Siyo kosa kabisa mkuu.
Charles Njonjo alipotaka kumng'oa mzee Jomo Kenyatta akaenda kum-consult babake kwanza. Babake akamwambia ebu fungua jokofu hilo hapo, chukuwa kipande cha nyama mpe paka, Charles akafanya hivyo, paka alivyoanza kukila mzee Njonjo akamwambia Charles ebu sasa mnyang'anye paka hicho kipande cha nyama kabla hajakimaliza, Charles akasema haiwezekani, mzee Njonjo akamuuliza kwanini haiwezekani, Charles akajibu paka atanidhuru. Mzee Njonjo akamwambia Charles sawasawa kabisa kumbe umeelewa somo, sasa ukitaka kumnyang'anya mzee Jomo Kenyatta urais jiandae kudhuriwa. Mimi simo! Charles akapanda ndege kurudi London akaghairi mpango huo. Nimefafanua kifasihi zaidi.