi zaidi nia ovu ya wahafidhina hawa.
12. Mama angeruhusu mikutano ya kisiasa, hata akaonyesha tu uwezekano wa lini anaweza kuonana nao na pengine akaahidi chaguzi 2024/25 zitakuwa ni kwa mujibu wa katiba mpya, Chadema wasingeona katiba mpya ni kipaumbele. Kumbuka mikutano ya kisiasa ni halali kwa mujibu wa katiba.
13. Wa kulaumiwa kwenye kadhia hii si Chadema. Ifahamike kuwa Chadema wanabeba ajenda ya hata wasiokuwa wanachama wao kudai haki ya uwepo wa mikutano na katiba mpya.
14. #13 inawapa Chadema uhalali wa kumwona Mama peke yao. Pia uwepo wa vyama vilivyo washirika wa CCM ambao aghalabu wanawasiliana na hata kukutana mara zote wanakutana na Mama na Chadema kwa ajenda ipi ya pamoja?

Namshauri Mama akili za kuambiwa achanganye na za kwake. Kumshirikisha JK kwa mawazo si unyonge. Hii ngoma inakoelekea si kwenyewe.

Auvae ujasiri wa kuwadhibiti mahafidhina hawa. Asisahau wengine baina yao walitaka kumzima urais wake. Wengine wanataka kuchukua nafasi yake 2025. Kimsingi wengi wao hawampendi na hata ni watuhumiwa wa maovu ya awamu ile.

Cc: BAK johnthebaptist Yoda
 
Hapana,nikumchonganisha na Rais.
Tafsiri itakuwa mbaya pande zote mbili

Kwanini tukimbilie busara nje wakati hazina ipo?

Anatakikana mtu wa kuwadhibiti wahafidhina. Inafahamika bila Kikwette palikuwa na kimbembe kwenye transition (awamu 5 - 6) na hata kwenye u makamu pia.

Hata hapa kwa mawazo ya watu kama Kikwette, tungevuka salama pasipo na haja ya makabiliano yasiyo kuwa na tija.
 
Back
Top Bottom