Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
Tusiyopenda kuyasikia kwenye Elimu ya Uraia.
Kimsingi madai ya Katiba mpya kwa minajili ya kushika nafasi ya urais naamini ni ndoto isiyotimia kwa vizazi vingi vijavyo. Uki-study historia mahala pengi utakubaliana nami kwamba madai ya Katiba mpya siyo kwa ajili ya wanaogombea urais kuingia Ikulu bali ni kwa ajili ya kuleta mfumo mzuri wa jamii imara iliyoshikamana kwa malengo maridhawa.
Katiba mpya imewaingiza wagombea wapya Ikulu kwa asilima ndogo sana sana isiyostahili wingi wa madai hayo na isiyoakisi gharama halisi za mchakato wa kuandika Katiba mpya hizo.
Kwa uelewa wangu, Rais hapelekwi Ikulu kwa Katiba mpya, Rais anapelekwa Ikulu kwa mfumo wa Dola (vetting ya dola), Katiba mpya na mfumo wa uchaguzi vinawapa tu wapigakura uwezo wa kuwapeleka wabunge Bungeni, Madiwani Halmashauri na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji basi. Katiba hata ikiwa mpya haiwapi wapigakura (wananchi) uwezo wa kumpeleka Rais Ikulu. Huu ndiyo uhalisia wa Afrika. Thought stirring discourse.